Na John Walter-Babati


Mbunge wa jimbo la Babati vijijini Mhe. Daniel Sillo amekabidhi mabati 160 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la ofisi ya kijiji cha Duru kata ya Duru Wilayani Babati mkoani Manyara ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa hapo awali.

 

Katika tukio hilo pia Mhe. Sillo amesikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa kata hiyo na kuahidi kuzifanyia ufumbuzi ambapo baadhi yake tayari kazi imeanza.

 

Katika hatua nyingine wananchi wa kata hiyo wameshukuru kwa namna ambavyo mbunge huyo amekuwa akitekeleza ahadi zake ikiwemo usambazaji wa mashine za photocopy na kompyuta mpakato mashuleni zilizosaidia kufufua ufaulu wa wanafunzi mfano mzuri ukiwa ni shule ya  Haitemba Sekondari iliyopanda na kushika nafasi ya 8 kiwilaya na ya 23 kimkoa.

 

Ikiwa pia ni muendelezo wa utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi CCM Mhe. Sillo ameeleza mpango madhubuti wa kutatua changamoto ya maji na barabara kwa uchimbaji wa visima na ujenzi wa barabara mbalimbali kwa kiwango cha changarawe na madaraja likiwemo lile la kwa Hawu lililopo kata ya  Duru lililokumbwa na uharibifu mkubwa ambalo ujenzi wake unaanza hivi karibuni.

 

Mhe. Sillo pia amekabidhi katiba za chama cha mapinduzi CCM kwa matawi yote ya chama katika kata hiyo.

 

 

Share To:

Post A Comment: