Na John Walter-Manyara

Mkuu wa mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere  ameutaka uongozi wa Halmashauri ya mji wa Babati kuhakikisha wanasimamia ipasavyo zoezi la anuani za makazi kwa wananchi likamilike kikamilifu kama ilivyoelekezwa.

Nyerere alisema hayo mjini Babati leo Mei 28,2022 wakati lipofanya ziara maalum ya ukaguzi wa zoezi hilo katika mitaa na vijiji mbalimbali vya wilaya hiyo.

Nyerere alisema kuwa katika utekelezaji wa zoezi hilo hakuna mbadala isipokuwa ni kutekeleza kwa nguvu zote kwani Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria kuwasadaidia wananchi katika kuboresha mawasiliano katika sehemu mbalimbali ikiwemo makazi yao, sehemu zao za biashara na maeneo mengine ya huduma za kijamii.

Aidha alisema Lengo la utekelezaji wa zoezi la Anwani za Makazi ni kurahisisha mawasiliano na kuifanya jamii kuwa ya kisasa zaidi bila kusahau kuimarisha ulinzi katika makazi yao. 

Nyerere aliwataka viongozi Katika wilaya zote za mkoa wa Manyara kusimamia na kuhamasisha jambo likamilike kikamilifu.

Naye kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Babati Anna Fissoo alisema kuwa katika Halmashauri ya mji wa Babati  yenye Kata nane zoezi hilo linaendelea kutekelezwa.

Kwa Upande wake mratibu wa zoezi la Anuani za Makazi mkoa wa Manyara Alphonce Malibiche amesema zoezi hilo lipo katika hatua za mwisho na kwamba  tayari nyumba nyingi zimepewa namba na kinachoendelea kwa sasa ni uwekaji wa Vibao kwenye nyumba ambazo bado.


Share To:

Post A Comment: