Na John Walter-Babati

Mjumbe wa bodi ya shirika la maendeleo ya viwanda vidogo Mkoa wa Manyara (SIDO) ndugu Jitu vrajlal son amesema kuwa sasa wakazi wa mkoa huu wanapaswa kutumia vizuri fursa za vivutio vya utalii vilivyopo ili kujiongezea kipato na kuondokana na changamoto ya ukosefu wa ajira.

Jitu ameyasema hayo kwenye mjadala wa kumbukizi ya miaka 61 ya uhuru wa Tanzania bara uliofanyika ndani ya ukumbi wa halmashauri ya mji wa Babati huku akiongeza fursa za utalii ni nyingi katika mkoa wa Manyara ikiwemo uwepo wa ziwa Babati hifadhi ya Tarangire, Maji ya moto, Kisima cha Mungu hivyo vikitumika vizuri ni manufaa kwa wana Manyara wote.

Pia ameongeza kuwa kwa upande wa serikali hususani idara ya mazingira wanapaswa kutunza vizuri vyanzo vya maji kwani ndio msingi mzuri wa kudumisha mazingira bora yanayopelekea watalii mbalimbali kuvutiwa na kuja kutembelea vivutio vilivyopo hali itakayochochea ongezeko la mapato kwa serikali

Tanzania bara leo inaadhimisha  miaka 61 ya uhuru huku wadau mbalimbali wakiendelea kutoa maoni juu ya maboresho ya sekta mbalimbali za maendeleo kama kilimo kinachotegemewa na asilimia kubwa ya watanzania kama sehemu ya kuwa patia kipato.

Share To:

Post A Comment: