Na Christina Thomas, Morogogo


BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro limetoa mwezi mmoja kwa wamiliki wa magari yote ya abiria yanayofanya shuguli za usafirishaji ndani na nje ya Manispaa maarufu kama daladala kuhakikisha wanaingia kwenye kituo kipya cha daladala Mafiga ili kuiingizia mapato Halmashauri hiyo. 


Akizungumza Kwa niaba ya madiwani  wa manispaa hiyo katika kikao cha kawaida cha Baraza la madiwani  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Pascal Kihanga  amesema agizo  hilo kwa daladala na magari yote ya abiria yanayofanya shuguli za usafirishaji ndani ya Manispaa  linapaswa kutekelezewa vinginevyo sheria itashika nafasi yake.


Amesema kuingiza magari katika kituo kipya cha mafiga kutasaidia  kuongeza mapato ya halmashauri hiyo huku abiria WA kutoka sehemu mbalimbali wakipata huduma ya usafiri ya uhakika tofauti na sasa ambako magari yamekuwa yakizunguuka katikati ya mji pekee.


Aidha  amesema  lengo la kujengwa kwa kituo hiko cha daladala cha mafiga  ni kuwarahisishia wananchi huduma ya usafiri ili waweze  kusafiri kwa urahisi.


Hivyo amewaomba viongozi kusimamia agizo hilo na kuhakikisha linatekelezeka ili Halmashauri iweze kukusanya mapato kutoka kwenye chanzo hicho cha mapato kama kwenye vyanzo vingine.


Baadhi ya magari ikiwemo daladala zinazofanya safari zake kutoka Kihonda yamekuwa hayaingii kwenye kituo hicho na kufanya halmashauri kutokusanya mapato ya kutosha kwenye kituo hicho.

Share To:

Post A Comment: