Na,Jusline Marco;ArushaKatibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Mary Makondo  amewataka mawakili wa serikali nchini kuwa waadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao pamoja na kufanya kazi kwa bidii, umakini na uzalendo kutokana na mchango wao kuwa mkubwa katika kuchangia uchumi wa nchi.

Ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya mawakili walio katika ofisi za serikali yaliyofanyika Jiji Arusha ambapo amesema Ofisi hiyo imechangia  katika uokoaji wa mapato ya serikali kwa kuisaidia kutolipa fidia  ya zaidi ya trilion 10 ambazo zingelipwa na mashauri yaliyo ndani na nje ya nchi ambayo kutokana na migogoro mbalimbali inayoibuka katika utekelezaji wa mikataba serikali inashtakiwa na kudaiwa fidia. 

Aidha amesema suala ya uendeshaji wa kesi ni suala mtambuka kwasababu ya kuhusisha wadau kadhaa katika mashauri amnapo ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali imefungua mfumo mahususi wa kuwatambua mawakili wa serikali na wanasheria ili kuwawezesha kufanya kazi kwa weledi,bidii na uzalendo katika kuijenga nchi.

"Fedha hizo zikiokolewa zinarudishwa katika mfumo mkuu wa serikali na kutumika katika maendeleo ya nchi na huduma zake kwa ujumla kama elimu,ujenzi wa miundombinu, sekta ya afya na kuchangia katika ujenzi wa nchi yetu,"alisema  Katibu Mkuu huyo.


Vilevile amesema serikali inaendelea kuboresha masuala yote yanayohusisha upelelezi na uendeshaji wa mashtaka kwa kushirikiana na muhimili wa mahakama ambao umefanyiwa manoresho na serikali.

Ameongeza kuwa mafunzo hayo ya uendeshaji wa mashauri pamoja na upatanishi usuluhishi kwa mawakili wa serikali yametokana na kutambulika kwa umuhimu wa mawakili hao katika kuchangia uandaaji wa nyaraka katika sekta na taasisi zote za serkali ambapo imelenga kuwajengea uwezo mawakili hao 

Kwa upande wake  Wakili wa Serikali mwandamizi Jenipher Amosi Kaaya amssema zaidi ya triilioni 11 zimetumika katika uendeshaji wa mashauri ya madai ya kuiwakilisha serikali.

Ameongeza kuwa mafunzo hayo yatawajengea uwezo,weledi na kijiamini katika kushindana na mawakili wenzao mahakamani endapo wakishtakiwa  watakuwa na nguvu kubwa kuliko ya awali katika kuwasilisha hoja zao za kisheria.

Hata hivyo amesema mafunzo hayo yamelenga uendeshwaji wa mashauri pamoja na upatanishi usuluhishi lengo ni kutambua umuhimu wa mawakili wa serikali katika kuchangia uandaaji wa nyaraka ipasavyo katika taasisi za serikali,usimamizi na uendeshwaji wa mashauri yanayofunguliwa dhidi ya serikali au serikali yenyewe yakisimamiwa na wakili mkuu wa serikali.

Naye Wakili Mkuu wa Serikali Mhe.Gabriel Malata amesema tangu kuanzishwa kwa ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali mwaka 2018 wamefanikiwa kuokoa zaidi ya trillion 10 za serikali ambazo zingelipwa kwa watu wasio stahili kama serikali ingeshindwa mashauri.


"Tumeendesha mashauri ya madai na usuluhishi kwa weledi kwa niaba ya serikali ikiwa ni pamoja na kushiriki katika ukuzaji wa sheria nchini kupitia uendeshaji wa mashauri mahakamani ikiwemo mashauri ya madai, Katiba, haki za binadamu na usuluhishi,”Alisema.

Sambamba na hayo amesema kuwa pamoja na changamoto ya uhaba wa mawakili wa serikali wapatao 312,wamekuwa wakipata faida mbali mbali ikiwemo utoaji wa elimu kwa mawakili na kutatua migogoro kwa wakati.Share To:

JUSLINE

Post A Comment: