Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene (kulia), akimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi Jinai, David Elias (kushoto) akimueleza kuhusu uchunguzi wa kimaabara wa dawa za kulevya unavyofanyika kwa kutumia mitambo ya kisasa katika Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwenye Maadhimisho ya Siku ya Dawa za Kulevya Duniani ambapo kitaifa yamefanyika katika Uwanja wa Nyerere Square, mkoani Dodoma leo. Katikati ni Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald Msabila Kusaya.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia), akimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi Jinai, David Elias (kushoto) wakati akimuonesha takwimu za uchunguzi wa dawa mbalimbali za kulevya zilizochunguzwa katika maabara za Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kipindi cha miaka sita wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Dawa za Kulevya Duniani leo tarehe 26 Juni, 2021 ambapo Waziri Simbachawene alishiriki kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ambapo kitaifa yamefanyika katika Uwanja wa Nyerere Square, mkoani Dodoma. Katikati ni Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald Msabila Kusaya.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia), akisaini kitabu cha Wageni baada ya kutembelea banda la Mamlaka wakati wa kilele cha Maonesho ya Maadhimisho ya Siku ya Dawa za Kulevya Duniani ambapo kitaifa yamefanyika mkoani Dodoma katika Uwanja wa Nyerere Square leo tarehe 26 Juni, 2021.

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto) akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald Msabila Kusaya (kulia).

Mkemia Mkuu wa Serikali, (katikati) na Msajili wa Baraza la Wafamasia, Elizabeth Shekalaghe (kulia) wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald Msabila Kusaya (kushoto) wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Dawa za Kulevya jijini Dodoma leo.

Mkemia Mkuu wa Serikali, (wa pili kulia) akimsikiliza Kamishna wa Ukaguzi na Sayansi Jinai wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Betha Mamuya (kulia) mara baada ya kutembelea banda la Mamlaka katika Maadhimisho ya Siku ya Dawa za Kulevya yaliyofanyika leo jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi Jinai wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, David Elias.

Watumishi wa Mamlaka walioshiriki Maonesho ya Maadhimisho ya Siku ya Dawa za Kulevya jijini Dodoma.

Mtumishi wa Mamlaka, Muhsin Kilonzo (kulia) akiongea na mmoja ya mdau aliyetembelea banda la Mamlaka kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya siku ya Dawa za Kulevya yaliyohitimishwa leo katika Uwanja wa Nyerere Square, Dodoma.

Kutoka kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo na Kamishna wa Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald Msabila Kusaya, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi Jinai, David Elias (hayupo pichani) walipotembelea banda la Mamlaka katika Maonesho ya Maadhimisho ya Siku ya Dawa za Kulevya yaliyofikia kilele leo jijini Dodoma.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: