Wasafirishaji wote wa vifurushi na vipeto wanaofanya kazi katika kanda ya nyanda za juu kusini yametakiwa kutumia muda huu wa upendeleo kurasimisha huduma zao za usafirishaji kwa kuchukua leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
Akizungumza katika mkutano wa wadau wa huduma za Kiposta Mkoa wa Mbeya Meneja wa TCRA kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mhandisi Asajile John amesema umiliki wa leseni ya TCRA unaongeza mapato kwa watoa huduma kwani wateja wengi wanavutiwa zaidi kutuma mzigo kwa watoa huduma rasmi na kuondoa usumbufu namna ya upatikanaji wakati anahitaji kutuma kifurushi/Kipeto.
Amesema kuongezeka kwa wateja kunapelekea kuongezeka kwa mapato ya watoa huduma ambayo yanachangia ongezeko la pato la taifa.
Mhandisi Asajile amesema ili kufanikisha hilo TCRA imeanzisha mfumo wa utoaji leseni mtandaoni ujulikanao kama mfumo wa Tanzanite ambapo mtoa huduma anaweza kuomba hadi kupata leseni kwa njia ya mtandao jambo ambalo linarahisisha utendaji na kuokoa gharama.
Ameongeza kuwa iwapo waombaji hao wa leseni watakumbana na changamoto katika kuombq leseni wanaweza wasiliana na TCRA kupitia namba ya dawati la huduma ambayo ni 0800008272 au kufika katika ofisi yoyote ya Mamlaka kwa msaada zaidi.
Mkutano huu ni sehemu ya kampeni ya kuhamasisha wananchi kutumia huduma za watoa huduma wa kusafirisha vifurushi waliosajiliwa ijulikanayo kama TUMA CHAP kwa usalama ambapo inahusisha kuhamasisha watoa huduma wajisajili na jamii kuwatumia watoa huduma rasmi.
Na; Elizabeth Paulo,Dodomaa
Naibu Waziri wizara ya habari mawasliano na Taknologia ya habari Mhandisi Kundo Methew amesema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wote wa sekta ya habari na utangazaji katika maendeleo ya Taifa.
Mhandisi Methew amesema hayo leo Februari 13 jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa mwaka wa watoa huduma wa sekta ya utangazaji Tanzania uliyoenda sambamba na siku ya radio Duniani.
Amesema Serikali ipo tayari kushirikiana na wadau wa habari na utangazaji, huduma ya utangazaji imekuwa na mabadiliko makubwa huku vyanzo vya mapato vya kuendesha vituo vikiwa vilevile,na huduma ya utangazaji Kwa kiasi kikubwa inategemea matangazo ya biashara na ufadhili wa vipindi kutoka kwa wafadhili.
Aidha amesema tekinolojia ya Internet nayo imebadilisha huduma za utangazaji Duniani,watu wengi wamehamia kwenye jukwaa la Internet kupata habari na huduma nyingine kwa njia ya kielectronic.
Kuhusu Changamoto ya kiuchumi kwenye vyombo vya utangazaji Mhandisi Methew amesema kuwa Serikali imechukua hatua ya kupunguza ada za mwaka za leseni za utangazaji kwa takribani asilimia 40 pia imeweza kupunguza ada za masafa Kwa maeneo ambayo hayana tija kibiashara na imeunda kamati ya kuchunguza uchumi wa vyombo vya habari ili kupata hali halisi ya changamoto wanazopitia.
“Matarajio ya serikali ni kwamba kamati hiyo itakuja na majibu sahihi yatakayowezesha serikali kuchukua hatua stahiki zitakazokidhi changamoto za kibiashara zinazokabili vituo hivyo,” amesema na kuongeza
“Hatua za kwanza Serikali iliyochukua ni kupunguza ada za mwaka za leseni utangazaji kwa takribani asilimia 40,” amesema Methew
Naibu Waziri huyo amesema hatua hiyo yote ni dhamira safi ya serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia kuhakikisha kwamba huduma za utangazaji zinaboreshwa.
"Kazi kubwa inayofanywa na Rais Samia ni kuhakikisha kwamba watoa huduma za utangazaji hasa redio zinazidi kuwa na tija katika uchumi wa vituo na taifa kwa ujumla"amesema Methew
Amesema Sekta ya utangazaji imekuwa ikipitia mabadiliko ya kiteknolojia ambayo kila wakati yanahitaji kurejea kanuni za utangazaji ili kwenda na hali halisi iliyopo kwenye soko.
"Historia ya redio na runinga nchini kwa takribani miaka 50 utangazaji wake ulitumia mitambo ya analogia. kwa runinga hadi mwaka 2010 nchi ilihama kutoka kutumia mitambo ya analogia na kwenda wa kidigiti,"amesema Methew
Na kuongeza kuwa "Safari hiyo ya utoaji huduma za utangazaji imekuwa ya mabadiliko, lakini vyanzo vya mapato vya kuendesha vituo vikiwa vile vile. Huduma ya utangazaji kwa kiasi kikubwa inategemea matangazo ya biashara na ufadhili wa vipindi kutoka kwa wafadhili"amesema Methew.
Akizungumzia Siku ya Redio Duniani alivitaka vyombo vya utangazaji nchini kuzingatia kaulimbiu, ‘Redio na Amani’ ili kuhakikisha kuwa maadhui wanayolisha wasikilizaji yanaendelea kuleta amani na umoja nchini.
Naibu waziri huyo amesema matangazo ya redio nchini yanatakiwa kufika mahali popote hasa yale maeneo ya pembezoni ili wananchi wanaoishi katika maeneo hayo waendelee kuwa sehemu ya jamii ya Tanzania.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk Jabir Bakari amesema TCRA inasimamia sekta ndogo tatu ikiwemo mawasiliano ya simu na intaneti, utangazaji pamoja na posta na usafirishaji wa vipeto ambapo katika sekta ya utangazaji hadi kufika Desemba2022 kuna jumla ya watoa huduma 787.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TCRA, Othman Sharif Khatib amesema kaulimbiu ya mkutano huo ni Mchango wa Sekta ya Utangazaji katika kukuza uchumi wa kidigatali, hivyo washiriki wa mkutano huo kama uwanja wa kubadilisha uzoefu na kuelewa fursa zilizopo katika uchumi wa kidigitali katika kuendeleza utangazaji wao.
Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi za Mawasiliano Afrika Mashariki (EACO), Dk.Ally Simba amesema jumuiya imeunda kikosi kazi cha kuandaa mwongozo kuhusu upatikanaji wa redio na mwingiliano katika mipaka ya nchi saba za Afrika Mashariki.
MASWALI NA MAJIBU MUHIMU
Zipi ni hatua za kufuatwa ili kuhakiki laini zangu za simu zilizosajiliwa kwa namba ya Kitambulisho cha Uraia?
JIBU: Ili kuhakiki namba zako zilizosajiliwa kwa namba ya Kitambulisho cha Uraia, fanya kama ifuatavyo: -
KWENYE SIMU YAKO:
Bofya *106#(kisha bonyeza kitufe cha kupiga simu kwa mtandao husika;
Menyu itajitokeza kwenye skrini ya kifaa chako cha mawasiliano ikiwa na vipengele vitano (5);
KUMBUKA: Menyu hii inafanana kwa mitandao yote;
Ikiwa una namba moja pekee kwa Mtandao husika, unashauriwa kuhakiki kama namba yako ya Kitambulisho cha Uraia ilitumika kusajili namba hiyo pekee, au namba nyingine usizozitambua;
Kutekeleza zoezi hili chagua kipengele cha Tatu (3) kwenye menyu inayoonekana kwenye skrini ya kifaa chako. Iwapo utabaini uwepo wa namba za simu usizozitambua fika kwenye duka la Mtoa Huduma wako, ili uzifute.
“Hakikisha unacho kitambulisho chako cha Uraia au NAMBA TAMBULISHI (NIN) ili kukamilisha zoezi hili”
Ikiwa unamiliki namba zaidi ya moja za Mtandao mmoja zilizosajiliwa kwa namba za kitambulisho chako cha Uraia, unapaswa kuzihakiki;
Kutekeleza zoezi hili, chagua kipengele cha Tano (5) kwenye menyu iliyotokeza kwenye skrini ya kifaa chako. Kisha, bofya kipengele namba (1) ili kuchagua Namba Kuu. halafu, rudia kwa kubofya kipengele namba (2) kuhakiki namba za ziada.
Ipi ni tarehe ya ukomo ya zoezi la Uhakiki wa Laini za Simu?
JIBU:
Awali Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) iliweka tarehe-ukomo ya zoezi hili kuwa Januari 31 mwaka huu. Kwa kuona Umuhimu wa kuhakikisha kila Mwananchi anaetumia huduma za Mawasiliano hakosi huduma hizo Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kupitia Waziri mwenye dhamana, Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb.) alitangaza wakati wa Mkutano wake na Waandishi wa Habari Dodoma mnamo tarehe 24 Januari 2023 kuongeza muda wa zoezi hili kutoka tarehe ya awali Januari 31 hadi Februari 13, 2023 saa 10:00 jioni.
Mara baada ya tarehe ukomo kupita laini za simu ambazo hazitakuwa zimehakikiwa kwa kufuata utaratibu uliobainishwa zitazuiliwa KUTOA na KUPOKEA huduma/zitafungwa.
Zipi ni faida na hasara za kutohakiki laini zangu za simu?
JIBU: Faida za kuhakiki laini zako zilizosajiliwa kwa Kitambulisho cha Uraia ni nyingi, kama ifuatavyo: -
Uhakiki unakuhakikishia Usalama wako wewe kama mtumiaji wa huduma za Mawasiliano ya simu;
Ni utekelezaji wa matakwa ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) na Kanuni zake zinazoelekeza kwamba laini zote zisajiliwe kwa utaratibu bayana;
Zoezi hili litawezesha kuondoa kwenye ikolojia ya Mawasiliano simu-laghai zinazosababisha matukio ya uhalifu miongoni mwa watumiaji wengine wa huduma za Mawasiliano ya simu;
Uhakiki unakupa utambulisho thabiti (Digital identity). Unakuwezesha wewe Mwananchi kuwa mshiriki Madhubuti katika Ujenzi wa uchumi wa Taifa lako (Uchumi wa Kidijitali).
Kuboresha Huduma. Taarifa za watumiaji zilizokamilika zinaiwezesha Serikali kupitia TCRA kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za Mawasiliano.
Hasara za kutohakiki ni kama ifuatavyo:-
Utakosa huduma. Laini yako itafungwa.
Kuunganishwa kwenye jinai.
Vipi ikiwa nilimsajilia mtu mwingine Laini ya Simu?
JIBU:
Ikiwa ulimsajilia mtu mwingine laini ya simu, mtake akasajili laini yake kwa utambulisho wake mwenyewe, kwa kufuata utaratibu uliobainishwa; ikiwa ni pamoja na kupata namba ya kitambulisho cha uraia kutoka NIDA.
Wewe uliemsajilia unalazimika/ unapaswa kuwasiliana na mtoa Huduma ili afute usajili wa namba ya huyo uliemsajilia na kuhamisha usajili kwa kutumia utaratibu uliowekwa.
Izingatiwe kwamba: Kila mtumiaji wa Mawasiliano ya simu nchini, aliekidhi vigezo vya kuwa na kitambulisho wa uraia anapaswa kwa mujibu wa kanuni za usajili wa laini za simu, kusajili na kuhakiki laini zake kwa utambulisho wake husika.
Mnasema zoezi hili litapunguza Uhalifu, kivipi?
JIBU:
Ni sahihi kwamba zoezi hili litapunguza matukio ya utapeli mtandaoni kwa kuwa, itakuwa rahisi sasa kumtambua kila mtumiaji wa huduma za Mawasiliano ya simu. Utambulisho halisi wa kila mtumiaji sasa utakuwa umetunzwa vema katika Kanzidata.
Kwa sasa baadhi ya watumiaji wa huduma za Mawasiliano ya simu wenye nia ya kutenda uovu kwenye Mtandao wamekuwa wakijificha kwenye kichaka cha usajili wa watu wengine kwa kutenda makosa ya kimtandao kwa kuwa usajili wa laini za simu wanazotumia si wa kwao;
Hivyo, tukihakiki wote na kuondoa namba tusizozitambua na kuhakikisha wale tuliowasajilia wao pia wanasajili laini zao wao wenyewe tutafanikiwa kupunguza matukio ya utapeli mtandaoni kwani kila mtumiaji atatambuliwa kwa laini yake ya simu anayotumia.
Ilikuwaje watu wakawa na laini za simu zisizokuwa na utambulisho wao?
Baadhi ya mawakala wa watoa huduma hawakuwa waaminifu, walikuwa wakiwasajilisha wenye vitambulisho zaidi mara moja na kutengeneza laini za simu za ziada, tofauti na ile ya muhusika kisha kuziuza laini hizo, ambazo wenye nia mbaya wamekuwa wakizitumia kutenda makosa ya kimtandao;
Mawakala hawa wasio waaminifu TCRA tuliwadhibiti kwa kushirikiana na Watoa Huduma, na tukatoa maelekezo kwa Watoa Huduma kuhakikisha mawakala wao wanazingatia sheria na taratibu zilizopo wanaposajili laini za watumiaji wapya au wale wanaohitaji kuongeza laini za simu;
Nikufahamishe kwamba tumeendelea kuzifutia huduma laini hizi za simu zinazotenda makosa mtandaoni ambapo hadi Novemba mwaka jana 2022 tulifungia laini zaidi ya 52,000 zikiwemo zilizokuwa zikijihusisha na utapeli.
Baada ya tarehe ya mwisho kupita 13/02/2023 ndiyo itakuwa basi tena?
JIBU: Zoezi hili ni endelevu. Hata hivyo kwa wale wenye laini zinazotumika sasa, ikiwa hawatakuwa wametekeleza takwa la uhakiki tutaziondolea huduma itakapofika tarehe ya ukomo, ili kuhakikisha kila mtumiaji wa huduma za Mawasiliano, anatambuliwa na kumbukumbu yake inatunzwa kwenye Kanzidata, hii itawezesha Serikali yetu kuwa na takwimu sahihi na kamili za watumiaji halisi wa huduma za Mawasiliano ya simu, intaneti na huduma za kifedha mtandaoni.
Ikiwa nitabaini uwepo wa namba za simu nisizozitambua baada ya kutekeleza zoezi la Uhakiki, nifanyeje?
JIBU: Fika kwenye duka la Mtoa Huduma wako, kisha toa Taarifa ya namba hizo ili ziweze kufutwa kwa kuzingatia utaratibu wa bayometria na kuwasilisha namba za Kitambulisho chako cha uraia.
Je, mnafikiria kuongeza Muda zaidi?
Tayari muda umeongezwa kutoka tarehe-ukomo ya wali ambayo ilikuwa Januari 31, 2023 na sasa zoezi la uhakiki wa laini za simu zinazotumika limeongezewa muda hadi Februari 13, 2023.
Zoezi hili la kuhamasisha uhakiki wa laini za simu zinazotumika lilianza Desemba 2021.
Mnataka kufunga hilo zoezi mbona wananchi hatujapata Taarifa za kutosha?
Kampeni hii ya Elimu tunaiendesha kwa ushirikiano na watoa huduma wote wa huduma za Mawasiliano ya simu. Kwa upande wao wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii, pia wamekuwa wakituma ujumbe wa moja kwa moja kwa watumiaji wote wa Mawasiliano ya simu wakiwakumbusha kila mtumiaji wa huduma za Mawasiliano ya simu kuhakiki laini zao za simu. Hivyo, TCRA tunaamini kila mtumiaji wa Mawasiliano ya simu amepokea Taarifa hizi za uhakiki kupitia ujumbe mfupi uliotumwa na watoa huduma, au kupitia kurasa za mitandao ya kijamii ya TCRA, watoa huduma na Wizara ya sekta.
Zoezi linaendaje hadi sasa?
Zoezi linaendelea kwa mafanikio makubwa. Hadi sasa zaidi ya asilimia 90 ya laini za simu zinazotumika nchini zimehakikiwa. Hivyo hima! mtumiaji wa huduma za Mawasiliano wewe ambae bado hujakamilisha uhakiki wa laini zao za simu, tekeleza zoezi hilo sasa kwa kubofya *106# kisha fuata maelekezo.
Muhimu kukumbuka ni kwamba itakapofika tarehe 13 Februari 2023 kama laini yako haijahakikiwa itazuiliwa kutoa na kupokea huduma. Hakiki sasa!

KAMATI ya kudumu ya Miundombinu ya Bunge imefanya ziara katika Ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kupata maelezo ya usimamizi wa mnada wa msafa utakaoiwezesha Serikali kupata Dola za Kimarekani milioni 187.4.
Aidha wajumbe wa kamati hiyo wameelezwa namna vitalu vya masafa vitakavyowezesha utoaji wa huduma za ziada za mawasiliano ikiwemo intaneti ya kasi ya Kizazi cha Tano yaani “5G.”
Mbali na hayo, Kamati hiyo imepokea maelezo kwamba Tanzania ni nchi ya kwamza barani Afrika kuuza Masafa yenye thamani kubwa kwa mfumo huu, kwa kutumia wataalam wa ndani kwa mafanikio makubwa.
Kamati hiyo pia ilielezwa mafanikio katika usimamizi wa sekta ya Mawasiliano nchini, uliotolewa na wataalam wa Mawasiliano wa TCRA na Wizara inayosimamia sekta ya Mawasiliano nchini.
Ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Selemani Kakoso, kamati imepokea wasilisho kuhusu mnada wa masafa uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam ulioshuhudia watoa huduma za Mawasiliano ya simu watano wakipata masafa kwa ajili ya kuwezesha huduma za mawasiliano katika teknolojia za kizazi cha nne yaani 4G na 5G.
“Naamini kwamba sekta ya Mawasiliano ni sekta muhimu kwa kuwa inatengeneza uchumi wa nchi yetu,” alisisitiza Kakoso.
Akiwasilisha mbele ya kamati hiyo, Dk Jabiri Bakari, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA aliwaeleza wajumbe wa kamati kwamba jumla ya vitalu 11 vya masafa viliuzwa kupitia Mnada huo wa masafa uliofanyika kwa njia ya uwazi na kuwezesha watoa huduma kupata rasilimali hiyo adimu inayowezesha Mawasiliano.
“Masafa ni moja ya rasilimali za nchi kama ambavyo tuna rasilimali zingine kama vile rasilimali madini au rasilimali ardhi; masafa kama rasilimali inawezesha kubeba taarifa kutoka upande mmoja kwenda mwingine, inaweza kuwa katika mfumo wa picha, sauti au data,” alifafanua.
“Utaratibu wa kugawa masafa kwa njia ya Mnada ni utaratibu ambao unatumika kimataifa na tumefanikiwa kuendesha zoezi la ugawaji wa vitalu kwa mafanikio. Kabla ya utaratibu huu masafa yalikuwa yanagawiwa kwa utaratibu wa ‘first come first served’ yaani atakaewahi ndie huyo anahudumiwa, ilikuwa mtu mmoja anaweza kuchukua masafa zaidi kiasi kwamba mtu mwingine akija akiambiwa masafa yamekwisha yanakuwa yamekwisha,” aliongeza.
Alifafanua kuwa utaratibu wa masafa kwa njia ya Mnada umeongeza uwazi juu ya zoezi la ugawaji masafa na kuongeza Imani kwa watoa huduma wanaohitaji rasilimali hiyo, kwa kuzingatiwa kuwa wanashirikishwa kila hatua.
Mbele ya kamati hiyo, TCRA ilitoa maelezo juu ya utendaji kazi wa Mamlaka, utoaji na usimamizi wa Leseni za Mawasiliano, ambapo wajumbe wa Kamati walipata wasaa wa kuuliza maswali mbalimbali yaliyotolewa ufafanuzi na wataalam wa Mamlaka.
Akizungumza wakati wa majumuisho baada ya kupokea maelezo ya wataalam wa TCRA, Menejimenti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Kakoso ameipongeza Mamlaka hiyo katika kuleta mapinduzi kwenye sekta.
Mwenyekiti Kakoso katika majumuisho baada ya kupokea maelezo na Menejimenti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habar alipongeza
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt Jabiri Bakari
Na Mwandishi Wetu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imebainisha kuwa maelfu ya namba za simu zilizojihusisha na wizi, utapeli na ulaghai kupitia Mtandao wa simu zimefungwa.
Akizungumza jijini Dodoma hivi karibuni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt Jabiri Bakari, alisema kuwa jumla ya namba tambulishi Hamsini na Mbili Elfu na Themanini na Saba 52,087 zikiwemo zilizoripotiwa kupotea, kuibiwa au kuhusika katika matukio ya kihalifu zimezuiliwa kupokea na kutoa huduma za Mawasiliano.
“Kwa mfano, Kuanzia Julai 2021 hadi kufikia Septemba 2022 jumla ya namba tambulishi (IMEI) zilizofungiwa na mfumo huu ni 52,087 ambazo ziliripotiwa kupotea, kuibiwa au kuhusika katika matukio ya kihalifu, hivyo kuwezesha kupunguza matukio ya wizi na kusaidia upatikanaji wa vifaa vya Mawasiliano vyenye ubora kwenye soko,” alisisitiza Dkt. Bakari.
Alieleza kuwa, kupitia kanzidata ya Namba Tambulishi (Central Equipment Identity Register), moduli hiyo imewezesha uhakiki wa vifaa vyote vinavyounganishwa na mitandao ya watoa huduma kama vinakidhi viwango vya kimataifa na ni salama kwa watumiaji.
Moduli hiyo iliyopo katika Mfumo wa Usimamizi wa Mawasiliano (TTMS) imewezesha kuzuia matumizi ya simu zilizoripotiwa kuibiwa, kupotea au kuharibika pamoja na kuzuia matumizi ya simu zisizokuwa na viwango.
“Usimamizi huu unawezesha kubaini na kufungia namba tambulishi za vifaa vya Mawasiliano zilizonakiliwa (Duplicate IMEIs), namba tambulishi za vifaa vilivyotumika kwenye udanganyifu pamoja na namba tambulishi zilizotolewa taarifa ya kupotea au kuibiwa,” aliongeza.
Wakizungumza na gazeti hili baadhi ya wananchi akiwemo Mpoki Mwakabinga mkazi wa Kinondoni Dar es salaam waliishukuru Mamlaka ya Mawasiliano kwa jitihada inazofanya kuhakikisha uhalifu mtandaoni hasa unaohusisha vifaaa vya Mawasiliano kiganjani unatokomezwa kwa ushirikiano na vyombo vya ulinzi na Usalama.
“Tunaishukuru TCRA, hakika inajitahidi sana kuwalinda wananchi kupitia mifumo yake ya usimamizi wa Mawasiliano, hawa matapeli wamekuwa wengi kiasi kwamba tunakuwa na wasiwasi, kama wanafungiwa hili ni jambo la heri,” alibainisha Mpoki.
Mamlaka hiyo awali ilieleza kuwa watumiaji wa huduma za Mawasiliano ya simu mara wanapobaini kupokea simu au ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) wenye viashiria vya utapeli wanapaswa kutoa taarifa kwa kutuma ujumbe mfupi wenye neno “utapeli” kwenda namba 15040 na kutuma namba ya tapeli kwenda namba hiyohiyo.
Aidha TCRA ilisisitiza kila mtumiaji wa huduma za Mawasiliano ahakikishe anahakiki namba zake za simu zilizosajiliwa kwa njia ya kibayometria, kwa kutumia namba ya kitambulisho cha Taifa wanapaswa kubofya *106# kisha kufuata maelekezo.
Na Janeth Raphael
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Kuwe amesema kuwa Uwiano baina ya mitandao na matumizi yanaonesha kuwa maeneo mengi yamefikiwa na huduma za Intanet ila watumiaji ni wachache hivyo kuna haja ya kuongeza upatikanaji wa simu janja.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa Majukumu ya Mamlaka hiyo kuanzia Julai 2021 hadi Septemba 2022 , mbele ya waandishi wa habari Novemba 3,2022,Jijini Dodoma ,Dkt.Jabir amesema kuwa Muelekeo wa kufikia lengo la serikali la asilimia 80 ya watumiaji wa huduma za Intanet ifikapo mwaka 2025 zinaendela vema.
"Tuna haja ya kuangalia nini kifanyike ikiwezekana kuongeza kwa kasi elimu ya matumizi ya simu janja na kuongeza upatikanaji wake kwa wananchi kwani Uwiano baina ya mitandao na matumizi yanaonesha kuwa maeneo mengi yamefikiwa na huduma za Intanet ila watumiaji ni wachache ,"Ameeleza Dkt.Jabir
Dkt.Jabir amesema kuwa Sekta ya Mawasiliano ya Simu nchini imeendelea kukua na hadi kufikia Septemba, 2022 kulikuwa na laini za simu 58.1 Milioni, Idadi hii ya laini za simu inahusisha laini zinatotumiwa na watu na laini zinatumiwa kwa ajili ya mawasiliano kati ya mashine kwa mashine (M2M).
"Takwimu zinaonyesha kwamba mikoa mitano (5) Tanzania inayoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya laini za simu zinazotumika yaani (Active SIM-cards) hadi Septemba 2022 ni Dar es salaam (Laini Milioni 9,756,697), Mwanza (Laini 3,700,914), Arusha (3,448,200), Mbeya (3,089,848), na Tabora (3,060,407),"Amesema Dkt.Jabir
Dkt.Jabir amebainisha kuwa Takwimu za sasa zinaonesha kuwa matumizi ya Intaneti yameongezeka kwa asilimia 4.2 kutoka milioni 29,858,759, mwaka 2021 hadi kufikia 31,122,163 mwezi Septemba 2022.
"Idadi ya watumiaji wa intaneti kwa sasa wamefikia 31,122,163,Mwelekeo wa ongezeko la watumiaji wa intaneti linaonesha kwamba kulikuwa na ukuaji wa takriban asilimia 17 kila mwaka, katika kipindi cha miaka 5 ambapo mwaka 2017, kulikuwa na watumiaji Milioni 16,106,636 na mwishoni mwa mwaka 2021 waliongezeka kufikia Milioni 29,103,482,
Na kuongeza kuwa "Ongezeko la matumizi ya intaneti limechangiwa pia na matumizi ya Kiswahili, Maudhui ya Kiswahili kwenye intaneti yanaongezeka kwa kasi na Program tumizi (applications) kwa lugha ya Kiswahili zimeongezeka pia,"Ameeleza Dkt.Jabir
Akizungumzia takwimu za ripoti ya utendaji wa sekta ya Mawasiliano nchini Mkurugenzi huyo amebainisha kuwa kuna mitandao mitano (5) ya kijamii inayotumiwa zaidi, hivyo kuongoza kwa kiwango kikubwa cha data iliyotumika kwa kipimo cha GB; ambapo Mtandao wa kijamii wa FaceBook uliongoza kwa kurekodi (GB Bilioni 2.59), ukifuatiwa na YouTube wenye (GB Bilioni 1.91), kisha WhatsApp uliokuwa na (Bilioni 1.58), na TikTok ukiwa na (GB Milioni 999) ikifuatiwa na mitandao mingine.
Pia ,Dkt.Jabir amesema kuwa TCRA inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kama UCSAF, Watoa huduma za mawasiliano, TANESCO, Wakala wa Umeme Vijijini (REA), Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA) pamoja na kuchangia katika Mfuko wa Mawasiliano kwa wote ili kuhakikisha kuwa huduma za Mawasiliano zinafikishwa kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inaendelea kusimamia Sekta ya Mawasiliano ikiwa ni pamoja na kushirikiana na wadau mbalimbali katika ngazi ya Kitaifa, Kikanda na Kimataifa ili kuhakikisha Sekta ya Mawasiliano inatoa mchango katika maendeleo ya nchi na kuwa kichocheo cha ukuaji wa uchumi wa kidijiti na uchumi wa buluu.
Na Chalila Kibuda
Ripoti ya Utendaji wa Kisekta imeonesha ongezeko la asilimia 3.4 kwa laini za simu zinazotumika, ambapo hadi mwezi Juni 2022 kulikuwa na laini Milioni 56.2 idadi iliyoongezeka hadi kufikia laini milioni 58.1 mwezi Septemba 2022.
Takwimu zinaonyesha kwamba mikoa mitano nchini inayoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya laini za simu zinazotumika yaani (Active SIM-cards) hadi Septemba 2022 ni Dar es Salaam (laini Milioni 9,756,697), Mwanza (laini Milioni 3,700,914), Arusha (laini Milioni 3,448,200), Mbeya (laini Milioni 3,089,848) na Tabora (laini Milioni 3,060,407).
Ameyasema hayo leo Oktoba 25,2022 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk. Jabir Bakari wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema uchambuzi wa laini hizo kwa watoa huduma unaonyesha kwamba kuna ushindani mkubwa kwani hakuna mtoa huduma mwenye zaidi ya asilimia 35 ya laini ya zilizosajiliwa.
"Mwelekeo wa usajili kwa miaka mitano iliyopita unaonyesha ongezeko la asilimia nane kwa mwaka. Kuenea kwa laini miongoni mwa watu kumeongezeka kwa asilimia nne kwa mwaka. Kuenea kulikuwa asilimia 78 mwaka 2017, asilimia 81 mwaka 2018 , asilimia 88 mwaka 2020 na asilimia 91 mwaka 2021". Amesema.
Aidha amesema wastani wa gharama za vifurushi vya simu zilikuwa shilingi 7.8 kwa kupiga simu ndani ya mtandao Septemba 2022, kutoka shilingi 7.7 Juni 2022. Pamoja na ongezeko hili dogo, gharama bado ni chini kulinganisha na vifurushi vya simu kwenda mitandao mingine". Amesema.
Amesema wastani wa vifurushi vya simu kwenda mitandao mingine ulikuwa shilingi 8.1 Septemba 2022, ikiwa ni ongezeko kutoka shilingi 7.6 Juni 2022.
Hata hivyo amesema watumiaji wa intaneti wameongezeka kutoka 29,169,958 Juni 2022 hadi 31,122,163 Septemba 2022 sawa na ongezeko la asilimia 6.7.
"Mwelekeo wa ongezeko la watumiaji wa intaneti linaonesha kwamba kulikuwa na ukuaji wa takriban asilimia 17 kila mwaka, katika kipindi cha miaka 5 ambapo mwaka 2017, kulikuwa na watumiaji Milioni 16,106,636 na mwishoni mwa mwaka 2021 waliongezeka kufikia Milioni 29,103,482". Ameeleza.
Ameeleza kuwa matumizi ya intaneti yameongezeka kutoka wastani wa MB 6,037, kwa mtumiaji Machi 2022 hadi MB 6,626 kwa mtumiaji Septemba 2022.















.jpg)


