Na,DENIS CHAMBI, TANGA.

Kampuni ya Silverland Coastal ambao ni wazalishaji wa vifaranga ya kuku wa kisasa pamoja na huduma nyingine za ufugaji wa kuku wameiomba serikali kutoa bei elekezi kwa wauzaji na wasambazaji wa vyakula vya kuku hapa nchini ambao itakuwa rafiki kwa wajasiriamali wanaojishuhulisha na ufugaji huo.

Ombi hilo limetolewa na Meneja wa kampuni hiyo ya  Silverland Coastal   Kanda ya kaskazini Deogratias Massawe wakati wa semina kwa wafungaji wa kuku  yenye lengo la kuwajengea uwezo wa namna bora ya ufugaji  kuibua changamoto na matatizo yanayowakumba katika tathnia hiyo na hatimaye kuyapatia ufumbuzi pamoja na kuwaunganisha kuweza  kushirikiana katika tathnia hiyo.

"Sisi kama Silverland Coastal kufanya semina na wafugaji ambao ni wateja wetu wakubwa  ni sehemu ya kutoa elimu kwao kwa sababu kila siku dunia inabadilika na hata masoko pia yanabadilika, tunarudi kwa wafugaji  kuwaelekeza na kuwaonyesha sehemu ambayo wamekosea  katika tathnia lakini kikubwa zaidi ni kuongeza ushirikiano kwa sababu huwezi kufanya biashara bila ya kuwa pamoja" alisema Massawe .

Meneja huyo amesema kupanda kwa  bei ya vyakula ikiwemo mahindi kumechangia kwa kiasi kikubwa kupanda wa vyakula na madawa ya kuku hali ambayo imekuwa ikiwapa wakati mgumu wafanyabiashara wa Kuku ikiwa ni pamoja na kukosa mtaji wa kutosha kuwasaidia kuwekeza katika tathnia hiyo.

"Bei ya  chakula cha kuku inapanda kila siku kwa sababu ya kupanda kwa malighafi zinazotumika kuzalishia vyakula hivyo leo hii bei ya mahindi kote nchini inazidi kupanda  sasa ukiangalia  kwa kiasi kikubwa chakula cha kuku ni mahindi kwahiyo kadiri bei inavyozidi kupanda kadharika pia na bei ya chakula cha kuku inazidi kupanda" alisema .

Hata hivyo katika kutafuta suluhu ya kupambana na kupanda kwa bei ya vyakula meneja huyo amewashauri wafugaji pamoja na wafanyabiashara wa kuku kuunda umoja wao kushirikiana katika upande wa masoko hali ambayo itawasaidia na kuwawezesha kuondokana na changamoto zinazowakabili

"Lakini Wafugaji wangekuwa na umoja wangeweza kukabiriana na changamoto ya bei sokoni , wangekuwa na ushirikiano  huu ungewasaidia kutoa bei elekezi , serikali hapo pia ingalie namna ya kuja na sera mpya  ya kutoa bei elekezi kama inawezekana lakini nawashauri wafugaji wakati tunasubiri serikali wao wenyewe waje na umoja wao wakiwa na sera moja ya bei elekezi tunaweza kufikia sehemu nzuri" alisema Masawe.

Kwa upande wao wafugaji akiwemo Alfa Mosha wameeleza namna semina inayotolewa na kampuni hiyo yanavyowasaidia ikiwemo kuimarisha  ulinzi, kutoa chanjo na kuandaa mazingira rafiki kwaajili ya ufugaji huo ambao unaweza  kuwasaidia kuondokana na athari mbalimbali ikiwemo vifo huku wakieleza changamoto ya bei ya kuku iliyopo sokono kwa sasa ambayo haiwalipi

"Tunashukuru mafunzo haya  ni mazuri na yenye faida kubwa sana kwetu sisi wafugaji  ikiwemo ufugaji bora kuwekeza ulinzi kwenye banda kukabiliana na magonjwa ya kuku, kazi ya kufunga sio ngumu lakini changamoto kubwa ambayo tunakutana nayo hapa ni bei ya kuku haipandi  na vyakula navyo vimekuwa vikipanda  bei ya kuku haiendani na bei ya vyakula iliyopo kwa Sasa "alisema Mosha.

Sister Consolata Mgumba ameiomba kampuni ya Silverland kuendelea kutoa elimu kwa wafungaji kuwajengea uwezo wa namna ya kuweza kujikita katika sekta hiyo ambayo sasa inazidi kuwa chanzo cha ajira kwa wajasiriamali hapa nchini.

"Kila  kuku unayetaka kumfunga lazima ufuate Sheria na taratibu za ufugaji ikiwemo kupangilia aina ya vyakula kwa wakati husika ukikosea unaweza ukamdumaza kuku  elimu kwa wafugaji ni muhimu sana , bei inaweza ikakusumbua kwa sababu ya kukosa elimu, kabla ya kuanza ufugaji ni lazima ujue unataka ufuge kuku wa aina gani na unatarajia upate nini kwa wakati gani  " alisema  Sister Consolata.



Share To:

JUSLINE

Post A Comment: