Mkuu wa mkoa wa Tanga (katikati)  Omari Mgumba akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya uchunguzi wa moto uliounguza ghala lililokuwaa likimilikiwa na Mamalaka ya Mapato Tanzania TRA.

Na Denis Chambi, Tanga. 

Mkuu wa mkoa wa Tanga Omari Mgumba ametoa maagizo ya kusimamishwa kazi watumishi 21 wakiwemo 6 kutoka mamalaka ya usimamizi ya Bandari na wengine 7 wa Mamlaka ya mapato Tanzania mkoa wa Tanga kufwatia tuhuma zinazowakabili kutokana na tukio la kuungua moto ghala lililokuwa limehifadhia bidhaa zilizokamatwa kwa magendo na zile zilizoshindwa kulipiwa. 

Maagizo hayo ameyatoa November 29 mara baada ya kupokea taarifa iliyotolewa na kamati maalumu aliyoiunda kwaajili ya kuchunguza tukio hilo lililotokea hivi karibuni ambapo taarifa zimeonyesha kuwa hakukuwepo na viashiria vyovyote vya hitilafu ya umeme iliyopelekea kuungua kwa ghala hilo lililokuwa eneo la bandari ambalo linalomilikiwa na mamlaka ya mapato Tanzania. 

Watumishi hao 6 wa mamlaka ya bandari 'TPA' wote ni walinzi huku wengine 7 wa kutoka mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa Tanga wanaotuhumiwa na makosa ya kiutendaji ni kutoka vitengo mbalimbali vya forodha wakiongozwa na meneja forodha mkoa wa Nassoro Kupaza na mkuu wa kitengo cha kuzuia magendo mkoa David Kisanga.

 "Jambo la kwanza watuhumiwa hawa wote waliotuhumiwa wa mamlaka ya bandari 6 wote waendelee kusimama kazi kuanzia leo kupisha uchunguzi wa kina utakaofanywa na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, watumishi 7 wa TRA wanaotuhumiwa kwa makosa ya kiutendaji na makosa ya uzembe wote hawa wasimame kupisha uchunguzi wa kina utakaofanywa na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama" alisema Mgumba. 

Aidha Mgumba ameagiza mtumishi mmoja wa shirika la viwango Tanzania TBS pamoja na wengine walinzi 7 wa kampuni ya ulinzi ya Suma JKT wasimame kupisha uchunguzi na kutokupangiwa lindo lolote kwa mkoa wa Tanga wala kujishughulisha na shuguli zozote za ubebaji mizigo ndani ya bandari.

 "Kutoka Suma JKT watumishi 7 wote wasimame kupisha uchunguzi na ni marufuku kufika kwenye bandari yeyote mkoa iliyokuwemo katika mkoa wa Tanga na hata hao walinzi wasipangiwe lindo lolote , mtumishi wa TBS naye asimame kwa makosa anayotuhumiwa ikiwemo kuchukua sampuli ya mafuta nyingi zaidi ya kiwango kinachohitajika"

 Mgumba pia ameagiza kukamatwa wafanyabiashara watatu ambao pia ni wamiliki wa vitenge vilivyokamatwa kwa njia ya magendo Abdila Ally 'Balozi' Siami Lukuni na Said Salimu wote wakamatwe kuhusiana na tuhuma zinazowakabili. 

"Watu wengine Bwana Abdila Mohammed mfanyabiashara wa vitenge vyote tulivyovikamata kamati imekiri mmiliki ni mmoja akamatwe popote alipo ili kujibu tuhuma , Siami Lukuni, na Salimu Said, TAKUKURU, jeshi la polisi na vyombo vingine vya usalama wakamateni haoa watuhumiwa wote ili wajibu tuhuma za kijinai wanazokabiliana nazo" . 

Hata hivyo Mgumba pia amewataka viongozi wa ngazi za juu katika mamlaka ya Bandari Tanzania TPA pamoja na mamlaka ya Mapato Tanzana TRA kuwachukulia hatua za kinidhamu watumiahi wote aliotangaza kusimamishwa kazi huku akiwataka mamenja wa ofisi hizo mkoa kujitathmini kiitendaji. 

" Kamishna wa mamlaka wa mamlaka ya mapato Tanzania 'TRA' pamoja na mkurugenzi wa bandari 
'TPA' ambao kimsingi ndio wakuu wa chombo hichi kuchukuwa hatua za kinidhamu kwa watuhumiwa wote kwa makosa ya kiutendaji kwa mujibu wa sheria , kanuni na taratibu haya sio ya TAKUKURU ni ya wakuu wa kazi"

 "Meneja TRA mkoa wa Tanga na meneja Bandari mkoa wa Tanga kwa haya ya kizembe kutoa mizigo kwenye mageti yasiyoruhusiwa, taarifa kutofautiana, walinzi kupangwa wale wale siku, mnapaswa mjitathmini na muwajibike kutokana na nafasi zenu lakini nimuagize katibu tawala mkoa wa Tanga kuchukuwa hatua kwa mameneja hao wawili" alisema Mgumba.

 Awali akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mwenyekiti wa kamati ya uchunguzi wa tukio hilo Sebastiani Massanja amesema kuwa uchunguzi uliofanywa na wajumbe wa kutoka mamlaka mbalimbali vikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama ulibainisha kuwa hakukuwa na hitilafu yeyote ya umeme ndani ya ngala uliyosababisha kutokea kwa tukio hilo jambo ambali linaonyesha kuna hujuma iliyofanyika.

 "Kutokana na yote yaliyoelezwa na watuhumiwa wa tukio hilo kamati imebaini kuwa chanzo cha moto huo ni hujuma iliyofanywa ili kupoteza ushahidi wa mzigo ulioibiwa kwenye ghala la TRA tarehe 20/10/2022 na tarehe 21 majira ya saa mbili mpaka saa tatu usiku" alisema Massanja 

Aidha ameeleza kuwa kamati ilikutana na changamoto katika kutekeleza majukumu yake ambapo katika eneo la tukio hakukuwepo na masalia ya bidhaa zilizoungua ambayo kwa namna moja au nyingine vingeiwezesha kamati hiyo katika uchunguzi wa kitaalamu. 

"Katika utekelezaji wa majukumu yake kamati ilipata changamoto ya kukosekana kwa masalia, wakati wa kuzima moto hii ilipelekea kukosa uhalisia wa tukio ambayo yangesaidia kwenye uchunguzi wa kitaalamu" aliongeza. 

Pamoja na hayo kamati imeishauri serikali kuhusu bidhaa zilizobaki ambazo zilikamatwa kwa njia ya magendo na nyingine zilizoshindwa kulipiwa kodi, kuuzwa kwa njia ya mnada au kutolewa msaada kwa taasisi mbalimbali hapa nchini

Mwenyekiti wa kamati ya uchunguzi wa tukio la moto Sebastian Massanja akitoa taarifa kwa mkuu wa mkoa wa Tanga kuhusu ripoti ya uchunguzi wa tukio la ghala lililoungua hivi karibuni  katika mamlaka ya bandari Tanga.


.
Share To:

Post A Comment: