Mkuu wa Wilaya ya Hanang.Janeth Mayanja (kulia) akishiriki kubeba matofali na wananchi wa Kijiji cha Lambo Kata ya Masakta mkoani Manyara wakati wakichimba mifereji jana kwa ajili ya kupitisha bomba za maji zitazoelekea katika kijiji hicho na kijiji cha jirani.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang.Janeth Mayanja (katikati) akiwa na wakina mama wakati wa kazi hiyo ya kuchimba mifereji.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang.Janeth Mayanja akichimba mifereji.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang.Janeth Mayanja (katikati) akiwa na wakina baba wakati wa kazi hiyo ya kuchimba mifereji.
Kazi ikiendelea.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang.Janeth Mayanja akichimba mifereji.


Na Mwandishi Wetu, Hanang.


 CHANGAMOTO  ya ukosefu wa maji iliyodumu kwa muda mrefu katika Kijiji cha Lambo Kata ya Masakta wilayani Hanang mkoani Manyara ina kwenda kukoma baada ya mkuu wa wilaya hiyo, Janeth Mayanja kuungana na wananchi wa kijiji hicho kuchimba mifereji kwa ajili ya kupitisha bomba za maji zitazoelekea katika kijiji hicho na kijiji cha jirani.

Wanakijiji wa eneo hilo wamemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Hanang.Janeth Mayanja kwa kuamua kuungana nao kwa ajili ya kuhakikisha.maji yanapatikana ndani ya muda mfupi katika kijiji hicho kwani tangu kuanzishwa kwa kijiji hicho huduma ya maji ilikua inapatikana kwa tabu hadi kufikia wanakijiji kushindwa kupata huduma ya maji kwa ukaribu.

Akizungumza katika zoezi hilo Mayanja alisema kuwa  usambazaji wa maji katika eneo hilo lipo chini ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira ( RUWASA) Wilaya ya Hanang ambapo alimtaka mkandarasi ahakikishe ndani ya miezi minne kijiji hicho kiwe kimepata maji.

Aidha Meneja wa RUWASA Wilaya ya Hanang Mhandisi Herbert Kijazi amewahakikishia wana kijiji wa eneo hilo pamoja na mkuu wilaya kuwa Ruwasa itahakikisha wanafanya kazi usiku na mchana na ndani ya miezi minne maji yatakuwa yanapatikana katika eneo hilo.

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: