Hatima ya wafanyakazi zaidi ya 50 wa Katani Limited, kampuni ya mkonge ya Tanga ambayo ilianzisha kilimo cha mkonge kwa wakulimqa wadogo, ambao hawakuingizwa na kampuni mpya ambayo imechukua shughuli zake, iko katika hali ya utata baada ya wanahisa watatu wa kampuni hiyo kukubaliana kuitangaza kuwa imefilisika.


Kwa mujibu wa taarifa ilizozipata Mwananchi hapa wanahisa watatu waliofanya makubaliano ya pamoja ni Mkonge Investments Management (MIM ambayo inajumuisha wafanyikazi wa zamani wa Mamlaka ya Mkonge Tanzania - TSA), Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Afrika Mpya . 


NSSF baadaye iliunda kampuni tanzu, Sisalana Limited kusimamia shughuli za Katani Limited. 


Kulingana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Katani Limited, Fadhili Mhina, makubaliano ya pande zote yametoa mamlaka Katani kuwaandikia barua wafanyakazi za kustaafishwa.


Hatua hiyo, kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Katani, Fadhili Mhina kuwawezesha wafanyakazi hao kudai mafao yao NSSF. 


Alikubali kuwa ni kweli kwamba Sisalana imechukua uendneshaji wa kampunj na ilifanya tathmini ya kujua ni wafanyikazi wangapi na wa aina gani wanapaswa kuendelea kufanya kazi katika kampuni hiyo. 


Katani ilikuwa na jumla ya wafanyikazi 326 katika vitengo vyao, pamoja na Tancord (223), KeS (68) na Makao Makuu (35). 


Vyanzovya habari vimebaini kuwa wafanyakazi 33 ambao walikuwa na mikataba ya endelevu na mingine inayoishia Desemba 2021 wafanyikazi kutoka Tancord hawakuajiriwa katika kampuni hiyo mpya, wakati wafanyikazi 22 kutoka KeS pia wameachwa. Pia kuna jumla ya 13 wa makao makuu pia wamekubwa na mkasa huo.


Malalamiko ya wafanyikazi, ambayo kulingana na chanzo katika kampuni hiyo, ni pamoja na kuachishwa bila kufuata utaratibu. Mengine ni malimbikizo ya mishahara,posho za likizo na posho ya usafiri.


Katani pia inakabiliwa na kesi tatu zilizowasilishwa na wafanyikazi, Kamishna Mkuu wa Kazi na Chama cha Wafanyakazi wa Mashambani na Kilimo Tanzania (TPAWU ambao pia wamewasilisha kesi kwa niaba ya wafanyikazi. 


Alipoulizwa ni wapi Katani ambayo tayari wabia wake wamekubaliana kuifilisi itapata pesa za kulipa mafao ya wafanyikazi , Mhina alisema kuwa hajui kampuni hiyo itapata pesa kutoka wapi. 


Habari ziliptikana hapa zinaonyesha kuwa Katani tayari imekabidhi mali zake kwa Sisalana, jambo ambalo litafanya iwe ngumu kwa wafanyikazi kutumia mali hizo kama njia ya kupata malipo zao kupitia kuzuia na kuziuza. 


Katibu wa TPAWU wa zamani wa Shamba la Mkonge la Ngombezi alisema kuwa wafanyakazi wana madai ya malimbikizoya mishahara ambayo ni zaidi ya milioni 46.7 ambayo haijalipwa tangu 2018.


Alijiuliza zaidi kwanini maafisa wa Katani Limited hawakuwepo wakati kampuni ya Sisalana Limited ilipokuja kuchukua mali na shughuli ya kampuni. 


"Ninasita kuamini kuwa kampuni ya umma ingekuja bila utambulisho wowote na kuwaamuru wafanyakazi kuondoka katika nyumba bila neno lolote juu ya haki zao na mafao yao," Katibu huyo alisema. 


Mwingine, Elias Thomas alisema kuwa wameachishwa ajira bila kupewa barua yoyote. Alimwomba Rais, Samia Suluhu kuingilia kati ili kuwaokoa kutoka kwa unyanyasaji na kupata mafao yao ya mwisho. 


Mwingine, David Lukindo, mlinzi wa Ngombezi alishangaa ni vipi kampuni hiyo mpya inaweza kuja kuwafuta bila uwepo wa Katani ambayo imewaajiri. 


Mchunguzi mmoja wa mambo ya kisheria hapa pia alishangaa jinsi uchukuaji wa shughuli za kampuni hiyo unaweza kufanywa na mbia mmoja kabla ya makubaliano ya pamoja ya kutangaza Kampuni kufilisika kufanywa. 


Aliuliza ni wapi wafanyakazi watakimbilia kupata mafao yao ikiwa kampuni hiyo tayari imetangazwa kufilisika. 


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikuwa ameamuru wakati wa moja ya ziara zake Tanga kwamba kampuni ambayo itachukua usimamizi wa shughuli za Katani itarithi mali na madeni ya kampuni hiyo, pamoja na malimbikizo misharahara ya wafanyakazi na marupurupu mengine. 


MWISHO

Share To:

msumbanews

Post A Comment: