Na Denis Chambi, Tanga.

JUMLA ya makocha 25 wapo mkoani Tanga wakipatiwa mafunzo ya ukocha ngazi ya  Diploma B ya CAF inayoendeshwa na shirikisho la soka Tanzania ‘TFF’ hii ikiwa ni jitihada moja wapo zinazofanyika kukuza na kuboresha soka hapa nchini pamoja na kuwajengea uwezo utakaowasaidia  kuingia katika soka la ushindani.

Kozi  hiyo  ya siku 10  ambayo imeanza February 28 hadi Marh 9,2023 imejumuisha pia raia wawili  wa kigeni  kutoka   Rwanda na Kenya ambapo mara baada ya washiriki  kuhitimu watapata nafasi ya kwenda kushiriki kozi ya leseni  A  ya shirikiho la soka Barani Africa ‘CAF’ sambamba na kupewa fursa ya kwenda kuwa wasaidizi kwenye mabenchi ya timu mbalimbali hapa nchini.

Kozi hiyo ambayo inafanyika katika kituo cha michezo kinachojengwa na TFF kilichopo Mnyanjani jijini Tanga imehudhuriwa  pia na baadhi ya wachezaji wa zamani waliowahi kuzichezea timu mbalimbali  hapa nchini akiwemo Mussa Hassan Mgosi, Nizar Khalfan, Abdi Kassim , Aggrey Morris, pamoja na Kali Ongala.

Akifungua mafunzo hayo Rais wa shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ Walles Karia alisema kuwa  mpango uliopo  kwa sasa ni kuhakikisha kuwa wanawatumia wachezaji wa zamani waliowahi kucheza kwa nyakati tofauto tofauti hapa nchini kuwapa fursa ya  kupata kozi hizo ili kuziongoza timu zinazoshiriki ligi mbalimbali za ndani ikiaminikma kuwa wao watakuwa ni chachu na mchango mkubwa wa kuzidi kukuza vipaji kwa wachezaji na kuzisaidia timu za taifa katika michuano ya kimataifa.

“Ni faraja kubwa sana kwa sababu kozi hii imejumuisha wachezaji wengi wa zamani kwa maana wametambua kuwa wao baada ya uchezaji wao  wameendelea kufundisha lakini pia wanataka wafundishe wakiwa wenye sifa na vigezo  vinavyostahili ninawapongeza kwa hilo”

 “Lakini pia ni  utaratibu wetu sisi TFF  kuhakikisha kwamba tunawatumia  wachezaji wa zamani kwa sababu wametumikia mpira muda mrefu  na wamepitia katika mifumo ambayo ipo nchini kwetu  na  wanatambua hali halisi na mazingira  kuhakikisha kwamba  mchezaji asije akasikitika kwamba muda wake umeisha bado anang’ang’ania  kucheza mpaka ligi ya wilaya ajitambue kwamba anaweza akatumika katika sehemu nyingine yeyote ile ikiwemo kusaidia katika timu zetu za Taifa” alisema Rais Karia.

Alisema mpaka sasa  bado ipo changamoto ya makocha wa Tanzania kushindwa kufundisha soka nje ya mipaka ya Tanzania hii ikichangiwa pia na kukosa vigezo stahiki hata hivyo ni matamanio makubwa ya TFF kuona wanaendelea kuzitatua  ikiwa ni pamoja na kuendesha kozi mbalimbali zitakazoweawezesha makocha kuingia katika soka la kiushiundani ndani na nje.

“Suala la makocha wetu  kwenda kufundisha nje ya nchi bado ni changamoto ambayo ipo lakini huko nyuma walishawahi kwenda sasa  hivi tunataka hii hali ambayo makocha wanakuja Tanzania  na wa kwetu hawatoki  ije ibadilike  lakini haiwezi kubadilika kama wao wenyewe hawatakuwa na vigezo  vinavyostahili”  aliongeza Rais Karia.




Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania 'TFF' akiwa pamoja na mkurugenzi wa ufundi wa shirikisho hilo leo mkoani Tanga wakati wa mafunzo ya uleseni ya CAF Diploma B iliyotolewa kwa makocha 25 wa Tanzania wakwemo wawili wa Rwanda na Kenya.

Share To:

Post A Comment: