Christina Thomas Morogoro.


Wizara ya mambo ya ndani ya Nchi imelitaka jeshi la zimamoto na uokoaji kuendelea kujifunza mbinu mpya za kisasa  na kiteknolojia kutoka mataifa rafiki ilikuendelea kutekeleza majukumu yao kiufanisi zaid licha ya jeshi hilo kukabiliwa na changamboto mbalimbal ikiwmo ya watumishi ambapo kwa mwaka jhuu wameweza kuajiri wtumishi 400 ambao bado hawakizi kwa vituo vyote hapa nchini.


Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi bi, Gaudensi Mmmasi akimwakilisha  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  katika ufunguzi wa kikao kazi cha balaza dogo la wafanyakazi wa  jeshi  lazimamoto na uokoani  kilichofanyika mkoani morogoro na kukutanisha wajumbe wa balaza na viongozi kutoka mikoa yote ya tanzania.


Mkurugenzi Mmasi amesema kuwa wizara inatambua changamoto ilioko ya uhaba wa watumishi katika jeshi hilo kwani watumishi 400 hawatoshi katika vituo vyote vya wilaya na mikoa yote ya tanzania lakini walau si haba na mambo ya taendelea kuwa mazuri tukizingatia mamlaka za juu za serikali Rais wa Jamuhuri ya Mmungano wa Tanzani Samia Suluhu Hassan  hivi karibuni alianza kutoa fursa za kuajiri.


Mkurugenzi Mmasi amesema kuwa tukikumbuka karibu miaka mitano  iliyopita serikali ilikuwa haiajiri watumishi lakini walau kwanzia mwaka jana serikali imeanza kufungua mlango na tunaamini kidogo kidogo  serikali itaona umuhimu wa kuongeza nafasi za watumishi katika jeshi letu pia ameeleza kuwa serikali inaendelea kuboresha maslahi ya wafanya kazi  ambapo walau mwaka jana Rais wa Jamuhuri ya Mmungano wa Tanzani Samia Suluhu Hassan aliwaongezea mshahara kidogo kwa watumishi na maswala ya posho yfanyiwa kazi ambapo  mazingira ya kazi ya naendelea kuboreshwa.


Aidha amelipongez serikali na uongozi wa jeshi kwa ufwatiliaji makini  kwani bado jeshi lina endelea kufwatilia hivyo tuendelee kuwaunga mkono na kuwatia moyo kwa kuendelea kutimiza majukumu yetu vizuri ili na wao waweze  kuendelzaea juhudi zao kufatilia upatikanaji wa  maslahi yetu  bora zaidi.


Pia amesema kuwa serikali inendelea chukua hatua katika kuboresha mazingira bora ya kazi kwa watumishi  katika usimamizi mahiri wa viongozi wetu wa jeshi la uokoaji lakini katika changamoto zote hizo bado tata uendelee kuhimizana kutekeleza majukumu yaliyo mbele yetu kwa ujasiri na ubunifu mkubwa ilikuona namna  bora ya kutekeleza majukumu hayo kwa ufanisi na tija kubwa lakini pia kwa faida la taifa letu kwa sababu kazi mnayo ifanya mnasaidia umma  kwani kuokoa maisha ya mtu , mali na vifaa sio vya serikali ni  kwaajili ya  wananchi tunao wategemea.


Naye Kamishna wa  utawala na fedha jeshi la zimamoto na uokoaji  Mbaraka Semwanza amesema kuwa jeshi la zimamoto na uokoaji linaendelea kutekeleza miladi ya maendeleo  katika mikoa 9 mbayo ni Ilala,Aarusha , Morgoroo, Dodoma, Songwe, Tanga , Simiyu Ruvuma na Mwanza  na kupewa na serikali shilingi  zaidi  bilioni 9   ambapo jeshi limefikia hatua za mwisho ya kuanza  kutekeleza miladi mbalimbali kama ya ujenzi na ukalabati wa vituo.


Pia ameishukuru serikali kwa kuajiri watumishi 400 kutoka chuo cha mafunzo chogo handeni   mkoa wa tanga  ambapo vijana hao wamepunguaz kiasi flani changamoto ya watumishi katika jeshi na kuiomba serikali kuboresha maslahi ya maafisa na askari wa jeshi la zima moto kwani wamendelea kufwatilia na kuratibu malipo ya posho za kikanuni ambapo jumla ya posho nane zinztarajiwa kulipwa wakati wowote pindi pesa zitakapo patikana na utekelezwaji wa posho hizoutakapo anza makamanda watapata maelekezoya hatua za kuchukua ili maafisa na askari wenye sifa waweze kupewa posho hizo .

Share To:

Post A Comment: