Ferdinand Shayo ,Manyara. 

Kampuni ya Mati Super Brands Limited imeibuka na kuwa mshindi wa pili wa Tuzo za Walipa kodi Mkoa wa Manyara zilizotolewa na Mamlaka ya Mapato nchini Tazania (TRA ) ikiwa ni njia mojawapo ya kutambua mchango wa kampuni hiyo katika kulipa kodi mbali mbali za serikali ambazo zinachangia maendeleo ya Taifa. 

Mkurugenzi wa Huduma na na Elimu kwa Mlipa Kodi (TRA) Makao Makuu Richard kayombo  ambaye ni mgeni rasmi katika halfa ya utoaji wa tuzo za walipa kodi katika Wilaya 5 za mkoa wa Manyara pamoja na Mkoa wa Manyara ameitunuku tuzo Kampuni ya Mati Super Brands Limited tuzo hiyo kwa kushika nafasi ya pili kimkoa huku  kampuni ya Manyara Sugar ikishika nafasi ya kwanza kimkoa. 

Richard Kayombo amepongeza kampuni ya Mati Super Brands Limited kwa kuwa kinara katika masuala ya ulipaji kodi na pia kushiriki katika masuala mbali mbali ya jamii na kutoa misaada mbali mbali. 

Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited David Mulokozi ameishukuru serikali kupitia TRA kwa kuwapatia tuzo ambayo inaamsha ari ya kufanya kazi kwa bidii na kulipa kodi ili kuchangia maendeleo ya Taifa. 

"Tunaishukuru sana Tra kwa tuzo hii tutaendelea kushirikiana nao vizuri pia tunaipongeza serikali kwa kuweka mazingira rafiki ya ulipaji kodi" alisema Mkurugenzi wa Mati Super Brands Limited  David Mulokozi . 

Share To:

Post A Comment: