NA DENIS CHAMBI, TANGA.
MWENYEKITI wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Tanga, Tanga Pres Club(TPC) Bi Lulu George amewaasa wanahabari kujikita katika uandishi wa habari za kiuchunguzi na za kijamii hasa zile zinazohusu kundi la watoto hii ikiwa ni pamoja na kuibua matukio ya ki ukatili yanayotokea katika jamii ili kuunga mkono kampeni ya serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo hapa nchini ya kupinga na kutokomeza ukatili dhidi yao.
Ametoa wito huo November 5,2022 wakati wa semina
iliyoandaliwa na taasisi ya Tanga Youth Talent Association (TAYOTA) kwa
waandishi wa habari yenye lengo la kuwajengea uwezo na ulewa wa kuripoti taarifa
zinazohusu ukatili dhidi ya watoto na vijana wa kundi balehe zinazotokea katika
jamii ambapo amesema kuwa bado yapo
matukio mengi ya ukatili yanatokea na hayatolewi taarifa hivyo ni vyema wanahabari
wakajua kuwa wanahusika moja kwa moja
katika kupiga na kutokomeza ukatili ambao unazidi kushamiri kwenye maeneo
mbalimbali.
“Suala la uandishi wa habari za kiuchunguzi hatuwezi
kulikwepa hili jukumu ni letu na ndio litaleta hasa maana halisi ya kile tunachokiandika ambapo kitakuwa na tija kwa jamii niwaombe sana tuone kuwa sisi ni sehemu na
daraja katika suala la kupinga na
kutokomeza ukatili kwa maslahi mapana ya Umma” alisema Lulu,
Amesema kuwa mwandishi wa habari hapaswi kufungamana na
upande wowote pale anapohitaji kutolea taarifa zinazohusu ukatili wa mtoto
kwenye jamii badala yake asimamie maadili taratibu na kanuni zinazomuongoza katika
taaluma yake huku akiwataka kupenda kujifunza na kusoma kwa kina sheria zinazomlinda
mtoto ili ziweze kuwarahishia wakati wanapohitaji kuchunguza matukio ya ukatili
yanayotokea kwenye maeneo mbalimbali.
“Na kama tunataka kuandika maswala ya watoto kwa kina ni lazima tuepushe uharaka tusome sheria na
majarida mbalimbali inahitaji utulivu na
niwatoe hofu kwamba uandishi wa habari za kiuchunguzi sio kuandika kila kinachosemwa peke yake bali tupende
kujifunza kwa kina sheria zinazomlinda mtoto na sasa hivi teknolojia imekuwa ni
rahisi na nyepesi sana kwetu ni suala la sisi kujua na kupenda kile kinachozungumzwa
tunakifwatilia kwa namna gani”aliongeza
Akizungumza katika semina hiyo Afisa vijana kutoka halmashauri ya jiji la Tanga Fadhili Secha amesema kuwa lipo wimbi kubwa la vijana na watoto wanaojishughulisha na biashara za uuzaji wa kahawa, karanga na mayai ambao kwa umri wao wanapaswa kuwepo shuleni hivyo ni vyema waandishi wakafanya uchunguzi kujua sababu zinazopelekea kuongezekwa kwa kundi hilo ambao licha ya kujihusisha katika biashara hizo zipo adha mbalimbali wanazokutana nazo.
“Vipo visa vya watoto wanaofanya baiahara za uuzaji wa
karanga mayai na kahawa lakini wengine wanatoka katika mazingira magumu, ukweli
ni kwamba wanakutana na changamoto nyingi sana hili ni kundi ambalo lintakiwa
liangaliwe hivyo waandisi wa habari
tunatakiwa tusiwe waoga au tusiache kuripoti taarifa kama hizo” alisema Secha
Aliongeza kuwa zipo jitihada mbalimbali zinazofanywa na halmashauri
ya jiji la Tanga katika kuhakikisha kundi
la vijana wasio na ajira mtaani linapungua au kuondoka kabisa ambapo
wanaendelea kutoa mikopo ya asilimia 10 isiyo na riba kwa kundi hilo hivyo kuwaomba
waandishi wa habari kutumia weledi wao kuelimisha jamii hasa vijana kujiunga
katika vikundi mbalimbali vitakavyowawezesha kupata mikopo hiyo ili iweze
kuwaletea maendeleo na hatimaye kuepuka kujihusisha na makundi hatarishi .
“Hili kundi la vijana linataabika sana na mambo mengi , wengi
wanahangaika kwaajili ya kupata namna ya kujitegemea katika maisha na wengine
ni suala la kukosa mitaji lakini
serikali kwa namana walivyotengeneza kuna fursa za utoaji wa mikopo ile mikopo ipo tena ni mikopo ambayo ina masharti
nafuu niwakumbushe waandishi wa habari sehemu
ambayo tutakuwa tunapita tuwakumbushe vijana waje kwenye halmashauri zao kuja kuchukuwa mikopo hiyo wakiwa kwenye
vikundi vyao”.
“Lakini pia Tarehe 14 October mwaka huu tulipokea muongozo
mpya kutoka wizara ajira vijana na watu wenye ulemavu iliyompa fursa kijana
mmoja mmoja kuweza kukopeshwa na hii ni mikopo kutoka wizarani hivyo kijana
anaweza akaja akajaza fomu tukazituma Dodoma na hatimaye akapata fedha zake”
alisema
Kwa upande wao baadhi ya wadau walioshiriki semina hiyo wameipongeza
taasisi ya Tanga Youth Association (TAYOTA) kuwa kulitambua kundi la wanahabari
katika jitihada zao za kupambana na vitendo vya ukatili huku wakiwaomba
kupelekaa semina hiyo kwa makundi mengine wakiwemo wazazi ili kuzidi kupanua
wigo na kuongeza elimu kwa jamii katika kupiga vita ukatili hususani kwa watoto na vijana waliop0 kwenye kundi
balehe.
Post A Comment: