Mkuu wa Wilaya ya Ikungi  Jerry Muro (wa nne kulia) akiongoza kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Ikungi kilichoketi na wananchi kwa ajili ya kumaliza mgogoro baina ya baadhi ya wafugaji kutoka Mkundi mkoani Shinyanga, Iramba na Igunga dhidi ya wananchi wa Kata ya Mwaru Kijiji cha Mdughuyu kilichoketi jana wilayani humo mkoani Singida. Aliyeketi kushoto kwa meza ni Diwani wa Kata ya Mwaru, Iddi Makangale.

DC Jerry Muro akisisitiza jambo kwenye kikao hicho.

Wananchi na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo wakimsikiliza mkuu wa wilaya hiyo, Jery Muro.



Na Mwandishi Wetu, Ikungi


KAMATIi ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Ikungi  imemaliza mgogoro baina ya baadhi ya wafugaji kutoka Mkundi mkoani Shinyanga, Iramba na Igunga dhidi ya wananchi wa Kata ya Mwaru Kijiji cha Mdughuyu na kuifanya wilaya hiyo kuendelea kuwa salama kwa wafugaji na wakulima.

Akizungumza katika kikao kilicho keti jana Mei 23,2022 na wananchi wa maeneo hayo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi  Jerry Muro  amewataka wafugaji wahamiaji kutoingiza mifugo katika mashamba ya wananchi na badala yake kuelekeza mifugo yao katika ushoroba wa bonde la Wembere ambalo baadhi ya maeneo yametengwa kwa ajili ya ufugaji.

DC Muro alisema tayari Mheshimwa Rais. Samia Suluhu Hassan alishatoa maelekezo maalum ya namna ya kutatua migogoro ya wafugaji na wakulima pamoja na wananchi na kusisitiza maelekezo ya Rais Samia yanapaswa kufuatwa na kuheshimiwa ili kuleta amani na usalama wa wafugaji pamoja na wakulima.

Awali wananchi wa Kitongoji cha Shololi walizua taharuki kufuatia uwepo wa mifugo mingi kutoka maeneo ya Shinyanga, Iramba na igunga ambayo ilitishia uhai wa mashamba na maeneo yao ya asili ya kuchungia jambo lililosababisha kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Ikungi kuweka kambi kutatua changamoto hiyo.

Katika kikao hicho Diwani wa Kata ya Mwaru Iddi Makangale pamoja na kushukuru hatua ya haraka iliyochukuliwa na uongozi wa Wilaya ya Ikungi kufika kwenye eneo la changamoto haraka na amehaidi kusimamia maelekezo ya Mkuu wa Wilaya Jerry  Muro katika kuhakikisha wananchi wanapata fursa ya kuchunga na kulima pasipo kutengeneza migogoro.

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: