Mkurugenzi wa Taasisi ya Agri-thamani Foundation ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha Mashirika yasiyo ya Kiserikali(NGos) Neema Lugangira akimuoneshaa baadhi ya vyakula vya asili Mwakilishi wa Balozi wa EU, Bi.Anna Constine wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 'Msosi Asilia' linalolenga kuhamasisha ulaji vyakula vya asili.


WAZAZI na walezi wameshauriwa kuwa na mazoea ya kuwaruhusu watoto wao kushiriki katika matamasha ya chakula cha asili ili waweze kujifunza umuhimu wa vyakula hivyo na kuondokana na janga la udumavu.

Akizungumza katika uzinduzi wa Tamasha la 'Msosi Asilia' linalolenga kuhamasisha ulaji vyakula vya asili iliyofanyika leo Oktoba 23,2022 Temeke Jijini Dar es Salaam Mwakilishi wa Balozi wa EU, Bi.Anna Constine,amesema kuna umuhimu mkubwa jamii ikafahamu umuhimu wa kula vyakula vya asilia iki kuondokana na maradhi nyemelezi.

"Tunashirikiana na Tanzania na FAO ili kuendelea kuhamasisha ulaji wa vyakula vya asili kwasabu vinaleta nguvu zaidi ukilinganisha na vyakula vingine vya kisasa,"Amesema Bi.Anna

Nae Afisa Kilimo Mkúu kutoka Wizara ya Kilimo,Bi.Magreth Natai amesema,serikali inaendelea kushirikiana na Shirika la Kilimo na Chakula(FAO) kuhakikisha Watanzania wanaachana na ulaji wa vyakula visivyofaa na kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

"Wizara ya Kilimo tunaendelea kuhamsisha ulaji wa vyakula vya asili kila Mkoa kwasababu vinavirutubishi vyakutosha,tatakuwa na mbinu mbalimbali

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi Msaidizi wa FAO Charles Tulahi,amesema kampeni ya ulaji vyakula vya asili inalenga kukabiliana na tatizo la lishe nchini mbalo limekuwa changamoto kwa baadhi ya jamii nchini.

Amesema FAO imeongeza kasi kuhamasisha ulaji vyakula vya asili kukabiliana na tatizo la utapiamlo katika nchi za Afrika.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Agri-thamani Foundation ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha Mashirika yasiyo ya Kiserikali(NGos) Neema Lugangira, amesema vyakula vya asili ndio vina viini lishe vya kutosha na vinamsaidia mtu kupata kinga.

Neema alisema tamasha hilo litakuwa endelevu Kila mwaka na litakuwa linafanyoka katika mkoa wa Mbeya na visiwani Zanzibar.

"Huu ni sehemu ya mradi wa Agriconnect ambao uko chini ya Wizara ya Kilimo FAO na EU,na lengo ni kuhamasisha ulaji wa vyakula vya asili ndio tumeanza na tutafanya Mbeya na Zanzibar,"Amesema.

Hata hivyo kwa upande wake Mwenyekiti wa Mama Lishe na baba Lishe Wilaya ya Temeke Bi.Maria Mtesa amewataka wadau mbalimbali kujitokeza na kuwasaidia ili waweze kuwa na moyowa kuuendelea na kazi ambayo wamekuwa wakiifanya ya Mama Lishe na Baba Lishe katika Wilaya hiyo.

Baadhi ya vyakula vya asilia katika uzinduzi wa Tamasha la 'Msosi Asilia' linalolenga kuhamasisha ulaji vyakula vya asili. Mwakilishi wa Balozi wa EU, Bi.Anna Constine, akipata picha ya pamoja na Mama Lishe na Baba Lishe katika uzinduzi wa Tamasha la 'Msosi Asilia' linalolenga kuhamasisha ulaji vyakula vya asili.

Mwakilishi wa Balozi wa EU, Bi.Anna Constine akipatiwa baadhi ya vyakula vya asili aweze kula na kuona radha yake katika uzinduzi wa Tamasha la 'Msosi Asilia' linalolenga kuhamasisha ulaji vyakula vya asili.Mwakilishi wa Balozi wa EU, Bi.Anna Constine akipatiwa baadhi ya vyakula vya asili aweze kula na kuona radha yake katika uzinduzi wa Tamasha la 'Msosi Asilia' linalolenga kuhamasisha ulaji vyakula vya asili.

Mwakilishi wa Balozi wa EU, Bi.Anna Constine akizungumza katika uzinduzi wa Tamasha la 'Msosi Asilia' linalolenga kuhamasisha ulaji vyakula vya asili .m Mkurugenzi wa Taasisi ya Agri-thamani Foundation ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha Mashirika yasiyo ya Kiserikali(NGos) Neema Lugangira akizungumza katika uzinduzi wa Tamasha la 'Msosi Asilia' linalolenga kuhamasisha ulaji vyakula vya asili.Mwakilishi Mkazi Msaidizi wa FAO Charles Tulahi akizungumza katika uzinduzi wa Tamasha la 'Msosi Asilia' linalolenga kuhamasisha ulaji vyakula vya asili . Mwenyekiti wa Mama Lishe na baba Lishe Wilaya ya Temeke Bi.Maria Mtesa akizungumza katika uzinduzi wa Tamasha la 'Msosi Asilia' linalolenga kuhamasisha ulaji vyakula vya asili.

Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: