Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu ametoa rai kwa Watanzania kuendelea kujilinda na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa kufuata miongozo ya watalaam ikiwemo kupunguza vitu kama chumvi, mafuta na sukari katika vyakula.

Waziri Ummy Mwalimu ameyasema hayo katika mdahalo wa Space katika mitandao wa Kijamii ulioandaliwa na kampuni ya Mwananchi juu ya miaka miwili ya Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu.

Ambapo akizungumza katika mdahalo huo, aliweza pia jibu maswali mbali mbali hususani magonjwa ya Afya ya Akili.

"Changamoto kubwa kwa sasa hivi ni ongezeko ya magonjwa yasiyo kuambiza kama saratani, moyo na mengine, 

Pia magonjwa ya figo, na ni gharama kubwa sana kuyatibu.

Punguzeni chumvi, sukati na mafuta ilikujilinda na magonjwa hayo yasiyo ya kuambukiza, ili nimewekea mkazo sana ilituende kulimaliza,

Lakini pia tunaenda kuimarisha Afya ya Jamii mfano Afya ya Akili, magonjwa yasiyo ya kuambukiza, uzazi na mengine," amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy Mwalimu pia amesifu huduma bora za Kibingwa ikiwemo za upandikizaji wa figo, na upandikizaji wa puto, ambazo zimeanza kufanyika nchini ndani ya miaka miwili ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Share To:

Post A Comment: