Na Mwandishi Wetu.

 Tigo na Hisense KUPELEKA washindi 50 QATAR KUSHUHUDIA KOMBE LA DUNIA NA 30 KUJISHINDIA Kifurushi cha vifaa VYA NDANI , PROMOSHENI YA WAKISHUA TWENZETU QATAR NA Hisense. 

Oktoba  11, 2022,  Kampuni inayoongoza kwa Utoaji wa huduma za kidijitali Tigo Tanzania, kupitia Promosheni yake ya WAKISHUA TWENZETU QATAR na Hisense kwa kushirikiana na kampuni ya HISENSE wametoa tiketi 3 za kwenda Qatar kushuhudia kombe la Dunia ( kwa washindi watatu wa awamu ya kwanza) na zawadi ya Vyombo vya ndani kama vile Friji , Spika za Mziki (SubWoofer), Smart Tv , pamoja na Microwave kwa mshindi mmoja. 

Akizungumza baada ya kukabidhi zawadi hizo kwa washindi Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa Bi. Mary Ruta amesema kuwa

" Hawa washindi wa leo wamepatikana kwenye Droo ya kwanza , washindi hawa walifanya miamala kama kulipa bili , kufanya malipo ya kiserikali , kupokea pesa kutoka nchi za nje , benki , mitandao mingine , LIPA KWA SIMU , kununua muda wa maongezi  na huduma nyingine mbalimbali za Tigo Pesa ambapo baada ya kufanya ivyo waliingia kwenye droo na mwisho wa siku kuibuka washindi wa Kampeni hii Ya WAKISHUA TWENZETU QATAR NA HISENSE , Tunawasihi wateja wetu endeleeni kufanya miamala na Tigo Pesa ili kuibuka mshindi maana Tiketi na zawadi bado zipo "

Promosheni yetu ndo kama inaanza maana tutahitaji kupata washindi 50 watakaojishindia safari ya kwenda kuangalia mechi za Kombe la Dunia pamoja na Washindi 30 watakaojishindia vifaa vya Nyumbani " Alimalizia.

Naye kwa upande wake Afisa Masoko wa Kampuni ya HISENSE Bwn. Joseph Mavura amesema kuwa kampuni ya Hisense inatoa ofa ya punguzo la 20% katika maduka yao yote kwa mteja atakayenunua bidhaaa na Kulipia kwa Tigo Pesa " Alimalizia 

Naye kwa Upande wake mshindi wa Vifaa vya nyumbani ( Friji , Microwave , Smart Tv , na (Subwoofer) kutoka Hisense  Bi. Jamida Athuman Mkazi wa Dar Es Salaam ameipongeza kampuni ya Tigo na Hisense kwa kuja na promosheni hii na kuwasihi watanzania kuichangamkia fursa hii kwa kufanya miamala mbalimbali na Tigo Pesa huenda wakaibuka washindi kama ilivyotokea kwake " 

Naye mmoja ya washindi wa Safari ya kwenda QATAR Bwn. Wilson Masawe amesema kuwa " Ninayo furaha sana kuibuka mshindi wa Kwenda Qatar kutazama kombe la dunia kwa mwaka huu 2022 , hakika nimefurahi sana maaana sikutegemea na kwa mara ya kwanza maishani mwangu napata nafasi ya kwenda kuitazama hasa Timu yangu ya Brazil , nawaahukuru sana Tigo na Hisense kwa fursa hii maana sikutarajia maishani mwangu , nawasihi Watanzania kufanya miamala kwa wingi na Tigo Pesa huenda mkaibuka washindi kama ilivyotokea kwangu maana nafasi bado zipo" Alimalizia

Share To:

Adery Masta

Post A Comment: