Muandaaji wa Mashindano ya Rede 2021 Nassoro Makau ambaye pia ni Mkurugenzi wa Five Borthers akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuelekea fainali za Mashindano hayo kesho kushoto ni Afisa kutoka Idara ya Usimamizi Tanga Fresh Bakari Mohamed na anayefuatia ni Mratibu wa Mashindano hayo Zaituni Mango kulia ni Meneja Masoko  na Mauzo wa Kampuni ya Anjali Soda Factory Saa Mumy Mohamed
Muandaaji wa Mashindano ya Rede 2021 Nassoro Makau ambaye pia ni Mkurugenzi wa Five Borthers akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuelekea fainali za Mashindano hayo kesho kushoto ni Afisa kutoka Idara ya Usimamizi Tanga Fresh Bakari Mohamed na anayefuatia ni Mratibu wa Mashindano hayo Zaituni Mango
Meneja Masoko  na Mauzo wa Kampuni ya Anjali Soda Factory Saa Mumy Mohamed akizungumza wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari leo kushoto Muandaaji wa Mashindano ya Rede 2021 Nassoro Makau ambaye pia ni Mkurugenzi wa Five BorthersMratibu wa Mashindano hayo Zaituni Mango akizungumza wakati wa mkutano huo

Msemaji wa Kampuni ya Five Brothers  Hamis Kanda akizungumza wakati wa mkutano huo
MKURUGENZI wa Arbab TV akiuliza swali wakati wa mkutano huo
 

MASHINDANO ya Rede 2021 yameunga mkono kwa vitendo juhudi za Rais Dkt John Magufuli za kuwawezesha wanawake katika kujikita kwenye ujasiriamali ili waweze kujikwamua kiuchumi wao na jamii zao.

Fainali ya Mashindano hayo huchezwa kila mwaka mkoani Tanga yanayoandaliwa na Kampuni ya Five Brothers Intertainment itafanyika kesho kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani Jijini Tanga  huku mgeni rasmi akitajwa kuwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurahaman Shillow.

Hatua hiyo inatokana na kwamba baadhi ya zawadi ambazo zinatolewa kwa washiriki hao kama chachu ya kwenda kuanzisha shughuli ndogo ndogo za ujasiriamali ambazo zitawezesha kujikwamua na kupata kipato halali na hivyo kuondoa utegemezi kwenye jamii zao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo,Muandaaji wa Mashindano hayo,Nassoro Makau ambaye pia ni Mkurugenzi wa Five Borthers alisema kwamba mashindano hayo yaliyoanza mwaka 2017 yameibua wakina mama wengi ambao kwa sasa wanaendelea na shughuli za ujasiriamali.

“kesho Jumapili ni Fainali za Mashindano hayo na tunatarajia mgeni rasmi kuwa Meya wa Jiji la Tanga na wageni waalikwa kushudu fainali ambapo bingwa mpya atatangazwa”Alisema Mkurugenzi huyo

Alisema kwamba zawadi zitatolewa kwa mshindi wa kwanza mpaka wa sita ikiwemo wa sabu mpaka 11 wanazawadi zao na wa tano mpaka 11 watakapat bidhaa kutoka Kampuni ya Azam soda na cheti.

Muandaaji huyo alisema mshindi wa kwanza atapata kombe kubwa lenye hadhi ya kimataifa na kitita cha pesa taslimu 150,000 watapata medali za dhahabu,watapata ngano kilo 25 kutoka kwa AA Shehoza Limited na mafuta lita 10 ambazo zitawezesha wajikite kwenye ujasiriamali ikiwemo soda ,

Alisema mshindi wa pili atapata fedha taslimu 100000,medali za `Silver,ngano 15kg,soda na maji kutoka Anjari huku mshindi wa tatu fedha taslimui 70,000 ,mafuta,ngano 10g ,soda,cheti na maji   na maziwa watapata.

Hata hivyo alisema washindi wengine watapata fedha ,ngano mafuta,cheti soda huku mchezaji bora  atapata fedha taslimu,kikombe kidogo na mwaka huu mhamasishaji bora atapata ,timu yenye nidhamu,walikuwepo nje wanaweza kuona shindano hilo moja kwa moja.

Awali akizungumza katika mkutano huo Meneja Masoko  na Mauzo wa Kampuni ya Anjali Soda Factory Saa Mumu Mohamed alisema wameamua kudhamini ili kuweza kuunga mkono tamaduni za Tanza za mchezo wa rede.

Alisema pia wamedhamini ili kuenzi tamaduni za Tanga na wamedhamini kupitia maji yao ya kiu na maji ambayo yanatengeneza Tanga huku akieleza mipango yao ni kuendelea kudhamini msimu unaokuja wanatarajia kuongeza nguvu kubwa ya udhamini.

“Lakini sisi kama Ajali tunaweza kuona namna nzuri ya kuwasaidia kuwawezesha wanawake wanaoshiriki mashindano hayo kupata mitaji ambayo itakuwa chachu kubwa kwao kufikia malengo yao”Alisema

Timu ambazo zitacheza fainali hiyo ambayo itachezwa kesho Jumapili ni Tanga Kwanza ambaye ni Bingwa Mtetezi kugombea kombe hilo ambaye atacheza na

 

mwisho

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment:

Back To Top