Kiongozi na mkuu wa msafara kutoka Shirika la Mzinga David Msabi akizungumza na waandishi wa habari katika kilele cha mashindano ya SHIMUTA mkoani Tanga. 

Na Denis Chambi, Tanga.

Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1967 kuanzishwa kwa mashindano ya SHIMUTA hapa nchini shirika la Mzinga kutoka mkoani Morogoro wamefanikiwa kuibuka kuwa washindi wa jumla kwenye mashindano hayo mwaka 2022 yaliyofanika hapa Tanga hii ni baada ya kushinda kwenye michezo mingi iliyohusisha mashirika , taasisi na makampuni zaidi ya 52 yaliyoshiriki kutoka kila kona ya Tanzania.

 Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutwaa tuzo hiyo kiongozi na mkuu wa msafara kutoka Shirika la Mzinga David Msabi amesema kuwa wameipa kipaumbele vilivyo sera ya michezo na hii ndio siri ya mafanikio yao.

"Sera ya michezo kwetu sisi kwa sababu tunaamini michezo ni sehemu ya kazi na ndio tunayoidumisha na kama taasisi ambayo ipo chini ya wizara ya ulinzi inapokea maagizo kutoka juu na yakishakuja lazima yatekelezwe na hii ndio siri ya mafanikio yetu" alisema Msabi. 

Shirika hilo ambalo lina historia ndefu ya kushiriki michuano hiyo tangu ilipoanzishwa mwaka 1977 limekuwa likifanya vizuri lakini mwaka huu wametimiza ndoto na kiu yao ya muda mrefu ya kutwaa kombe la jumla hatua ambayo wanajivunia nayo

"Tuna historia ndefu sana katika mashindano haya kwa sababu kati ya timu za zamani ambazo zinashiriki michuano hii moja wapo ni Mzinga tupo mpaka leo tangu mwaka 1967 na tuliendelea kushinda kwa michezo mbalimbali lakini kwa mara ya kwanza kwa ushindi wa jumla ni mwaka huu 2022" alisema.

 Aidha amelipongeza shirikisho la SHIMUTA lililoratibu na kusimamia michezo hiyo wakiziba mianya ya kupenyeza watumishi mamluki ambao kimsingi sio walengwa wa mashindano hayo hatua ambayo mwaka huu kila mtu alipambana kwa hali yake akijipanga kutetea adhima na malengo ya taasisi aliyotoka. 

"Kwa niaba ya Shirika la Mzinga niwapongeze sana SHIMUTA kuweza kuratibu na kusimamia michezo hii zaidi ya mashirika 52 yenye watu zaidi ya elfu mbili sio kitu kidogo wanapaswa kupongezwa na kama kuna makosa madogo madogo ni vyema wakaendelea kujirekebisha kwa mwaka huu hatukuona mamluki kwa sababu walidhibitiwa mapema"

Aliwapongeza wachezaji wao wote walioshiriki michezo kwa nana jinsi walivyoshirikiana ili kuhakikishsa kuwa hawarudi mikono mitupu   huku akikiri kuwa haikuwa rahisi kupenya katika nafasi hiyo na hatimaye kutwaa kombe la jumla hii ni kutokana na upinzani waliokutana nao kwa timu mbalimbali karibia michezo yote waliyoshiriki tangu mwanzo mwa mashindano hayo.

"Ushindi huu tulioupata ni kwa sababu ya jitihada za wachezaji  walizozionyesha tangu mwanzo wa mashindano na waliahidi kuwa wanakuja kupambana na kweli wameonyesha ushindani tunawapongeza na kuwashukuru sana" aliongeza

Mashindano hayo ysliyowahusisha watumishi kutoka mashirika ya umma , Taasisi na makampuni binafisi yalianza kurindima mkoani Tanga November 15 hadi 29, 2022  timu mbalimbali zikichuana viwanja tofauti tofauti vilivyopo jijini Tanga. 

Mzinga mwaka huu 2022 kwenye mashindano ya Shimuta iliweza kuweka tekodi katika michezo mbalimbali ambapo mpira wa miguu walikuwa mshindi wa tatu , riadha na netball wakiwa hawajaambulia kitu .

Shirika hilo pia liliweza kufunika katika michezo ya jadi ambapo kupitia michezo ya Bao , Dats waliibuka vinara kwa pande zote za wanawake na wanaume, huku wakichukuwa mshindi wa kwanza mwanamke kwenye michezo ya Karata na Polltable, na mshindi wa kwanza mwanaume kwenye kukimbia ndani ya magunia.

Mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka yakiwahusisha watumishi kutoka mashirika ya umma taasisi na makampuni binafsi hufanyika kila mwaka ambapo mwaka huu yalifanyika mkoani Tanga yakifunguliwa rasmi na makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ambaye pia ni mlezi wa SHIMUTA Dkt.Phillip Mpango  November 15 ambapo yamefungwa na mkuu wa mkoa wa Tanga Omari Mgumba November 29 ,2022.

Share To:

Post A Comment: