Chama Cha Msalaba Mwekundu mkoa wa Arusha (red Cross society)kimefanya uchaguzi wa kuziba nafasi za uongozi ndani ya chama hicho
Nafasi hizo ni pamoja na mshauri wa mafunzo mshauri wa maafa na habari mshauri mipango na maendeleo mshauri wa jinsia na nafasi ya makamu mwenyekiti wa red Cross mkoa wa Arusha
Akiongoza uchaguzi huo katibu mkuu wa red Cross taifa Julia's Kejo amewataka viongozi waliochaguliwa kutumia vyema nafasi zao katika kusaidia jamii kupata uduma ya kwanza
Katibu amesema kwamba viongozi hao wanapaswa kusaidia pale majanga yanapo tokea pamoja na kuongeza wanachama wa red cross kuwa wengi kuimarisha chama hicho kufikia malengo ya kujiendesha chenyewe
''Napenda kuona chama hiki kinafika mbali sana kwani Mkoa huu wa Arusha unaanzia herufi A hivyo mambo yote ya maendeleo katika chama hiki yanapaswa kuwa mbele hususani kuifikia jamii yenye uhitaji wa kupata huduma ya kwanza" alisema Katibu kejo ,,
Wakizungumza Mara baada ya kutangazwa kushinda nafasi zao viongozi waliochaguliwa wameleeza kufanya kazi na uongozi uliopo madarakani na kazi kubwa walionayo ni kuimarisha matawi katika Wilaya zote za Mkoa wa Arusha kuwa na nguvu ya kutoa huduma
Baadhi ya wajumbe wa (nec)wa chama hicho cha msalaba mwekundu akiwemo Doctar Christopher Nzella ambaye ni mhamasishaji mkuu wa chama na felician mtahengerwa mjumbe na mwenyekiti wa mahafa red cross taifa kwa pamoja wamesema kwamba wanategemea kuona viongozi walio patikana wakiwa na maono ya kupambania chama katika kufikia malengo ya umoja kuanzia kazi ya tawi Wilaya Mkoa na taifa kukitangaza chama hicho.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Red Cross mkoa wa Arusha Dora Samson amewataka wajumbe na viongozi walio chaguliwa kuacha tofauti zao ikiwemo makundi ya kurudisha nyuma chama hicho na kuwa pamoja katika kusaidia jamii.
Amesema kabla ya uchaguzi huo kufanyika kumekuwepo na makundi ya wanachama kugawanyika kila moja kumuunga mkono mgombea wake hivyo ametoa rai kwa wanachama kuvunja makundi na kukijenga chama
Makamu Mwenyekiti aliyechaguliwa Musa Luambano akiongea kwa niaba ya viongozi wenzake waliochaguliwa ya amesema kwamba Mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi na kuchaguliwa malengo ni kuhakikisha chama hicho kinakuwa na miradi yake inayojiendesha
Uchaguzi huo umefanyika Mara baada ya nafasi kuachwa wazi na wajumbe wa red Cross katika mkoa wa Arusha Mara baada ya kukosa wagombea katika kipindi Cha nyuma ulipofanyika uchaguzi mkuu mwaka 2019
Home
Unlabelled
RED CROSS ARUSHA YAFANYA UCHAGUZI KUJAZA NAFASI ZILIZOKUWA WAZI
Post A Comment: