-Moshi, Kilimanjaro

Katika hatua kubwa inayolenga kuleta mapinduzi kwenye soko huria na kumlinda Mlaji. Mamlaka ya Ushindani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACCA) zimekutana Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro leo Aprili 23, 2026 na kuwaapisha rasmi wajumbe wapya wanne kutoka Nchi za Tanzania, Somalia, Uganda na DRC ambao watasimamia mazingira mazuri ya ushindani wa biashara na walaji kwa Jumuiya hiyo.

Wajumbe hao walioapishwa kuanza safari ya miaka minne ya uongozi ni Bi. Khadija Ngasongwa (Tanzania), Bw. Zackey Kalega (Uganda), Bw. Ahmed Warsame (Somalia) na Bw. Dolly Kenga (DRC).

Akizungumza mara baada ya kuapishwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC), Bi. Khadija Ngasongwa amesema kuwa watahakikisha mazingira mazuri ya biashara yanakuwepo kwa wafanyabiashara wa Jumuiya hiyo pamoja na kulinda walaji wa jumuiya dhidi ya mbinu potofu sokoni

Aliongeza kuwa wamepewa dhamana ya kusimamia sera na sheria zinazolinda ushindani wa biashara na kuwatetea watumiaji kote katika kanda ya Afrika Mashariki.

Kuapishwa kwa makamishna hawa nchini Tanzania kunakuja katika kipindi mwafaka ambapo biashara kati ya nchi wanachama inazidi kushamiri, jambo linalohitaji mwamuzi imara wa kati. Mamlaka hii sasa inatarajiwa kuwa mlinzi mkuu wa walaji. Uwepo wa safu hii mpya ya uongozi unatoa ishara kwa wawekezaji wa kimataifa kuwa ukanda wa Afrika Mashariki sasa umekomaa kisheria na uko tayari kwa biashara yenye uwazi na ushindani wa kimataifa.

Mamlaka hii inafanya kazi chini ya Sheria ya Ushindani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2006. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Bi. Khadija Ngasongwa akila kiapo cha uaminifu kuwa Kamishna wa EACCA, pembeni ni Mwanasheria wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Denis Kibirige wakati wa mkutano wa Mamlaka za Ushindani za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Mjini Moshi Aprili 23, 2026.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Bi. Khadija Ngasongwa akiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Annette Mutaawe Ssemuwemba (kulia) na Mwenyekiti wa Muda, Bw. David Kemei (kushoto) wakati wa hafla ya kuapishwa kuwa Kamishna wa EACCA kwenye mkutano wa Mamlaka za Ushindani za Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyofanyika Mjini Moshi Aprili 23, 2026.

Safu ya Makamishna wa Mamlaka ya Ushindani ya Afrika Mashariki (EACCA), wakiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Annette Mutaawe Ssemuwemba mara baada ya kuapishwa rasmi kwenye mkutano wa Mamlaka za Ushindani za Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyofanyika Mjini Moshi Aprili 23, 2026.

Matukio mbali mbali kwenye picha wakati wa hafla ya uapisho wa Makamishna wapya wa Mamlaka ya Ushindani ya Afrika Mashariki (EACCA)
Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

OSCAR ASSENGA

Post A Comment: