Afisa Elimu Watu Wazima wa Wilaya ya Singida ambaye anashughulikia Afya,  Anthony Kibuga (wa tatu kushoto) ambaye alikuwa mgeni rasmi akipeana mikono na Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Community Initiatives Promotion (CIP) la mkoani Singida,  Parinemas Mashanjara katika hafla ya kukabidhiwa vyoo vilivyojengwa na shirika hilo iliyofanyika hivi karibuni katika shule ya Msingi Mwasauya iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Singida. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Afesso Ogenga, Mratibu wa Miradi wa Shirika hilo, Violet Shaku na Mwenyekiti wa Kijiji cha Masauya, Justine Kidima.

Ukaguzi wa vyoo hivyo ukifanyika kabla ya kukabidhiwa.

Afisa Elimu Watu Wazima wa Wilaya ya Singida ambaye anashughulikia Afya,  Anthony Kibuga, akizungumza katika hafla hiyo baada ya kukabidhiwa vyoo hivyo.

Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Community Initiatives Promotion (CIP) la mkoani Singida,  Parinemas Mashanjara akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la CIP, Afesso Ogenga akizungumza katika hafla hiyo.
Mratibu wa Miradi wa shirika hilo, Violet Shaku akizungumza wakati akitoa taarifa ya ujenzi wa vyoo hivyo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwasauya, Justine Kidima akizungumza.
Muonekano wa vyoo hivyo vilivyojengwa Shule ya Msingi Sokoine.

Afisa Elimu Watu Wazima wa Wilaya ya Singida ambaye anashughulikia Afya,  Anthony Kibuga, akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Sokoine wakati wa hafla hiyo.

Mratibu wa Miradi wa shirika hilo, Violet Shaku akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Sokoine wakati wa hafla hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la CIP, Afesso Ogenga akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Sokoine wakati wa hafla hiyo..

Wanafunzi wa Shule ya Msingi, Sokoine wakionesha furaha yao wakati wa hafla ya kukabidhiwa vyoo hivyo.
Picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Sokoine.
Muonekano wa vyoo hivyo vilivyojengwa Shule ya Msingi Mwasauya.
Muonekano wa vyoo hivyo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi, Mwasauya wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa vyoo hivyo.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea Shule ya Msingi Mwasauya.
Hafla ikiendelea.
Taswira ya hafla hiyo Shule ya Msingi Mwasauya.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Mwasauya, Ally Senge akizungumza.
Wananchi wakikagua vyoo hivyo vilivyojengwa Shule ya Msingi Mwasauya.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo akiongoza ukaguzi wa vyoo hivyo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwasauya wakitoa burudani kwenye hafla hiyo.
Mzee Said Abdallah wa Kijiji hicho akichangia jambo kwenye hafla hiyo.
Mratibu wa Miradi wa Shirika la CIP, Violet Shaku akimkabidhi taarifa ya ujenzi wa vyoo hivyo mgeni rasmi. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika hilo, Parinemas Mashanjara.
Diwani wa Kata hiyo, Salum Juma akizungumza kwenye hafla hiyo.
Afisa Elimu Kata ya Mwasauya, Michael Zacharia akichangia jambo.

Walimu wa shule hizo wakiwa kwenye hafla hiyo. Kutoka kulia ni Mwalimu, Mkese Isango, Mwalimu Onjai Kasali na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi, Sokoine, Rosemary Itoba.
Baiskeli zilizotolewa na shirika hilo kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mwasauya.
Mwalimu Mkese Isango akitoa taarifa ya shule ya Msingi Mwasauya mbele ya mgeni rasmi.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mwasauya wakiwa na baiskeli baada ya kukabidhiwa.
Mkurugenzi wa Shirika la CIP, Afesso Ogenga akipokea zawadi kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi, Mwasauya.

 

Na Dotto Mwaibale, Singida

 

SERIKALI ya Austria kupitia Shirika la Sister Cities Salzburg –Singida (SCSS) lililoko Salzburg Austria kwa kushirikiana na Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Community Initiatives Promotion (CIP) la mkoani Singida limeendelea kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuinua sekta za elimu na afya nchini kupitia miradi mbalimbali inayofadhiliwa ambapo limejenga vyoo viwili vyenye matundu 22 kwa thamani ya Sh.25 Milioni katika Shule za Msingi ya Sokoine na Mwasauya zilizopo Halmashauri ya Wilaya Singida Vijijini.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la CIP , Afesso Ogenga akikabidhi vyoo hivyo alisema Ushirikiano  wa maendeleo wa mashirika hayo ulioanza tangu miaka 1980 ndio unaoendelea kutekeleza miradi mingi ya kuchangia maendeleo kwa kiasi kikubwa ndani ya mkoa wa Singida.

Alisema makabidhiano  ya vyoo hiyo yameanzisha mchakato wa kihistoria ambayo italeta manufaa makubwa katika jamii ya kizazi cha sasa na kijacho kutokana na mradi huo ambao ni muhimu sana katika sekta ya elimu.

Ogenga alisema ili mwanafunzi aende shule ni lazima mazingira ya shule husika yawe bora na rafiki na moja ya vitu muhimu ni kuwa na mahali pa kujisitiri na kama hakuna huduma hiyo wanafunzi wanalazimika kwenda vichakani au mbali zaidi kuifuata lakini inapokuwa karibu inawarahisishia kuhudhuria masomo na kuwapunguzia msongo wa mawazo wa kufikiria mahali pa kwenda kujisitiri.

“Vyoo hivi ambavyo tunavikabidhi leo hii vimezingatia mahitaji ya watoto maalum hasa wasichana, tunajua kwamba takwimu zinaonesha kuwa baadhi ya wasichana waliopevuka hawaji shule kwa sababu ya kukosa sehemu ya kujihifadhi laikini katika vyoo hivi tumetenga eneo hilo jambo ambalo litawasaidia kutositisha masomo” alisema Ogenga.

Alitaja jambo lingine kuwa vyoo hivyo vimejengwa kwa mfumo wa kisasa vina maji ya kutosha ya kuflashi na sio vya shimo na kuwa ni bora zaidi kwa matumizi kwani vinapunguza maambukizi ya magonjwa ya matumbo na UTI ukililinganisha na vile vya shimo na hata kuvifanyia usafi inakuwa rahisi.

Alisema vyoo hivyo kwa kuvikadiria vitaweza kutumika hadi miaka 30 ijayo ndio maana alisema makabidhiano hayo ynanakwenda kuweka historia hiyo ambayo itaanzia kwa wanafunzi wanaoshuhudia tukio hilo na wale watakaokuja baadae na kusoma katika mazingira rafiki.

Mratibu wa Miradi wa Shirika hilo, Violet Shaku awali ya yote alitumia nafasi hiyo  kuwashukuru wakazi wote wa Kata ya Mwasauya, kwa muitikio wao katika kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo, ambao kwa kiasi kikubwa umechangia katika ukuaji, utekelezaji na mafanikio ya miradi ya maendeleo inayofanywa na Shirika la CIP.

Shaku alisema , shirika la CIP lilianzishwa mnamo mwaka 2002 lengo kuu likiwa ni  utoaji wa huduma kwa jamii zenye kiwango na endelevu kiuchumi na kijamii kwa watu waliombali na huduma katika mkoa wa Singida, kwa kuwaongezea uelewa, kuwajengea uwezo na utafutaji wa mali.

 Alisema katika kutekeleza miradi hiyo shirika hilo limejikita zaidi katika maeneo makuu matatu ambayo ni afya ambapo kwenye afya tumekuwa tukitekeleza miradi ya kutoa mafunzo, kugawa vifaa tiba, kufadhili wataalamu wetu kwa ngazi ya diploma na maswala ya boresha lishe kupitia kwa wahudumu wetu wa afya ngazi ya jamii, tumejikita pia kwenye maswala ya kuwainua kina mama kiuchumi kupitia miradi ya ufugaji kuku wa biashara na mwisho kabisa ni elimu.

Alisema katika kuunga mkono jitihada zinazo fanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuleta maendeleo kwa wananchi, Shirika la CIP  linaendelea kujivunia kuwa miongoni mwa masharika yanayotia mkazo kwenye swala la elimu shirikishi kwa manufaa ya kizazi cha sasa na baadae.

Akizungumzia mradi huo uliotekelezwa katika shule hizo mbili alisema shirika limeweza kujenga vyoo matundu 20 na vyumba vya faragha kwa wasichana viwili na kuweka mifumo wa maji iliyogharimu kiasi cha sh 25,000,600. Vyoo hivi vimejengwa kwa kushirikiana na uongozi na wananch katika kijiji cha Mwasauya. Ni vyoo vinavyozingatia mahitaji ya watoto wa kike kwasababu vinatumia maji na hivyo vinasaidia kupunguza magonjwa kama vile UTI na maradhi ya tumbo.

Shaku alisema  kwa miaka minne mfululizo shirika limekuwa likiwajengea uwezo walimu 32 kutoka kata za Mwasauya na Ikhanoda  katika masomo ya hisabati na kingereza, sambamba na hilo shirika limekuwa likisambaza vitabu vya kujifunzia kwa wanafunzi wa kata hizi mbili, katika kuendelea kuwajengea uwezo walimu shirika limekuwa likiwafadhili walimu kujiendeleza kimasomo kwa ngazi ya shahada na stashada katika vyuo mbalimbali nchini ambapo mpaka sasa limefadhili walimu wapatao wanne.

Aidha Shaku alisema shirika hilo limetoa baiskeli 15 kwa ajili ya kuwasiadia wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mwasauya wanaoishi mbali na shule hiyo ziweze kuwasaidia wakati wa kwenda shuleni na kurudi nyumbani ambapo awamu ya kwanza zilikuwa tano na awamu ya pili 10.

Shaku alitaja baadhi ya changamoto mbalimbali ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo  wakati wa kutekeleza miradi hiyo kuwa ni ongezeko la uhitaji wa huduma kuliko kile shirika linaweza kuhudumia,kukipokea fedha kidogo kutoka kwa wahisani ambayo haiwezi kukidhi mahitaji yote ya wanchi wetu.

“Leo hii tunapokabidhi vyoo hivi, ni matarajio yetu kuwa ofisi yako, kwa kushirikiana na viongozi wa chama na serikali pamoja na wananchi mtaunganisha nguvu katika kutunza majengo haya na kufanyia ukarabati pale itakapohitajika” alisema Shaku.

Akizungumza wakati akikabidhiwa vyoo hivyo Afisa Elimu Watu Wazima wa Wilaya ya Singida ambaye anashughulikia Afya,  Anthony Kibuga ambaye alikuwa mgeni rasmi alilishukuru shirika hilo kwa msaada mkubwa wanaoutoa katika wilaya hiyo kwa zaidi ya maiaka 20 katika nyanja za elimu na afya.

“Binafsi kwa niaba ya Serikali tunawashukuru sana kwa kazi kubwa mnayoifanya ya kuisaidia serikali katika maeneo yote mnayotusaidia” alisema Kibuga.

Diwani wa Kata ya Mwasauya  Salum Juma alilishukuru shirika hilo kwa misaada hiyo inayoitoa katika maeneo hayo hasa katika kata hiyo ambapo alitumia nafasi hiyo kuwaomba wanufaika wa miradi hiyo kuitunza na kuilinda huku akisisitiza kwa kusema msemo wa kiswahili usemao kulea mimba sio kazi bali kulea mtoto akimaanisha kuwa kupata mradi ni kazi moja na kuitunza ni kazi nyingine ambayo ndiyo ya  muhimu sana.


Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: