Na John Walter-Babati

Viongozi wa wilaya na mkoa wa Manyara wameaswa kufanya kazi kwa bidii ikiwemo kwenye miradi ya maendeleo ili kuepusha ucheleweshwaji wa kumalizika kwa miradi hali inayotoa mianya ya ongezeko la bei za miradi na kuharibika kwa vifaa vya kukamilisha miradi hiyo

Hayo yamesemwa na Khamisi Mohamed Babu aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali hapa nchini ikiwemo nafasi ya utendaji wa Kata, ambapo na amesisitiza kuwa miradi mingi kwa sasa inacheleweshwa hivyo ili kuendana na kasi ya maendeleo ni muhimu viongozi watekeleze kwa wakati miradi hiyo.

Akizungumza katika mjadala wa kumbukizi ya miaka 61 ya uhuru wa Tanzania Bara uliofanyika ndani ya ukumbi wa halmashauri ya mji wa Babati pia amepongeza hatua za serikali katika kusonga mbele kimaendeleo na kisiasa licha ya changamoto zilizopo ambazo pia zinapaswa kutiliwa maanani ili kupiga hatua zaidi

Kumbukizi ya miaka 61 ya uhuru wa Tanzania Bara inaadhimishwa leo huku ujinga Maradhi na umasikini bado imeonekana ni kikwazo kwa Watanzania, hivyo serikali inapaswa kufanya juhudi zaidi kutokomeza maadui hawa wakuu wa Maendeleo.


Share To:

Post A Comment: