Akizungumza na wananchi, Mbunge Mariam amesema mchango huo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na wananchi pamoja na wadau mbalimbali katika kuhakikisha shule hiyo inakamilika.
Akizungumza na wananchi, Mbunge Mariam amesema mchango huo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na wananchi pamoja na wadau mbalimbali katika kuhakikisha shule hiyo inakamilika.
Mbunge wa Jimbo la Hanang Mkoani Manyara ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Mhe. Asia Halamga, amekabidhi mifuko ya mbegu za dengu kwa viongozi na wananchi mbalimbali wilayani Hanang ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha sekta ya kilimo na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Akizungumza katika hafla ya ugawaji wa mbegu hizo Mbunge huyo amesema kuwa lengo la kutoa mbegu hizo ni kuongeza tija kwa wakulima na kuinua kipato chao kupitia kilimo cha kisasa hususani baada ya mvua nyingi za mwaka huu kuharibu mazao ya maharage shambani
Asia ameendelea kueleza kuwa kuwa utoaji wa mbegu hizo utasaidia kurejesha uzalishaji na kuimarisha usalama wa chakula kwa wakazi wa Hanang kwani mbegu za dengu ni mkakati wa kuongeza uzalishaji wa mazao ya biashara yenye soko la uhakika ndani na nje ya nchi.
Kwa upande Mkuu wa Wilaya ya Hanang Almishi Issa Hazali amemshukuru Mbunge Asia Halamga kwa kuwakumbuka wananchi wa Jimbo hilo na kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi
“Hatua hii ni ya kupongezwa kwani inaenda moja kwa moja kugusa maisha ya wananchi wetu na sisi kama Serikali tutaendelea kushirikiana na Mbunge sambamba na viongozi wengine wote wenye nia njema ya kuleta maendeleo katika Jimbo letu hili,” Amesema Almishi
Hata hivyo wananchi hao wamemshukuru sana Mbunge huyo kwa msaada huo ambao utaleta mapinduzi makubwa katika sekta ya kilimo.
Umoja wa Wanawake Machinga Dodoma(UWAMADO) wamempongeza Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa ujenzi wa soko la kisasa la Machinga Complex na miundombinu ya kisasa ya soko hilo ambalo ni la kipekee nchini.
Hayo yamesemwa jana wakati wa uzinduzi wa chama cha UWAMADO uliofanyika kwenye eneo la soko la Machinga Complex kwa kuzinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule
Akisoma Risala Katibu wa UWAMADO Bi. Mariam Kajembe amesema umoja huo umelenga kuwaleta wanawake Machinga pamoja ili kujijenga na kujiimarisha uchumi.
Aidha pia UWAMADO umempongeza Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa ujenzi wa Soko la Machinga Complex ambalo limesaidia kuwaleta pamoja wafanyabiashara wengi wadogo pamoja ambao awali hawakuwa katika maeneo rasmi na hivyo kuwafanya kutokuwa rasmi.
Akitoa hotuba yake,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule amewapongeza UWAMADO kwa kuamua kuanzisha umoja wao ambao utawasaidia kujiendeleza zaidi na kujiimarisha kiuchumi.
“Jambo hili la kuanzisha umoja ni jambo jema,hakikisheni umoja unafikia malengo mliyokusudia.
Mh. Rais kawajengea soko kubwa na zuri,soko hili liwe kichocheo cha ukuaji wenu kimtaji na kibiashara.
Niwatake Uongozi wa Jiji la Dodoma kuendelea kubuni na kuanzisha maeneo mapya ya kuwapanga vizuri wafanyabiashara wadogo wa Dodoma”Alisema Senyamule
Akitoa salamu zake Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde amewapongeza UWAMADO kwa kuona umuhimu wa kukaa pamoja kujiinua kiuchumi na kuwataka kuchangamkia fursa ya mikopo ya asilimia 10% ya mapato ya ndani ya Jiji ambayo kiasi cha Shilingi Bilioni 7 kimetengwa kwa ajili ya kuwawezesha wakina mama,vijana na watu wenye ulemavu.

















Akisisitiza umuhimu wa kuwa na Shukrani kama ambavyo imehubiriwa hii leo kwenye Ibada ya Pasaka kwenye Kanisa la KKKT Sinoni Jijini Arusha, Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Mrisho Gambo amemtaja Rais Samia kama Kiongozi aliyeweka alama nyingi za vielelezo vya miradi ya maendeleo Arusha Mjini, akimshukuru kwa kutenga fedha nyingi za kutekeleza miradi ya Maendeleo Arusha.
Mhe. Gambo aliyeshiriki Ibada ya Pasaka kwenye Kanisa hilo na kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo zinazoendelea kanisani hapo, ameeleza kwamba kuwa na Mwanamke Kiongozi kuanzia ngazi ya familia ni baraka na chanzo cha Maendeleo, akisema kwa Arusha pekee Rais Samia amefanikiwa kukuza uchumi wa wananchi kwa asilimia kubwa kwa kipindi kifupi ambacho amekuwa Rais wa Tanzania.
Mhe. Mrisho Gambo amewaambia waumini wa kanisa hilo kuwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa muda mfupi aliokuwa madarakani, ametoa Bilioni 286 kwaajili ya ujenzi wa Uwanja wa michezo Mirongoine kata ya Olmot, lakini pia amesisimua sekta ya utalii Mkoani humo kupitia filamu ya The Royal Tour, suala ambalo limekuza uchumi na kutoa ajira kwa Vijana na wajasiriamali wengi wa Mkoa wa Arusha, akieleza kuwa mambo hayo kwa Arusha yanafanikiwa kutokana na ushirikiano uliopo kati ya Ofisi yake na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Madiwani wa Arusha Mjini.
Gambo pia amezungumzia mradi wa Uendelezaji Miji Tanzania (TACTICS)ambapo ameeleza kuwa kutokana na jitihada za Rais Samia, fedha zimetolewa na Tenda imeshatangazwa ambapo kutafanyika Ujenzi wa Masoko makubwa mawili ya Kilombero na Morombo, yatakayokwenda sambamba na ujenzi wa Kituo kikuu cha Mabasi Arusha itakayojengwa eneo la Bondeni City.
Akizungumzia alama zilizowekwa na Rais Samia kwa Kata ya Sinoni, Mhe. Gambo ameeleza kuwa Rais Samia atatoa Milioni 250 za awali kwaajili ya ujenzi wa Kituo cha afya Sinoni, akitoa pia fedha katika Bajeti ijayo ya serikali kwa ajili ya Ujenzi wa shule ya Sekondari Sinoni ili kupunguza masafa marefu ya wanafunzi kufuata huduma ya elimu kwenye shule za nje ya Sinoni.
Mhe. Gambo amemshukuru Rais Samia pia kwa kuirejesha Arusha kwenye uenyeji wa mikutano ya Kitaifa na Kimataifa, akieleza kuwa mikutano hiyo imekuwa sehemu ya kukuza uchumi wa wananchi wa Arusha Mjini kupitia biashara na Ujasiriamali ambao wamekuwa wakiufanya na kuleta tija kutokana na mwingiliano na ugeni mkubwa wa watu mbalimbali wanaofika Arusha kuhudhuria Mikutano na warsha za ndani na nje ya Tanzania.