Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange ameagiza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha kupeleka timu maalum ya uchunguzi katika hospitali ya wilaya wilaya Arusha “Oltrument” kuchunguza upotevu wa mapato kupitia mfumo kukusanya mapato(GoTHOMIS) na upotevu wa dawa.

Ametoa maelekezo hayo leo tarehe 08 Machi 2023 wakati akikagua utoaji wa huduma za afya katika hospitali ya wilaya ya Oltrument mkoni Arusha na kubaini changamoto katika usimamizi wa hospitali.

Wakati akikagua utoaji wa huduma za afya, Dkt. Dugange amebaini upotevu wa fedha za mapato ya hospitali ambapo mfumo kukusanya mapato na kutunza taarifa za wagojwa (GoTHOMIS) hautumiki kwa zaidi ya miaka miwili.

“Ukusanyaji wa Mapato ya ndani ya hospitali hauridhishi ikilinganishwa na huduma na wagojwa wanaouhumiwa katika hospitali hii kutokana na kutotumika kwa mifumo kwa zaidi ya miaka miwili” ameswma Dkt. Dugange

Aidha, Dkt. Dugange amebaini upotevu wa dawa ambapo taratibu za ununuzi, upokeaji, utunzaji na utoaji wa dawa kwa wagojwa hazifuatwi na kupelekea dawa kupotea.

Ameagiza timu maalum ya uchunguzi ihakikishe ifikapo tarehe 15 Aprili 2023 iwe imekamilisha uchunguzi na kuwasikisha taarifa Ofisi ya Rais TAMISEMI ili hatua za kisheria zichukuliwe kwa wahuska watakaobainika.

Vile vile, Dkt. Dugange amemuagiza Mganga mkuu wa wilaya kuhakikisha ifikapo tarehe 05 Aprili 2023 hospitali iwe imefanya mpangilio na kurekebusha kasoro zote zilizobainika katika haspitali hiyo ikiwa ni pamoja na kutumia mfumo wa (GoTHOMIS).Share To:

Post A Comment: