KAMATI ya kudumu ya Miundombinu ya Bunge imefanya ziara katika Ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kupata maelezo ya usimamizi wa mnada wa msafa utakaoiwezesha Serikali kupata Dola za Kimarekani milioni 187.4.

Aidha wajumbe wa kamati hiyo  wameelezwa namna vitalu vya masafa vitakavyowezesha utoaji wa huduma za ziada za mawasiliano ikiwemo intaneti ya kasi ya Kizazi cha Tano yaani “5G.”

Mbali na hayo, Kamati hiyo imepokea maelezo kwamba Tanzania ni nchi ya kwamza barani Afrika kuuza Masafa yenye thamani kubwa kwa mfumo huu, kwa kutumia wataalam wa ndani kwa mafanikio makubwa.

Kamati hiyo pia ilielezwa mafanikio katika usimamizi wa sekta ya Mawasiliano nchini, uliotolewa na wataalam wa Mawasiliano wa TCRA na Wizara inayosimamia sekta ya Mawasiliano nchini.

Ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Selemani Kakoso, kamati imepokea wasilisho kuhusu mnada wa masafa uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam ulioshuhudia watoa huduma za Mawasiliano ya simu watano wakipata masafa kwa ajili ya kuwezesha huduma za mawasiliano katika teknolojia za kizazi cha nne yaani 4G na 5G.

“Naamini kwamba sekta ya Mawasiliano ni sekta muhimu kwa kuwa inatengeneza uchumi wa nchi yetu,” alisisitiza Kakoso.

Akiwasilisha mbele ya kamati hiyo, Dk  Jabiri  Bakari, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA aliwaeleza wajumbe wa kamati kwamba jumla ya vitalu 11 vya masafa viliuzwa kupitia Mnada huo wa masafa uliofanyika kwa njia ya uwazi na kuwezesha watoa huduma kupata rasilimali hiyo adimu inayowezesha Mawasiliano.


“Masafa ni moja ya rasilimali za nchi kama ambavyo tuna rasilimali zingine kama vile rasilimali madini au rasilimali ardhi; masafa kama rasilimali inawezesha kubeba taarifa kutoka upande mmoja kwenda mwingine, inaweza kuwa katika mfumo wa picha, sauti au data,” alifafanua.

“Utaratibu wa kugawa masafa kwa njia ya Mnada ni utaratibu ambao unatumika kimataifa na tumefanikiwa kuendesha zoezi la ugawaji wa vitalu kwa mafanikio. Kabla ya utaratibu huu masafa yalikuwa yanagawiwa kwa utaratibu wa ‘first come first served’ yaani atakaewahi ndie huyo anahudumiwa, ilikuwa mtu mmoja anaweza kuchukua masafa zaidi kiasi kwamba mtu mwingine akija akiambiwa masafa yamekwisha yanakuwa yamekwisha,” aliongeza.

Alifafanua kuwa utaratibu wa masafa kwa njia ya Mnada umeongeza uwazi juu ya zoezi la ugawaji masafa na kuongeza Imani kwa watoa huduma wanaohitaji rasilimali hiyo, kwa kuzingatiwa kuwa wanashirikishwa kila hatua.

Mbele ya kamati hiyo, TCRA ilitoa  maelezo juu ya utendaji kazi wa Mamlaka, utoaji na usimamizi wa Leseni za Mawasiliano, ambapo wajumbe wa Kamati walipata wasaa wa kuuliza maswali mbalimbali yaliyotolewa ufafanuzi na wataalam wa Mamlaka.

Akizungumza wakati wa majumuisho baada ya kupokea maelezo ya wataalam wa TCRA, Menejimenti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Kakoso ameipongeza Mamlaka hiyo katika kuleta mapinduzi kwenye sekta.

Mwenyekiti Kakoso katika majumuisho baada ya kupokea maelezo  na Menejimenti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habar alipongeza

Share To:

Post A Comment: