Na Lucas Myovela _ Arusha.

Waziri wa Fedha na mipango hapa Nchini Dkt, Mwigulu Lameck Nchemba, leo Mei 21, 2021 ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa semina ya wanahisa wa Banki ya CRDB katika ukumimbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC Jijini Arusha.
Dkt Mwigulu pia amewapongeza Banki ya CRDB kwa kutoa elimu ya kifedha kwa wanahisa na watanzania kwa ujumla wakati Banki hiyo ikiwa inaelekea kufanya Mkutano wake Mkuu wa 26 hapo May 22,2021.

Mwigulu amesema kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa wa bank ya CRDB kwa ustawi na ukuaji wa uchumi wa Taifa la Tanzania, kwa Banki hiyo kuweza kuitendea haki kwa kuwa ni Bank inayo msikiloza mteja.
"Katika ukuaji wa kimaendeleo niwapongeze sana kwa kufanya kazi vizuri na wanahisa ambapo hadi leo mnaendelea kupata mafanikio kutokana na mikakati mbalimbali mliyo jiwekea na kutoa gawio zuri kwa wanahisa wenu". Ameeleza Dkt Mwigulu.


"Nikiwa waziri wafedha ninawaahidi sera nzuri za kifedha katika kufanikiwa kwa taasisi za fedha na nimepanga kufanya mazungumzo na taasisi za kifedha  ili tuangalie sera zuri katika ukuaji wa taasisi hizi, Tunapokuwa na taasisi zinazo endelea kufanya vizuri ni taa kwa taifa letu huko nje ya Nchi na kuweza kupata wawekezaji wengi ambao wataweza kuwekeza hapa nchini". Dkt Mwigulu.
"Nawaelekeza BOT kufanya utafiti wa ufunguaji wa matawi ya kibenki katika nje ya nchi ili waweze kulipi huko huko maana hayo mabenki yao yanamatawi huku ili kurahisisha matawi ya kibiashara na kuweza kukuza uchumi wetu na katika hili niwaombe CRBD kuungana nami kwa kuwa nyie ni Bank kiongozi, Naamini tukifungua matawi mengi tutakuwa tumetoa ajira kwa vijana wengi na huku kujisahau kunatokana na kulidhika na sifa za kisiasa". Ameongeza Dkt Mwigulu.


Pia katika swala la riba Dkt Mwigulu amesema bado riba ni kubwa kwa wananchi na kusema katika mazungumzo yake na taasisi za kifedha kikubwa watangalia namna ya mazingira rafiki katika kurekebisha hilo katika maeneo ambayo ni vikwazo kwenye mzunguko wa fedha ili kutoa unafuu kwa wananchi kwa ajili ya ustawi wa taifa.
"Ukombozi wa karne ya sasa ni ukombozi wa kiuchumi nitakaa na secta zote kuangalia namna ya kufanikisha hayo na sisi kama wizara tutaangalia yale yote yanayo takiwa kufanyika ili kuondoa vikwazo vya utendaji na udhibiti maana kwenye uwekezaji ukimchelewesha mteja tu hawezi kubaki lazima ataondoka". Ameeleza Dkt Mwigulu

"Niwapongeze pia kwa kutoa elimu ya fedha hili ni jambo muhimu katika taifa lolote lile duniani kwa ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla maana mwanchi akijua elimu ya fedha ni rahisi kuwa mtumiaji wa fedha kwa ufanisi". Aliongeza Dkt Mwigulu.


Nae kwa uoande wa Naibu Gavana wa Banki Kuu ya Tanzania Dkt Bernad Kibese, amesema anaamini jitihada za kukuza ukuaji wa fedha kwenye taasisi za kifedha na mabenki wataweza kuongeza taawatanzania wenye kutambua ukuaji wa fedha ili kukuza uchumi wa Taifa. 

"Naami jitihada za kukuza ukuaji wa fedha na tutaweza kuongeza watanzania wenye kutambua ukuaji wa fedha na kukuza uchumi wetu wa tanzania, CRDB imefanya jambo jema kuwaweka pamoja wanahisa kwa kuwapa elimu na kiukweli banki hii ni bank kiongozi na wa wanahisa wenu ndiyo wamiliki na mmeweza kufaidi mazuri ya uwekezaji". Dkt Kobesa

"Pia niwaombe mnapoendelea kutoa huduma niwaombe kiwaangalia wananchi ambao ni wengi niwaombe mzidi kuwaangalia maana wanalia sana riba za mikopo nikubwa mmno niwaombe kutoa huhuduma nzuri kwa wananchi kukuza ili kukuza uchumi". aliongeza Dkt Kibesa.


Kwa upande wake Mwenyekito wa Bodi ya Wakurugenzo wa CRDB, ALLY LAAY, ameeleza luwa bado kuna ufinyo wa muamko katika swala la hisa na uwekezaji maana wananchi wengi hawaamini katika soko la hisa.

"Ukweli ni bdao kuwa kama Taifa tunamuamko mdogo sana linapokuja swala la hisa na uwekezaji maana bado wananchi wengi hawaamini katika uwekezaji kwenye soko la hisa". Ameeleza Ally Laay.

"Ukiangalia katika soko la hisa la Dar es salaam  utagundua kuwa wastani wa hisa Milioni Moja na laki saba humunuliwa na kuuzwa kwa siku kwa thamani ya shilingi Milioni mia nne na sitini pekee ambapo takwimu zimaonyesha ni sawa na watanzania laki saba kati ya watanzania milioni hamsini na tatu ambayo ni sawa na 1.25%". Ameongeza Ally Laay.
Share To:

Lucas Myovela

Post A Comment: