Na John Walter-Babati

Mbunge wa Jimbo la Babati vijijini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Bunge Daniel Sillo, leo mei 28, 2022 amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa Jimboni kwake kwa ajili ya kuwarahisishia huduma Wananchi.

Akiwa Nkaiti alikagua barabara ya Minjingu-Kakoi yenye urefu wa kilomita 12 inayojengwa kwa kiwango cha Changarawe huku Magugu akikagua barabara ya njia panda ya kuelekea Gichameda inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami  pamoja na ujenzi daraja la Ngarenaro.
Mheshimiwa Sillo akiwa kata ya Magugu amezungumza na Wananchi ambapo amewataka kuwa na subira wakati serikali ikiendelea kukamilisha miradi hiyo.

Aidha Mheshimiwa Sillo amefika kijiji cha Bacho kushuhudia ujenzi wa Daraja kijijini hapo lililoanza kujengwa chini ya usimamizi wa Wakala wa Barabara za mjini na vijijini (TARURA) wilaya ya Babati ambapo hadi kukamilika linatajwa kuwa litagharimu zaidi ya shilingi Milioni 189.

Aidha akiwa na TARURA wilaya ya Babati amefika kuona ujenzi wa bara bara ya Haysam-Bacho kwa kiwango cha Moram inayotarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi Milioni 201.

Kwa Mujibu wa diwani wa kata ya Ayalagaya Sabini John,Daraja hilo ni Muhimu kwa kuwa litawasaidia wananchi kuweza kupata huduma za kijamii.
Share To:

Post A Comment: