Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Prof. Riziki Shemdoe amesema kuwa shule ya Sekondari ya Kibasila ni miongoni mwa shule 86 zilizokarabatiwa kupitia mradi wa lipa kulingana na Matokeo unaolenga kuoboresha mazingira ya kufundisha na kujifnzia kote nchini
Prof. Shemdoe ameyasema hayo leo kwenye hafla ya uzinduzi wa magari 184 kwa ajili ya ufuatiliaji katika shule za Msingi kwenye Halmashauri zote nchini iliyofanyika katika shule ya sekondari ya kibasila Mkoani Dar es salaam.
Akifafanua kwanini walichagua uzinduzi wa magari ufanyiwe hapo amesema kuwa shule ya Sekondari ya Kibasila ilijengwa mwaka 1951 na kuanza kutumika kama sekondari mwaka 1979 na ni moja ya shule ambayo imekarabatiwa kupitia mradi wa lipa kulingana na matokeo
Amefafanua kuwa Lengo kuu la kuchagua eneo hilo ni kuonyesha juhudi kubwa iliyofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuboresha miundombinu ya shule ikiwemo ukarabati wa shule kongwe.
Amesema kuwa pia eneo la uzinduzi limepambwa na mjasiriamali mmoja wa wanufaika wa nikopo ya asilimia kumi inayotolewa na Serikali katika Manispaa ya Temeke hii inaonyesha utekelezaji wa Sheria unaofanywa na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuhakikisha wananchi wanajikwamua kiuchumi.
Amesema pamoja uzinduzi wa magari pia kuna ukarabati wa shule umefanywa kwa ajili ya kuhakikisha wanafunzi wa Kitanzania wanapata mazingira mazuri ya kujfunzia.
Post A Comment: