Meneja wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Manispaa ya Singida Mhandisi Lambert Bayona  (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Ummy Mwalimu wakati akikagua ujenzi wa barabara ya mbadala ya Kindani-Mtamaa kwa kipande cha Ziwa Kindai ya kilomita 2.6  wakati wa  ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo iliyopo Manispaa ya Singida jana. Wengine ni viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Singida.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge akitoa maelezo kwa Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Ummy Mwalimu kuhusu ujenzi wa barabara mbadala katika Manispaa ya Singida.
Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Ummy Mwalimu akikagua barabara hiyo. Kutoka kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Mussa Sima na Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Muragili.
Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi (hawapo pichani) wakati akikagua moja ya darasa la Uviko-19 kati ya sita la Shule ya Sekondari Mandewa.
Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mwankoko, Seleman Ally, akitoa maelezo ya kazi mbalimbali zinazofanyika katika zahanati hiyo kwa Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Ummy Mwalimu. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Manispaa ya Singida, Anwar Milulu.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mandewa, Georgia Maghiya akisoma taarifa ya ujenzi wa madarasa ya UVIKO-19 mbele ya Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Ummy Mwalimu.
Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Ummy Mwalimu akizungumza na viongozi mbalimbali wa Manispaa ya Singida wakati akikagua moja ya darasa la Uviko-19.
Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Ummy Mwalimu akizungumza na wafanyakazi wa zahanati ya Mwankoko wakati alipokuwa akikagua ujenzi wa jengo la kujifungulia wajawazito.
Diwani wa Kata Kata ya Unyianga Geofrey Mdama akizungumza mbele ya Waziri Ummy Mwalimu kuhusu ujenzi wa barabara ya Kindai- Mtamaa.
Muonekano wa moja la darasa la Uviko-19 lilijengwa Shule ya Sekondari ya Mandewa.
Diwani wa Kata ya Mwankoko, Emanuel Daniel akizungumzia ujenzi wa chumba cha kujifungulia wajawazito. Kulia ni Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo Anwar Milulu.
Mbunge wa Singida mjini Mussa Sima akizungumza katika ziara hiyo.
Mkazi wa Mwankoko Neema Kambi akiishukuru Serikali kwa kusaidia ujenzi wa zahanati ya kata ya eneo hilo.
Mkazi wa Kata ya Mwankoko akichangia jambo kwenye ziara hiyo.
Baadhi ya Wauguzi wa Hospitali ya Sokoine wakimsikiliza Waziri Ummy Mwalimu (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa chumba cha X-Ray.
Muonekano wa chumba cha X-Ray kinachojengwa katika Hospitali ya Sokoine.Na Dotto Mwaibale, Singida


 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Ummy Mwalimu ametoka siku saba kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida kuhakikisha anapeleka Sh.26 Milioni kwa ajili ya kumaliza ujenzi wa chumba cha X-Ray katika Hospitali ya Sokoine ili kuwaondolea adha wananchi wanaokosa huduma hiyo.

Hatua hiyo imefikiwa jana na Waziri Ummy baada ya kupokea taarifa ya ujenzi wa chumba hicho na kubaini kusuasua wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja katika Manispaa hiyo ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.

"Mkurugenzi nakupa wiki moja leta Sh.26 Milioni hapa kwa sababu mapato mnayo nahitaji jengo la X-ray likamilike waoneeni huruma wanasingida" alisema Ummy.

Alisema jambo la kushangaza ni pale mkurugenzi anayehusika na vifungu anaposema hajui chochote na akahoji kwanini changamoto hiyo iwe manispaa ya Singida tu na si maeneo mengine na fedha hizo zinatolewa kidogo kidogo kama fedha za hisani.

Alisema amefurahishwa na mradi huo kwa kuwa unatekelezwa kwa fedha za mapato ya ndani lakini haiwezekani ujengwe kwa miaka mitatu mradi unatakiwa ujengwe kwa mwaka mmoja na kama ikishindikana isizidi miaka miwili ili waendelee na jambo jingine. 

Alisema fedha hizo si hisani zinatolewa na wananchi wa Singida kutokana na ushuru mbalimbali wanaolipa hivyo wanapaswa kuzirudisha kwao ili zikatatue kero zao za maendeleo.

"Mkuu wa wilaya nakuachia jambo ili ulisimamie leo ni tarehe 21 nataka mpaka tarehe 31 Desemba fedha hizo ziwe zimekwisha letwa hapa hakuna cha sikukuu fedha hizo ziwezimefika" alisisita Mwalimu.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy amewataka walimu wakuu wa shule za sekondari kote nchini  kutowawekea vikwazo wanafunzi ambao wamechaguliwa kuanza masomo mwakani kwa sababu yoyote ile hata kama hawatakuwa na sare waruhusiwe wakati walezi na wazazi wao watakapokuwa wanawatafutia.

Waziri Ummy aliyasema hayo baada ya kukagua ujenzi wa madarasa sita ya Uviko 19 katika Shule ya Sekondari Mandewa ambapo Mkuu wa shule hiyo Georgia Maghiya alisema pamoja na samani zake umegharimu Sh. 120,000,000 na kuwa ujenzi wa madarasa hayo ulianza Oktoba mwaka huu.

Katika ziara hiyo Waziri Ummy alipata taarifa fupi ya ujenzi wa jengo la kujifungulia akina mama wajawazito katika zahanati ya Mwankoko iliyopo nje kidogo ya Manispaa ya Singida.

Akitoa taarifa hiyo Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo Anwar Milulu alisema ujenzi wa jengo hilo umetumia kiasi cha fedha Sh.29,839,000 ambapo Serikali Kuu ilitoa Sh.50,000,000 na kupitia michango ya wananchi na fedha za ruzuku ya Serikali walipata Sh.11,000,000 ambazo zilikamilisha kujenga boma.

Alisema fedha za mfuko wa jimbo kupitia kwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima ilikuwa ni Sh.2,000,000 huku Mbunge wa Viti Maalumu Martha Gwau akichangia Sh.1,000,000 na wadau wa maendeleo wakichangia Sh.4,457,000 fedha zilizochangwa katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

Kutokana na michango ya wadau na wananchi zahanati hiyo imeweza kuokoa kiasi cha Sh.20,161,000 ambapo Waziri Ummy amewaruhusu wajenge nyumba ya watumishi wa zahanati hiyo.

Aidha Waziri Ummy alitembelea na kukagua ujenzi wa barabara mbadala ya Kindai-Mtamaa kwa kipande cha Ziwa Kindai yenye urefu wa Kilomita 2.6 iliyopo Kata ya Unyianga ambapo aliwapongeza viongozi wa mkoa huo hasa Mkuu wa Mkoa Dkt.Binilith Mahenge kwa kuwa na maono ya ujenzi wa barabara zingine zitakazopendezesha mji wa Singida.

Waziri Ummy aliwashauri viongozi hao kuupima mji wa Singiga na kuupanga na kuachana na makazi holela na kuupendezesha mkoa wa Singida ili uwe na miundombinu mizuri na kuwa sebure ya Dodoma watu wakichoka kufanya vikao Dodoma vikao hivyo vifanyike Singida jambo litakalosaidia kuongeza mapato na kuacha na kukusanya Sh.Bilioni 16 tu kwa mwaka.

Pia Waziri Ummy alitembelea na kukagua kikundi cha Vijana Amkeni kilichopo Kata ya Minga ambapo alihitimisha ziara yake kwa kufanya mkutano na Baraza la Madiwani wa manispaa hiyo.

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: