Serikali kupitia Wizara ya ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa imetoa fidia ya fedha kiasi cha shilingi milioni 243.7 kwa ajili ya wananchi 160 wa Vijiji vya Choda na Mkiwa Wilaya ya Ikungi 

Akizungumza wakati wa kikao cha utoaji wa taarifa za mapokezi ya fedha hizo, Mkuu wa wilaya ya Ikungi Jerry C. Muro amesema Mheshimiwa Rais. Samia Suluhu Hassan ameridhia fedha hizo kutolewa kwa wananchi 112 wa kijiji cha mkiwa na wananchi 48 wa kijiji cha Choda mara baada ya kufanyiwa uthamini na kukamilisha taratibu zote za kisheria za ulipwaji wa fidia 

Kwa upande wao baadhi ya wananchi ndugu Mayunga Mayunga luhende na Pascal Michael Ghula pamoja na kumshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza kwa vitendo ahadi ya kuwalipa fidia ili wapishe shughuli za kambi ya jeshi katika kata ya mkiwa wamepongeza mchakato wote wa utathimini kuwa wa wazi na wa ukweli

Katika hatua nyingine Dc Muro pia aliwaomba viongozi wa jeshi wanaosimamia kambi ya mkiwa kutumia busara kwa kuwaruhusu wananchi wamalize kutoa mazao yao ambayo waliyapanda katika mashamba yanayozunguka kambi hiyo kutokana na wao kuandaa na kupanda kabla ya kulipwa fidia ombi lililokubaliwa na msimamizi wa kambi hiyo.


Share To:

Post A Comment: