Umoja wa Ulaya (EU) kwa kushirikiana na Taasisi ya Agrithamani Foundation imeitaka jamii kuwa na utamaduni wa kula vyakula vya asili ili kuwa  na lishe bora itakayowaepusha na tatizo la udumavu na kuwataka wazazi kuwafundisha watoto kuoika vyakula vya asiki ili kuondokana na utamaduni wa kupenda vyakula vya kileo .

Hayo yamezungumzwa na mwakilishi wa Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) Anna constine katika uzinduzi wa tamasha la 'Msosi Asilia' lililolenga kuhamasisha ulaji wa vyakula vya asili, tamasha hilo lililofangika Temeke jijini Dar es salam.

"Tutashirikiana na Tanzania pamoja na Shirika la kilimo na chakula (FAO) ili kuendelea kuhamasisha ulaji wa vyakula vya asili kwa sababu vinaleta nguvu zaidi ukilinganisha na vyakula vingine vya kisasa" - Anna.

Naye Magreth Natai ambaye ni  afisa kilimo Mkuu kutoka Wizara ya kilimo amesema Serikali inaendelea kushirikiana na shirika la kilimo na chakula ( FAO) kuhakikisha Watanzania wanaachana na ulaji wa vyakula visivyofaa na kuepuka magonjwa ya kuambukiza.

" Wizara ya kilimoitaendelea kuhamasisha ulaji wa vyakula vya asili kwa kila Mkoa kwa sababu vinavirutubishi vya kutosha tutakuwa na mbinu mbalimbali" - amesema Magreth Natai

Kwa upande wake mwakilishi mkazi Msaidizi kutoka FAO Charles Tulah amesema kampeni ya ulaji vyakula vya asili inalenga kukabiliqba na tatizo la lishe nchini na kutoa rai kwa watafiti kuendelea kutafiti ulaji wa vyakula vya asili kukabiliqba na tatizo la utapiamlo katika nchi za Afrika.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Taasisi ya Agrithamani foundation ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu anayewakilisha mashirika yasiyo ya kiserikali (NGos) Neema Lugangira amesema vyakula vya asili ndiyo vina viini lishe vya kutosha na vinamsaidia binadamu kupata kinga.

Mbunge Lugangira amesema tamasha hilo ni endelevu kila mwaka na litakuwa linafanyika katika Mkoa wa  Mbeya na visiwani Zanzibar.

"Hii ni sehemu ya mradi wa Agriconnect, ambao uko chini ya Wizara ya kilimo FAO  na EU na lengo ni kuhamasisha ulaji wa vyakula vya asili" - Mbunge Neema Lugangira.






Share To:

Post A Comment: