| MBUNGE wa Jimbo la Ulanga mkoani Morogoro Salim Alaudin 
Hasham akizungumza na wananchi mara baada ya kukabidhi matrekta matatu yenye thamani ya milioni 150 | 
| MBUNGE wa Jimbo la Ulanga mkoani Morogoro Salim Alaudin Hasham akizungumza na wananchi mara baada ya kukabidhi matrekta matatu yenye thamani ya milioni 150 | 
| MBUNGE wa Jimbo la Ulanga mkoani Morogoro Salim Alaudin Hasham kulia akiwa meza kuu kabla ya kukabidhi kukabidhi matrekta matatu yenye thamani ya milioni 150 | 
Sehemu ya Matrekta matatu aliyokabidhi Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Salim Alaudin Hasham
MBUNGE wa Jimbo la Ulanga mkoani Morogoro Salim Alaudin 
Hasham amekabidhi matrekta matatu yenye thamani ya shilingi Milioni 150 
kwaajili ya kuwasaidia wananchi kipindi hiki cha kilimo.
Akizungumza
 na wananchi wa kata ya mwanya wakati wa kukabidhi matrekta hayo Amesema
 hiyo ni moja ya ahadi yake aliyoiahidi wakati wa kampeni za uchaguzi 
wakati akiomba kura hivyo ameona afanye haraka kwani anajua uhitaji wa 
matrekta katika jimbo lake ni mkubwa.
Aidha
 Mbunge Salim amewatoa hofu wananchi juu ya Taratibu za upatikanaji wa 
matrekta hayo kwakuwahakikishia kuwa hayatakuwa na upendeleo wowote bali
 kila mwenye uhitaji atakaye toa taarifa katika ofisi yake basi 
atapatiwa kwa utaratibu maalum.
Mbunge
 Salim Alaudin ameongeza kuwa bado matrekta mengine yanaendelea kuja 
hivyo ni vyema wananchi wakayatunza haya matatu ili yatakapo kuja 
mengine yaweze kuwasadia wananchi kwa haraka na kuwawezesha kulima 
kisasa zaidi.
Wananchi wa
 Wilaya ya Ulanga kwa asilimia 80 wanategemea kilimo kwaajili ya 
kujiendesha kimaisha hivyo upatikanaji wa trekta hizo utawawezesha 
kulima kwa tija nankuwaletea manufaa makubwa bila kuwa na changamoto 
kubwa.

Post A Comment: