Na. Benedict Mlawa wa Jeshi la Polisi 


Jeshi la Polisi kupitia Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF-NET) limeshiriki katika kuadhimisha sherehe ya siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Machi 08, 2023 Wilayani Kondoa Jijini Dodoma.Maadimisho hayo yameongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ambaye ameongoza viogozi wa Kiserikali, Chama, Vyombo vya Ulinzi na Usalam, Taasisi , Mashirika, Dini Pamoja na Wananchi katika kuadhimisha ya siku ya Wanawake Duniani aambapo kimkoa yameadhimishwa katika Wilaya ya Kondoa.Senyamule aliwashukuru na kuwapongeza viongozi na wakazi wa Wilaya ya Kondoa kwa maandalizi mazuri waliyoyafanya kwa kuupokea ugeni mzima wa mkoa wa Dodoma katika wilaya hiyo huku akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Daktari Samia Suluhu Hassan kwa kuwa chachu ya mafanikio kwa Wanawake hapa nchini kwa kuamini kwamba Wanawake wanaweza hata ukiangalia katika uteuzi wake waviongozi, wanawake wamepewa nafasi kwa kuamini usawa wa Kijinsia.


Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa aliwataka wanawake kujitokeza na kuzifanyia kazi fursa mbalimbali ambazo zinatolewa na serikali ili kuweza kufikia malengo ya Usawa wa Kijinsia kwa maendeleo endelevu.


Kadhalika Senyamule aliongeza kwa kusema Jamii lazima izingatie haki za watoto wa kike kwa kumlinda mtoto wa kike dhidi ya ndoa za utotoni ili aweze kufikia na kufaidi huduma za jamii ikiwa ni pamoja na kupata elimu yenye kuwezesha kudai na kumlinda mtoto wa kike dhidi ya Ukatili wa Kijinsia.


Sambamba na hayo Mkuu wa Mkoa aliwatunuku zawadi wanafunzi mbalimbali wa Wilaya zote za Jiji la Dodoma waliofanya vizuri kwa kupata ufaulu wa (DIVISION 1) katika mitihani yao ya Mwisho ya kidato cha nne mwaka 2022.Maadhimisho haya yamebebwa na kauli mbiu isemayo “Ubunifu na Mabadiliko ya Technolojia, chachu katika kuleta Usawa wa Kijinsia”


Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: