Na,Imma Msumba ; Arumeru

Kamati ya Siasa Mkoa wa Arusha yaridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapindizi (CCM) katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Wilayani Arumeru ambapo mbali na fedha za zinatolewa na Serikali kuu, Halmashauri hiyo kupitia mapato yake ya ndani kwa mwaka wa fedha2022\/2023  unaoendelea imetoa zaidi Milioni 935.5 za utekelezaji wa  Miradi ya Maendeleo.

Akizungumza wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha Ndg. Zelothe Steven Zelothe amesema ameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye sekta ya afya na elimu katika Halmashauri ya Meru ambapo kamati hiyo ya  siasa Mkoa imeona thamani ya fedha kwenye miradi hiyo.

Aidha, Zelothe ameshauri ni vema  Halmashauri hiyo kuendelea  kuwashirikisha wananchi wakati wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwa  ni pamoja na utoaji wa taarifa za miradi ili kuwajengea uelewaa wa pamoja ikiwa ni pamoja\nKutatua  changamoto za wananchi .

Nae, Katibu wa CCM Mkoa  wa Arusha Bwn.Musa Matoroka amewataka wataalamu wa Halmashauri  kufanya ukaguzi wa mara kwa mara  wa  miradi ili kuongeza nguvu katika usimamizi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe.Jeremia Kishili amesema Halmashauri hiyo itaendelea kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani ili fedha zaidi zipatikane katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na wananchi waweze kupata maendeleo.

Kwa upande wake Mwl.Zainabu Makwinya ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru amesema katika kuwaletea wananchi maendeleo Halmashauri hiyo itahakikisha  inasimamia  na kupeleka  fedha za utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa mujibu wa muongozo.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Mhe.John Mongella amesema, serikali itaendelea kusimamia miradi yote ya maendeleo ili fedha zinazotolewa na serikali zipate thamani yake kwenye miradi hiyo na kuweza kusogeza huduma bora zaidi kwa wananchi.
Share To:

Post A Comment: