Mhe. Mohamed Chande Othman Jaji, Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania akifungua Mafunzo Elekezi kwa Mahakimu Wakazi Wapya yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.
Mhe. Paul F. Kihwelo, Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto akiwa anawakaribisha washiriki Mafunzo Elekezi kwa Mahakimu Wakazi Wapya yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.
Mhe. Sharmillah Sarwat Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania akitowa utambulisho kwenye Mafunzo Elekezi kwa Mahakimu Wakazi Wapya yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto
Washiriki wa Mafunzo Elekezi kwa Mahakimu Wakazi Wapya yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.wakiwa wanafuatilia hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo kutoka kwa Mhe. Mohamed Chande Othman (hayupo pichani)
Washiriki wa Mafunzo Elekezi kwa Mahakimu Wakazi Wapya yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.wakiwa wanafuatilia hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo kutoka kwa Mhe. Mohamed Chande Othman (hayupo pichani)
Washiriki wa Mafunzo Elekezi kwa Mahakimu Wakazi Wapya yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.wakiwa wanafuatilia hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo kutoka kwa Mhe. Mohamed Chande Othman (hayupo pichani)
Washiriki wa Mafunzo Elekezi kwa Mahakimu Wakazi Wapya yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.wakiwa wanafuatilia hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo kutoka kwa Mhe. Mohamed Chande Othman (hayupo pichani)
Mhe. Mohamed Chande Othman Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji Mafunzo Elekezi kwa Mahakimu Wakazi Wapya yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto


*****

Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman tarehe 18 Januari, 2022 amefungua mafunzo elekezi kwa Mahakimu Wakazi wapya thelathini na tano. 

Mafunzo haya yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto yatafanyika kwa muda wa siku tano kuanzia tarehe 18 Januari mpaka 22 Januari, 2022. 

Mahakimu hawa ni wale walioteuliwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama na kuapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahimu Hamis Juma tarehe 17 Januari, 2022.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo, Jaji Mkuu Mstaafu aliwaambia Mahakimu hao kuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo ni ngazi ya uongozi na hivyo wanaingia kwenye mahakama ya mwanzo kama viongozi kwa mategemeo ya kuongoza watumishi watakaofanya nao kazi waliochini yao.

 Pia aliongeza kuwa mahakama inawategemea katika kusimamia mpango mkakati na maboresho ya mahakama ili kuleta mabadiliko chanya ndani ya Mahakama.

Mhe. Othman aliwasisitiza Mahakimu hao kuwa taswira ya Mahakama ya Mwanzo kwa sasa imebadilika sana na hivyo wao pia waendelee kuibadilisha na kuifanya bora zaidi ili huduma kwa wananchi ziwe bora zaidi na kwa wakati.

“Mahakama za mwanzo ndio zinatoa fursa kubwa zaidi kwa Watanzania kupata haki kuliko mahakama nyingine zote kwa sababu zimetapakaa Tanzania nzima”, alisema Mhe. Othman.

Hata hivyo Mhe. Othman hakusita kuwakumbusha mahakimu hao kuwa makini kwenye nguzo muhimu ya uhuru wa kila hakimu na uhuru wa mahakama. Aliwasisitiza kuamua mashauri yaliyo mbele yao kwa sheria bila woga wala shinikizo.

“Watanzania wanataka Mahakama huru, inayotoa haki kwa wakati, mahakama adilifu, Mahakama ambayo ina uwezo na Mahakama ambayo haina gharama kubwa” aliongeza Mhe. Othman.

Mhe. Othman aliwaasa Mahakimu hao kujua na kufuata taratibu zilizowekwa na mahakama wakati wa uendeshaji wa mashauri hadi wanapofikia kutoa maamuzi ikiwemo taratibu za usikilizaji wa shauri na kutoa uamuzi unaoongozwa na sheria pamoja na kuweka sababu za hukumu bila kusahau kupata maoni kutoka kwa wazee wa baraza.

Kwa upande wake Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto alisema Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto ni kitovu cha mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa kada mbalimbali wa Mahakama na wadau wa sheria nchini.

Mhe. Dkt. Kihwelo aliendelea kwa kusema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Mafunzo ya Taifa ya 2013 na Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania 2021/22-2024/25, Sera ya Mafunzo ya Mahakama ya Tanzania ya mwaka 2019 ambayo inaelekeza kila mtumishi anayeajiriwa, kupanda cheo au kuteuliwa kabla hajaanza majukumu mapya apate mafunzo elekezi kwa lengo la kuboresha huduma za mahakama.

Mhe. Dkt. Kihwelo alielezea Mahakimu hao kuwa Chuo kina Mpango Mkakati wa miaka mitano wa mwaka 2018/19-2022/23, na eneo ambalo chuo limekuwa likijizatiti ni eneo la mafunzo ya aina hiyo ya kuwajengea uwezo watumishi wa mahakama.

Mhe. Dkt. Kihwelo aliendelea kwa kuwaomba Mahakimu wajitahidi sana kutoa huduma nzuri na kujiepusha na rushwa kwani kwa sasa mahakama zimeboreshwa kwa kuwa na majengo mazuri sana na hivyo basi huduma ziendane na majengo.

Wakati huohuo, Mhe. Sharmillah Sarwat, Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania ameupongeza uongozi wa Mahakama ya Tanzania kwa programmu za maboresho yanayaofanyika ikiwepo kuwekeza kwenye raslimali watu ambapo Chuo kimekuwa ikifanya kwa vitendo kuwajengea uwezo watumishi hao wa Mahakama wakiwemo Mahakimu ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi na weledi.

Share To:

Post A Comment: