Mbunge wa jimbo la Tanga na waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameitaka halmashauri ya jiji la Tanga kuangalia uwezekano wa kuongeza posho za wenyeviti wa mitaa wanazolipwa kila baada ya miezi mitatu ili kuongeza motisha ya ufanyaji kazi katika maeneo yao wanayosimamia. 

Waziri Ummy ametoa rai hiyo wakati wa kikao kazi na wenyeviti wa mitaa 181ya jiji hilo kujadili maendeleo ya halmashauri hiyo ikiwemo usimamizi wa miradi ya maendeleo ambapo pia amesema kuwa utaratibu huo ufanyike kwa kuzingatia maelekezo kuyoka ofis ya Rais Tawala za mikoa na serikali za Mitaa TAMISEMI. 

 "Tunakubaliana kwamba posho za wenyeviti zisipitishe tarehe 15 wawe wamwshapata na kiwango cha posho za mwezi kiongezwe lakini miongozo haijaweka kiwango maalum hii inategemea na uwezo wa makusanyo ya ndani ya halmashauri husika nimuombe sana mstahiki meya pamoja na mkurugenzi hili mliangalie vizuri na katika hili mimi binafsi nitashirikiana na waziri wa TAMISEMI ikiwezekana utoke muongozo mpya ambao utaelekeza namna ya malipo hayo" alisema Ummy. 


 Aidha Waziri Ummy amewataka wenyeviti pamoja na viongozi wote wa serikali za mitaa kuzingatia sheria kanuni na taratibu za uongozi huku akiwasisitiza kutenda haki kwa wananchi wanaowaongiz nyakati zote na sio kutumia madaraka yao vibaya. 

 "Nawasisitiza mkatende haki kwa wananchi kwa sababu pia tunapokea malalamiko baadhi yetu tunapindisha haki yanapokuja maswala ya wananchi niwaombe sana ndugu zangu tusiangalie leo tu lakini tuangalie na kesho, tutatue kero za wananchi mwenyekiti na serikali yako ya mtaa kuna mambo ya kutatua sio lazima aje mkuu wa wilaya au waziri" alisisitiza

 Pamoja na hayo Ummy amewataka wenyeviti wote kupitia vikao vyao ya kila mwezi kuendelea kupiga vita vitendo vya ukatili vinavyoendelea kufanyika katika maeneo yao hasa dhidi ya watoto ambavyo vimeendelea kukithiri kila kukicha pamoja na kuhimiza maswala ya lishe bora kwa mustakabali mzima wa vizazi vijavyo. 

 Hayo yanakuja baada ya taarifa ya viongiozi hao iliyotolewa na katibu wa umoja wa wenyeviti wa mitaa wa halmashauri ya jiji la Tanga Juma Mwahengwa kuomba kuongezewa posho zao za kila mwezi sambamba na kulipwa kwa wakati stahiki zote hii ikiwa ni njia ya kuongeza ari ya ufanyaji kazi katika kutimiza majukumu yao ya kila siku huku wakiahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii kwa maslahi mapana ya wananchi na serikali kwa ujumla. 

 "Wenyeviti wanaomba kiwango cha posho zile zinazolipwa kila baada ya miezi mitatu kiongezwe ikiwemo posho za vikao vya ODC lakini pia zilipwe kwa wakati mfano posho za baada ya kushiriki katika kampeni za kitaifa ikiwemo za magonjwa kama vile Polio, Matende na Ngirimaji hata hivyo tutaendelea kushiriki ipasavyo katika kampeni ambazo hazijatengewa fedha kwa maslahi mapana ya wananchi wa jiji la Tanga" alisema katibu huyo 

 Awali akizungumza mkuu wa wilaya ya Tanga Hashimu Mgandilwa amesema kuwa kamati ya ulinzi na usalama imekuwa ikiimatika kila kukicha viongozi wa serikali za mitaa kwa kushirikiana na jeshi la Polisi wakifanya kazi kubwa ya kupambana na uhalifu huku akiwataka kuendelea kuonyesha ushirikiano huo 

 "Kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama niwashukuru sana wenyeviti wote kwa kazi kubwa ambayo tunaendelea kuifanya huko kwenye maeneo yenu, wakati ninafika Tanga moja ya kitu ambacho kilikuwa kinatusumbua kwenye kamati za usalama ilikuwa ni watoto wa ibilisi sasa hivi kwa kiwango kikubwa sana hizo kelele hatuzisikii tena hii sio jitihada za jeshi la Polisi peke yake wala vyombo vya dola lakini ni pamoja na mchango mkubwa ambao ninyi mmeutoa binafsi yangu niwashukuru sana mmetimiza moja ya wajibu na haki ya msingi ya kila raia wa Tanzania" alisema Mgandilwa. 

 Kwa upande wake mtahiki meya wa Halmashauri ya jiji la Tanga Abdurahman Shillow amewataka wenyeviti wa mitaa kuandaa na kufanya mikutano ya mitaa kulingana na utaratibu uliowekwa huku akiwataka kutokujishughulishaa na uuzaji wa ardhi ambao umekuwa ukisababisha migogoro mbalimbali katika jamii. 

 "Niwakumbushe wenyeviti wetu wa mitaa wengi wao hawafanyi mikutano yao ya mitaa kila baada ya siku 60 kila mwenyekiti anatakiwa awe amefanya mikutano na wananchi wake na diwani naye awepo kwahiyo niwaombe muandae na kufanya mikutano hiyo na muktasari ya mikutano hiyo iende kwa mkurugeni wa jiji la Tanga , wenyeviti tambueni kwamba hamna mamlaka wala sheria ya kushuhudia maswala ya mauziano ya ardhi kazi hiyo inafanywa na mawakili wasomi wenye vitengo vyao pamoja na idara ya ardhi ambayo inafanya kwa niaba ya Mkurugenzi kwahiyo mwenyekiti huruhusiwi kuuza ardhi pamoja na kusimamia vyema matumizi ya fesha za miradi ya maendelo inayotekelezwa kwenye maeneo yao" alisema

 Sambamba na hilo Shillow akijibia hoja ya wenyeviti hao ya kuomba kuongezewa posho zao za kila mwezi amesema halmashauri ipo kwenye mchakato wa kuongeza kiwango cha posho hizo ambapo ifikapo july 2022 wataanza hii ikiwa ni kulingana na miongozo ya serikali kupitia ofis ya Rais tawala za mikaa na serikali za mitaa TAMISEMI. <
Share To:

Post A Comment: