Na John Walter-Manyara

Mkuu wa mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere amewataka wafanyabiashara na wananchi wa mkoa huo kuwa na tabia ya kutoa na kudai risiti pindi wanapouza au kununua bidhaa.

Amesema uzalendo wa nchi ni pamoja na kuwa na moyo wa  kulipa kodi  bila kushurututishwa.

 Makongoro akizungumza wakati akipokea jopo la watoa elimu kwa mlipa kodi kutoka TRA makao makuu,  amewaambia wananchi mkoani humo kuwa kitendo cha kudai risiti wakati wanapofanya manunuzi mbalimbali kunaiwezesha serikali kupata mapato yake kikamilifu.

Alisema kodi inayokusanywa kupitia kwa wafanyabiashara na wadau wengine ndio inayoiwezesha serikali kufanya shughuli zake za maendeleo kwa faida ya wananchi wenyewe.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange amesema watashirikiana na Mamlaka ya Mapato TRA kusimamia ukusanyaji wa mapato kwa faida ya wilaya na Taifa.

 Naye afisa mahusiano mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Mackdonald Mwakasindile amesema lengo la kampeni ya Door to Door ni kusisitiza umuhimu wa matumizi sahihi ya risiti na kuukumbusha Umma juu ya kutambua  bidhaa feki.

''Tumekuja Manyara tukiwa na jukumu la kuwatembelea walipakodi katika mpango au program inaitwa Door to Door yaani mlango kwa mlango, program hii inahusu kuwatembelea walipakodi katika maeneo yao ya biashara tukiwapa elimu kuhusiana na kodi,kusikiliza kero na matatizo yanayowakabili kuhusiana na kodi na kutafutia ufumbuzi'' alisema

Hatahivyo Mwakasindile amesisitiza wananchi pamoja na wafanyabiashara kutambuwa umuhimu wa kutoa na kudai risiti pindi mauzo yanapofanyika.

''Ikumekuwa hulka kwamba kunawatu wakinunua vifaa hawachukui risiti pia imekuwa hulka kwa watu wanao uza kutokutoa risiti, vilevile tunahamasisha umma kuweza kutambuwa bidhaa ambazo ni feki kwamba waweze kupakuwa app yao ya kutambuwa bidhaa ambazo siyosahihi wapakuwe kutoka kwenye simu zao za adroid ili waweze kuscan product na kuweza kutambuwa kuwa zipi ni feki''alisema

Mmoja wa wafanyabiashara mjini Babati Izack Polepole amesema kampeni ya mlango kwa mlango itawasaidia wengi kupata majawabu ya mambo mbalimbali yanayowatatiza ikiwemo utapeli unaofanywa na baadhi ya watu wanaojitambulisha kwa wafanyabiashara kuwa wao wanatoka ofisi za TRA.

Share To:

Post A Comment: