Meneja wa uwanja wa CCM  Mkwakwani Nassoro Makau 'Nassa' akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya fainali ya mchezo wa kombe Shirikisho la Azam utakaochezwa katika dimba hilo.

Na Denis Chambi,  Tanga.

Mkoa wa Tanga umepokea kwa furaha kubwa taarifa za  kutangazwa kuwa mchezo wa fainali  ya kombe la Shirikisho la Azam   utachezwa katika dimba la CCM Mkwakwani kwa  msimu huu wa 2022/2023.

Meneja wa uwanja CCM Mkwakwani Nassoro Makau 'Nassa' alisema wamepokea kwa bashasha taarifa hizo kuona kwamba uwanja wao unakidhi vigezo vya  kuchezwa fainali hizo huku akiahidi kwenda kuyafanyia marekebisho baadhi ya maeneo ambayo bado hayajakaa sawa kulingana na hadhi ya mashindano hayo.

"Hii ni fursa kubwa sana ambapo tunategemea kupata mashabiki wengi kutoka wilaya za mkoa wetu na kutoka  mikoa mingine  tofauti tofauti kuja kuangalia fainali hii katika mkoa wetu wa Tanga kwetu ni fursa kubwa , kuna viwanja vingi sana lakini huu ndio umechaguliwa hatuwezi kukubali fursa hii itupite"

" Toka kuanza kutangazwa kwa uwaja wa Mkwakwani kwetu huu ni mkakati namba moja kwa maana ya kwamba zile sehemu zote ambazo ni korofi  kwa upande wetu sisi tunapaswa kuzishughulikia ipasavyo katika eneo la Pitch  tutaendelea kuliboresha  na mengine  kwa sababu fainali hii ni kubwa tutakaa kama kamati  kuona baadhi ya maeneo gani ambayo tuweza kuanza nayo  lakini pia kuyashughulikia ndani ya wakati" alisema Nassa.

Alisema kuwa  licha ya wapezi mashabiki na wadau wa soka kupokea taarifa hizo kwa furaha itakuwa  pia ni fursa ya kipekee siku hiyo  itakayofungu mlango kwa watu mbalimbali ikiwemo   wafanyabiashara kutokana na uwepo wa watu tofauti wa kutoka nje na ndani ya mkoa huo.

"Licha ya Mashabiki wengi kuja Mkwakwani kushuhudia fainali hizi lakini pia ni fursa kwa watu wengine wakiwemo wafanyabiashara,  watu wa usafiri,  wauzaji wa vyakula pamoja  na wengineo wengi kila mwana Tanga kwa namna yake ni fursa kwake. Alisema Nassa.

Hatua ya robo fainali ambayo itaanza kuchezwa March 31  hadi april 2,2023 kwa timu ta Simba SC kukutana na Ihefu , Azam FC  wao watachuana na Mtibwa Sugar Singida wakiminyana Mbeya City na  mchezo wa mwisho utawakutanisha Yanga SC dhidi ya Geita Gold kutafuta tiketi ya kutinga nusu fainali..  
Share To:

Post A Comment: