Na; Elizabeth Paulo,Dodomaa

Naibu Waziri wizara ya habari mawasliano na Taknologia ya habari Mhandisi Kundo Methew amesema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wote wa sekta ya habari na utangazaji katika maendeleo ya Taifa.

Mhandisi Methew amesema hayo leo Februari 13 jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa mwaka wa watoa huduma wa sekta ya utangazaji Tanzania uliyoenda sambamba na siku ya radio Duniani.

Amesema Serikali ipo tayari kushirikiana na wadau wa habari na utangazaji, huduma ya utangazaji imekuwa na mabadiliko makubwa huku vyanzo vya mapato vya kuendesha vituo vikiwa vilevile,na huduma ya utangazaji Kwa kiasi kikubwa inategemea matangazo ya biashara na ufadhili wa vipindi kutoka kwa wafadhili.

Aidha amesema tekinolojia ya Internet nayo imebadilisha huduma za utangazaji Duniani,watu wengi wamehamia kwenye jukwaa la Internet kupata habari na huduma nyingine kwa njia ya kielectronic.

Kuhusu Changamoto ya kiuchumi kwenye vyombo vya utangazaji Mhandisi Methew amesema kuwa Serikali imechukua hatua ya kupunguza ada za mwaka za leseni za utangazaji kwa takribani asilimia 40 pia imeweza kupunguza ada za masafa Kwa maeneo ambayo hayana tija kibiashara na imeunda kamati ya kuchunguza uchumi wa vyombo vya habari ili kupata hali halisi ya changamoto wanazopitia.

“Matarajio ya serikali ni kwamba kamati hiyo itakuja na majibu sahihi yatakayowezesha serikali kuchukua hatua stahiki zitakazokidhi changamoto za kibiashara zinazokabili vituo hivyo,” amesema na kuongeza 

“Hatua za kwanza Serikali iliyochukua ni kupunguza ada za mwaka za leseni utangazaji kwa takribani asilimia 40,” amesema Methew

Naibu Waziri huyo amesema hatua hiyo yote ni dhamira safi ya serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia kuhakikisha kwamba huduma za utangazaji zinaboreshwa.

"Kazi kubwa inayofanywa na Rais Samia ni kuhakikisha kwamba watoa huduma za utangazaji hasa redio zinazidi kuwa na tija katika uchumi wa vituo na taifa kwa ujumla"amesema Methew

Amesema Sekta ya utangazaji imekuwa ikipitia mabadiliko ya kiteknolojia ambayo kila wakati yanahitaji kurejea kanuni za utangazaji ili kwenda na hali halisi iliyopo kwenye soko.

"Historia ya redio na runinga nchini kwa takribani miaka 50 utangazaji wake ulitumia mitambo ya analogia. kwa runinga hadi mwaka 2010 nchi ilihama kutoka kutumia mitambo ya analogia na kwenda wa kidigiti,"amesema Methew 

Na kuongeza kuwa "Safari hiyo ya utoaji huduma za utangazaji imekuwa ya mabadiliko, lakini vyanzo vya mapato vya kuendesha vituo vikiwa vile vile. Huduma ya utangazaji kwa kiasi kikubwa inategemea matangazo ya biashara na ufadhili wa vipindi kutoka kwa wafadhili"amesema Methew.

Akizungumzia Siku ya Redio Duniani alivitaka vyombo vya utangazaji nchini kuzingatia kaulimbiu, ‘Redio na Amani’ ili kuhakikisha kuwa maadhui wanayolisha wasikilizaji yanaendelea kuleta amani na umoja nchini.

Naibu waziri huyo amesema matangazo ya redio nchini yanatakiwa kufika mahali popote hasa yale maeneo ya pembezoni ili wananchi wanaoishi katika maeneo hayo waendelee kuwa sehemu ya jamii ya Tanzania.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk Jabir Bakari amesema TCRA inasimamia sekta ndogo tatu ikiwemo mawasiliano ya simu na intaneti, utangazaji pamoja na posta na usafirishaji wa vipeto ambapo katika sekta ya utangazaji hadi kufika Desemba2022 kuna jumla ya watoa huduma 787.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TCRA, Othman Sharif Khatib amesema kaulimbiu ya mkutano huo ni Mchango wa Sekta ya Utangazaji katika kukuza uchumi wa kidigatali, hivyo washiriki wa mkutano huo kama uwanja wa kubadilisha uzoefu na kuelewa fursa zilizopo katika uchumi wa kidigitali katika kuendeleza utangazaji wao.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi za Mawasiliano Afrika Mashariki (EACO), Dk.Ally Simba amesema jumuiya imeunda kikosi kazi cha kuandaa mwongozo kuhusu upatikanaji wa redio na mwingiliano katika mipaka ya nchi saba za Afrika Mashariki.


Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: