Bata Mzinga ni biashara nzuri sana ambayo watu wengi hatuitilii maanani sana.  Soko la Bata Mzinga ni kubwa sana katika Supermarkets.

Wengi watahoji nitafugia wapi! Hautakuwa una shida ya hela ndugu yangu, lakini sikulaumu sana kwa kuwa mfumo wa sisi hasa watanzania ni kuajiriwa, na ajira zetu hizi za kupata mwisho wa mwezi kiasi kidogo cha hela na kuridhika, huwa kinatudanganya sana.

Wengi wetu hujiingiza katika makundi ya udanganyifu kwa kuwa tunatafuta kipato cha ziada kwa njia isiyo halali, na mwisho wa siku ajira zetu sasa zina dhambi, dhambi ya rushwa, kutokuaminika, kuharibiana ajira.  Hii yote ni dhambi tu, hatutaki kushirikiana ili kuweza kufanya kazi kwa bidii na kukuza kipato chetu na kufanya kazi za umma kwa maslahi binafsi, na maslahi ya umma.


Bata Mzinga ni bata anayefugwa nyumbani, na ana uwezo wa kukua hadi kufikia kilo 15, ni
pambo la nyumba pia.

Kwanini namuongelea Bata Mzinga leo, nimegundua kila ninapoenda katika Super Markets kubwa nakuta nyama ya bata hawa inauzwa na tena bei kubwa tu, mfano mimi nilinunua kifaranga cha bata mzinga kwa shilingi 25,000 walikuwa watano ambayo ni sawa na shilingi 125,000.
Kwa wale wanaojua kilo moja ya bata mzinga inauzwa kuanzia shilingi 10,000 na bata mzinga ana kilo 15 ni sawa na shilingi 150,000 hivi huoni kuwa huyu muuzaji wa kilo moja moja anafaida kubwa sana kuliko wewe mkulima?

Bata mzinga mmoja mwenye kilo 12 kwa jike na kilo 15 kwa dume anauzwa hivi;
Bata mzinga jike ni shilingi 60,000
Bata mzinga dume ni shilingi 70,000
Mfano una bata mzinga 2,000, majike 1,000 na madume 1,000 unajua utakuwa una miliki shilingi ngapi?

Ukiwa na majike 1,000 wenye thamani ya shilingi 60,000 = 60,000,000
Ukiwa na madume 1,000 wenye thamani ya shilingi 70,000 = 70,000,000

Mfano ukijiingiza katika biashara hii kwa kununua bata mzinga wadogo 40 kwa shilingi 25,000 kwa kila mmoja unaweza kupata majike 25 na madume 15 kwanza ili uanze kutengeneza kizazi cha kufuga kwanza.  Chukulia mfano jike moja likitotoa vifaranga 10 x 25 = 250.  Fanya kila bata mzinga atotoe mizunguko mitano itakuwa 250 x 5 = 1,250

Sasa chukua hao watoto 1,250 nao wawe madume nusu na majike nusu 625 x 10 = 6,250.  Chukua idadi ya kwanza 40 + 250 + 1,250 + 6,250 = 7,790 unaona wanavyoongezeka kutoka 40 hadi sasa una bata mzinga 7,790 tayari hapa wewe ni milionea hizi ni sawa na shilingi 467,400,000 unazo ndani.

Bata mzinga 7,790 ukiwagawa madume na majike nusu kwa nusu utapata majike 3,895 chukua kila bata mzinga atotoe vifaranga 10 kila mmoja utapata bata mzinga 38,950


UUZAJI VIFARANGA
Hawa bata mzinga 38,950 unaweza kuuza kama vifaranga, na kila kifaranga utakiuza kwa shilingi 25,000.  38,950 x 25,000 = 973,750,000 hii ni fedha taslimu utaipata kwa kuuza vifaranga.

 Katika miaka kumi ya ufugaji wako wa bata mzinga unaweza kujikuta unakuwa bilionea kama ukiwa makini na mwenye nia kweli ya kuzitafuta pesa kwa kuwafuga hawa bata.

Leo tumeanza na bata mzinga 40 lakini tunamaliza na bata mzinga 46,740 wastani wa bata mzinga 50,000.

Kazi yangu ni kukupa changamoto mdau mwenzangu katika kutengeneza maisha ya ufugaji na fedha.  Unaweza kustaafu kazi ya kuajiriwa lakini ukaanza ufugaji na ukatengeneza hela nyingi zaidi, usikate tama.  Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, alianza madaraka mwaka 2005 jana tu tulimpigia kura kwa shangwe na vigelegele, kumbuka 2010 tena tumempigia kura na sasa amebakiza mwaka mmoja tu wa madaraka yake, je huoni kuwa jana tu imeshageuka leo? Hujachelewa bado kwa mwaka huu wa madaraka yake na mwezi huu Januari, 2014 badilika anza ufugaji nenda na malengo kama haya, nakuhakikishia nitakutafutia masoko pia, na nitakutangaza kwa moyo wangu wote. Sijui atakayenisaidia mbele ya safari.  Ila wewe utakayefuata haya ninayokuambia na ukafanikiwa usinisahau katika ufalme wako, hata kama sitakuwepo basi waangalie hata wanangu.

Ushauri wangu kwako usitake makubwa haraka nimekupa mfano wa Raisi wan chi ili uone kuwa miaka 10 ni mingi kuitaja, lakini ni michache ukibung’aa huku unangoja maisha bora na elimu yako unapanda jukwaani unalalamika pamoja na asiyena elimu, ni wakati sasa wakutoa vilivyo kichwani na kuviweka katika maandishi na vifanyiwe kazi.
Share To:

Post A Comment: