Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt Festo Dugange ameagiza kufanyika uchunguzi wa mapato ya hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Monduli yakiwemo malipo ya papo kwa papo baada ya kubaini ukusanyaji wa mapato ya hospitali hiyo kuwa sio wa kuridhisha.


Amesema ufanyike uchunguzi na kutolewa taarifa  ili wale wote waliohusika na ubadhirifu huo wachukuliwe hatua za kinidhamu dhidi yao.


Dkt  Dugange amesema kwa mfano katika mwezi wa Desemba 2021 ni mara saba tu fedha hizo zilipelekwa benki kwa ajili ya kuhifadhiwa lakini pia kukiuka kwa kanuni za fedha za kutopeleka fedha benki kwa ajili ya kuhifadhiwa.

.

Aidha, ameutaka Uongozi wa hospitali ya Monduli kuongeza mapato kutoka laki tano  kwa siku hadi shilingi laki tisa kwa siku lakini pia amewataka kuongeza upatikanaji wa dawa kutoka asilimia 85 ya  sasa  hadi 95 ili kuongeza utoaji wa huduma bora za afya.

Share To:

Post A Comment: