Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa Ndg, Fadhili Maganya, amesema kuwa Rais Samia suluhu ataendelea kushika dola hadi 2030 na kueleza kwa wale wasiopenda awepo wake madarakani au kusifiwa wajinyonge au wanywe sumu. 

Maganya amesema hayo leo ,Jijini Arusha alipo kuwa akiongea na uongozi wa Jumuiya hiyo ya wazazi mkoani hapa na kuonya vikali wanachama wa CCM wanaoendekeza chuki, fitna na makundi baada ya chaguzi kumaliziki kitu ambacho kinazaa unafiki ndani ya chama.

Maganya amedai kuibuka kwa watu hapa nchini wanao teseka kusikia Rais Samia akisifiwa juu ya utendaji kazi wake hasa katika swala zima la kuleta maendeleo ya nchi.

"Nataka niwaeleze ukweli nimechaguliwa hivi karibuni katika nafasi hii ila ni mwanachama wa siku nyingi na huu wakati ni wa mungu umekuja mimi kuongoza, niwahakikishie katika kipindi changu cha uongozi hakuna mtu yeyote atakae mgusa Rais samia nitakula naye sahani moja maana tunahitaji maendeleo na siyo maneno". Alisema Maganya.

"Na niwambie tu wale wanao teseka zaidi wachague vitu viwili kunywa sumu au wajinyonge ili wasione Samia akiongoza nchi, Pia kwasasa wana CCM tumemaliza uchaguzi naamini makundi yote yamevunjwa ila nikigundua bado kuna makundi ya kutafutiana ajali nitadili nao maana Arusha naijua vizuri". Aliongeza Maganya.

Aidha aliweka wazi kuwa yeye ni muumini wa uwazi na ukweli amewataka wanachama wa CCM kote nchini kukitetea chama ipasavyo na kwa wale ambao hawata fanya hivyo basi waanze kujiondoa kwenye siasa za chama hicho na waache tabia ya kusubilia wakati wa uchaguzi na kuanza kukivuta miguu chama hicho.

"Kwa wale wanakivuta chama miguu na kusubilia wakati wa uchaguzi nataka niwambie nitawafyeka wote na watasubilia sana majina yao kurudishwa itabaki stori maana hatuwezi kuwa na watu wanaokuponda chama huku wanataka uongozi kwa chama hicho chicho ambacho hawakisemei". Alisema Mganya.

"Najua chama chetu kilipitoa wakati mgumu sana manusula kifutwe ila kwasasa kimesimama imara na kitazidi kusimama na sita sita kuwa kuwasema ukweli wale wanao fanya vizuri ndani ya chama na ukiwa unatusumbua hata kukiwa na nafasi gani ya jina lako nitakutaja kuwa hufanyi vizuri katika chama kifupi huto tufaa ili tubaki na wachache waadilifu kwa chama na Taifa". Aliongeza.

Aidha Maganya aliutaka uongozi wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa Arusha kutafuta kiwanja kwaajili ya uwekezaji na atakikagua atakapo anza ziara za kila mkoa kwani mikakati ya kitaifa ni kujenga Hosptali ya rufaa, kujenga mashule pamoja na kuweka mashamba ya mifugo kila kanda hapa nchini.

Awali katibu wa jumuiya hiyo Mkoa wa Arusha, Deogratius Nakey alimwomba mwenyekiti huyo mpya kurejesha miradi ya jumuiya hiyo ambayo imekuwa na mgogoro na jamii kwa muda mrefu na kutimiza kiu ya Jumuiya ya wazazi hapa nchini.

"Ndg Mweyekiti wetu tunajua umeshinda kwa kishindo kikubwa ila tunakuomba katika utendaji kazi wako uweze kutimiza kiu ya wanajumuiya ya wazazi hapa nchini kwani viatu hivyo vinakutosha na umekuwa mwanasiasa muda mrefu na unajua kila kitu ndani ya juiya yetu". Alisema Nakey.

Nae katibu wa CCM Mkoa wa Arusha Mussa Matoroka aliushukuru uongozi wa Juiya hiyo kwa kuwa watulivu katika uchaguzi wao tofauti na juiya zingine zilitumia rushwa na ubadhilifu mwingine kwa wajumbe lakini wakaona na ngazi ya taifa na kuchukua uamuzi juu ya mambo hayo. 




Share To:

Post A Comment: