Saimon Maximilian Iranghe ameibuka kuwa Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha (UVCCM).
Msimamizi Mkuu wa uchaguzi huo wa Vijana Mkoa wa Arusha Thomas Apson ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro amemtangaza kuwa mshindi, baada ya kupata kura 345 kati ya kura zilizopigwa. 555
Thomas Apson alitangaza matokeo wakati wa uchaguzi wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Simba Hall (AICC)
Thomas Apson aliwashukuru wajumbe kwa kufanya uchaguzi wa uhuru na haki na kumtaka Mwenyekiti mpya na Mwenyekiti alipita kumaliza tofauti zao na kujenga chama imara.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha Mussa Matoroka amesema uchaguzi ulikuwa wa huru na haki na tunaendelea na chaguzi nyingine ndani ya Jumuiya zetu ngazi ya Mkoa ila pia niendelee kuwasihi wanachama wa CCM Mkoa wa Arusha kuwa watulivu ili tuweze kumalizia chaguzi zetu salama ila msisahau kwenda kutangaza yale yote mazuri yanayofanyika na yanafanywa na Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye ndiye Rais wetu wa Awamu ya Sita Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake Mwenyekiti huyo mpya, Saimon Maximilian Iranghe aliwataka vijana wote kufanya kazi kwa ushirikiano na kwamba uchaguzi umeisha na wote sasa ni kitu kimoja.
“Makundi sasa yaishe, tunachotakiwa vijana wenzangu kwa sasa tufanye kazi kwa bidii na kujenga chama chetu,” amesema Saimon.
Aliwashukuru wapiga kura kwa kumchagua kuwa Mwenyekiti na kuahidi kufanya kazi kwa ushirikiano na viongozi wapya pamoja na wale waliomaliza muda wao.
1.NAFASI YA MWENYEKITI UVCCM MKOA
1.Simon Maxmillian Iraghe Kura 345
2. Nicomed Axweso Josephat Kura 04
3.Mwinyi Said Njuhe Kura 08
4.Ikoyo Kilaye Laizer Kura 155
2.NAFASI YA MJUMBE WA BARAZA KUU TAIFA NA MKUTANO MKUU WA CCM TAIFA.
1.Tezra Furaha Semuguruka Kura 351
2.Baraka Joseph Shayo Kura 09
3.Norris Harry Minja Kura 15
4.Mohamed Khalifan Mwanga Kura 120
5.Rachel Stori Jumbe Kura 50
3.NAFASI YA MJUMBE WA MKUTANO MKUU WA UVCCM TAIFA
1.Alice Gaudence Mbaga Kura 181
2.Jacob Melembuki Mollel Kura 69
3.Happyness Samwel Laizer Kura 221
4. NAFASI YA MJUMBE WA MKUTANO MKUU CCM MKOA
1.Monica Joram Lukumay Kura 74
2.Ikoyo Kilaye Laizer Kura 195
3. Paulo Godwel Lukumay Kura 187
5.NAFASI YA MJUMBE KUWAKILISHA JUMUIYA YA UWT MKOA
1.Aminata Salash Toure Kura 218
2.Fatuma Sahimu Kimaro Kura 73
3.Tezra Furaha Semuguruka Kura 116
6.NAFASI YA MJUMBE WA MKUTANO MKUU UVCCM MKOA
1.Hassan Mohamed Abdul Kura 117
2.Marry Fulgence Mosha Kura 198
3. Alice Gaudence Mbaga Kura 154
7. NAFASI YA MJUMBE WA KUWAKILISHA JUMUIYA YA WAZAZI
1.David Msyoki Sainguran Kura
2.Esupath Mbaraka Laizer Kura 310
3.Rajabu Selemani Mwaliko Kura 127
Post A Comment: