Na Elizabeth Joseph, Monduli.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mh,Isack Copriano amemtaka Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh,Fredrick Lowassa kuhudhuria vikao vya Baraza la madiwani na sio kutuma mwakilishi.

Ameyasema hayo Novemba 30 wakati wa mkutano wa kawaida cha Baraza la madiwani baada ya Katibu wa Mbunge huyo Bw,Zacharia Murianga kuonekana mara kwa mara kwenye vikao vya mkutano wa Baraza hilo na kukaa kwenye nafasi ya Mbunge kama mwakilishi wake.

Copriano alibainisha kuwa kwa Kipindi Cha miaka mitatu  Mbunge huyo amehudhuria mikutano ya Baraza hilo mara moja pekee jambo ambalo alioneshwa kuchukizwa nalo na hivyo kumuelekeza Katibu wake kutoka katika kiti cha Mbunge na kumtaka akae katika viti vya wageni walioalikwa kuhudhuria mkutano huo.

"Kama Mbunge haudhurii vikao vya Baraza hakuna haja ya kutuma mwakilishi,Katibu utakuwa msikilizaji kama mwananchi wa kawaida tu sababu kanuni zetu haziruhusu wewe kukaa mbele kama mwakilishi"alisisitiza Mwenyekiti huyo.

Aidha alisisitiza alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Raphael Siumbu kuhakikisha Wakuu wa Taasisi za serikali ikiwemo Maji, TANESCO,TARURA wanapewa taarifa za vikao hivyo ili wafike na kujibu hoja zinazoibuliwa na madiwani zinazohusu changamoto katika Kata zao.

 "Kwenye vikao vya Baraza hatuhitaji wawakilishi Kama ni Meneja wa maji ama TANESCO afike yeye na sio kutupa wawakilishi wasio na majibu ya kutosha"alieleza Mheshimiwa Copriano.

Hata hivyo akijibu suala hilo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Raphael Siumbu alioneshwa kusikitishwa na tabia hiyo na kuongeza wakuu wa Taasisi hizo wamekuwa wakiandikiwa Barua kila mara na kuelezwa juu ya umuhimu wa wao kuhudhuria vikao hivyo na kusema imekuwa kawaida ya wao kutuma wawakilishi.

"Viongozi hawa wametumwa kuhudumia wananchi hivyo wanapokosekana katika vikao hivi ina maana na wananchi wanakosa majibu wanayoyahitaji katika kutatua changamoto zao hivyo nadhani sasa tuandike barua hata kwenye Wizara zao ili kukabiliana na changamoto hii"aliongeza Siumbu.





Share To:

Post A Comment: