Na. Asila Twaha - TAMISEMI


Kufuatia maagizo yaliyotolewa na Naibu  Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. David Silinde wakati wa ziara yake ya kukagua miradi  inayosimamiwa na wakala wa barabara za vijijni na  mijini (TARURA) mnamo Julai 25, 2021 katika Halmashauri ya  Wilaya ya Bunda  Mkoani Mara ukamilishaji wa ujenzi wa daraja la mihingo katika barara ya mugeta- sirorisimba umefikia katika hatua nzuri.


Silinde katika ziara yake Wilayani humo alikagua ujenzi wa daraja la mihingo na hakuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo na kutoa mwezi mmoja daraja na vifaa kufika site ikiwa pamoja na daraja hilo kukamilika.

 

Taarifa iliyowasilishwa na Meneja wa TARURA Halmashauri ya WIlaya ya Bunda Muhandisi Kassim Shabani imesema vifaa vya ukamilishaji wa daraja ikiwa ni pamoja upatikani wa bearing umefanyika  na zoezi la umwagaji zege (Deck slab beams) umeshafanyika kwa usimamizi wa wataalam na daraja liko katika hatua za mwisho za ukamilishaji.

                                                                                  Silinde ameendelea kuwataka  Wakala wa barabara za vijinini na mijini (TARURA) kuhakikisha wanasimamia miradi ya ujenzi ya miundombinu kukamilika  kwa wakati kwani azma ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha fedha zinazotolewa zinatumika kufungua barabara zitakazowaletea wananchi faida za kiuchumi.

Share To:

Post A Comment: