Na; Elizabeth Paulo, Dodoma 


Mamlaka ya Serikali Mtandao e-GA imesema wanapambana kuhakikisha mifumo yote muhimu inatengenezwa na inafanya kazi ili kuendelea kuiunga mkono serikali katika jitihada za kuhakikisha sayansi,teknolojia na ubunifu unatumika kwa faida na kuongeza uchumi wa taifa.


Ni vyema jamii ikatumia Mifumo ya ndani ya nchi yakimawasiliano ili kurahisisha kutoa huduma Kwa haraka na kuratibu shughuli za kimawasiliano Kwa kupiga simu Kwa Taasisi mbalimbali za umma.


Akizungumza na waandishi Wa Habari katika kilele Cha Maadhimisho ya wiki ya Ubunifu kitaifa Jijini Dodoma Afisa TEHAMA Wa Mamlaka ya serikali Mtandao Tumaini Masinsi Amesema Mfumo huo ni mahususi kwa ajili kuongeza ufanisi wakuhudumia wananchi wenye malalamiko, maulizo mapendekezo, na pongezi.



Tunachokifanya ni kuhakikisha tunaleta suluhisho katika matatizo na kupunguza gharama zinazotumika kutekeleza shughuli mbalimbali za serikali na Taasisi zake kwa kubuni mifumo wezeshi ambayo inarahisisha muda na inafanyika kwa ufanisi mkubwa


Katika Maonyesho hayo Mamlaka ya Serikali Mtandao eGA wamepata nafasi ya kuonesha bunifu mpya nane ambazo tayari zimeanza kufanya kazi na zimesaidia kuboresha utendaji katika sekta mbalimbali hapa nchini.



1.Intergrated CallCenter System & CRM


Ni mfumo wa kuratibu shughuli za kimawasiliano kwa kupiga simu kwa Taasisi mbalimbali za Umma.


Mfumo huu ni mahususi kwa ajili kuongeza ufanisi wakuhudumia wananchi wenye malalamiko, maulizo mapendekezo, na pongezi


2.ChatAI


Ni ubunifu unaotumia teknolojia ya akili bandia kusaidia Mamlaka ya Serikali Mtandao kujibu maswali ya mara kwa mara kuhusiana na utendaji kazi wa Mamlaka. Mfumo huu unapatikana kupitia ega.bot.all.co.tz



3.Alphachain Blockchain Network


Ni ubunifu wa ndani wa mtandao wa blockchain unaohimiza matumizi ya mtandao wa blockchain kutengenza mifumo mbalimbali.

4.Sec doc


Ni ubunifu wa mtandao unaotokana na teknolojia ya blockchain yenye malengo ya kuongeza ulinzi kwenye matumizi na utumaji wa nyaraka mbalimbali.



5.eMrejesho


Ni mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi kwenda kwa taasisi mbalimbali za umma. Mfumo huu unapatika kwa njia ya web “eMrejesho.gov.go.tz” njia ya mobile application kwa Playstore na Applestore kwa jina la mrejesho pia kwa njia ya msimbo *152*00# kisha namba 9, kisha namba 2.



6.EBoard


Ni mfumo wa kuratibu vikao vya bodi na kamati zake, menejimenti na kamati zake pamoja na madiwani.

Mfumo huu umekua suluhu kubwa katika kupunguza gharama za utendaji kazi kwenye eneo hili la vikao.


7.Oxygen


Ni ubunifu wa mtandao wa kijamii wenye usalama wa hali ya juu ulioundwa kwa lengo la kufanya mawasiliano kwa message, voice calls pamoja na video calls. Mtandao huu unapatikana kwa njia ya web na mobile application kwa android na IOS.



8.RSS


Ni ubunifu wa teknolojia unaofanania na TeamView na Anydesk, unaruhusu ku share skrini za kompyuta kwa watu walio kwenye maeneo tofauti ya ki jeographia, pia unaruhusu utumaji na upokeaji wa ma faili mbali mbali kwa njia ya kielectroni.


Kwa upande wake Afisa TEHAMA Wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi Wa umma na utawala Bora Osea laizer Amesema bunifu hizo zimelenga kusaidia makundi mbalimbali wakiwemo watumishi Wa umma.


Maonesho ya wiki ya Ubunifu Tanzania mwaka 2023 yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na kushirikisha na Taasisi za Elimu ya Juu, Taasisi za Utafiti na Maendeleo, Vyuo vya Ufundi, Mashirika na Taasisi za Umma, Mashirika na Taasisi binafsi za teknolojia, Wizara mbalimbali na Wabunifu walioendeleza katika programu ya MAKISATU na kufikia hatua ya ubiasharishaji.



Lengo likiwa ni kuwakutanisha wabunifu mbalimbali ambapo wanatumia maonesho hayo kama jukwaa la kuonesha bidhaa zao mpya ambazo wamezibuni kupitia Taasisi zao ili jamii ione na kuvichukuwa kwa ajili ya kwenda kuvitumia kwa kutatua changamoto zao na kurahisisha utendaji katika shughuli za kila siku.



PICHA NA OFISI YA MAMLAKA YA SERIKALI MTANDAO 


Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: