NA HERI  SHAABAN

MKUU wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema  ameisimamisha Kampuni ya Upimaji aridhi ya Dimwe ili kupisha uchunguzi kufuatia Kampuni hiyo ambayo imepewa tenda ya upimaji  imepokea fedha za wananchi kata ya Majohe  bila kutoa risiti za Serikali.


Mkuu wa wilaya Mjema alisimamisha kampuni hiyo katika ziara yake kata ya Majohe ya kupokea kero za wananchi.

"Afisa Aridhi wa Ilala nakuomba ufanyie uchunguzi kampuni ya Dimwe kwanini ikusanye fedha za upimaji bila kutoa risiti za mashine? alisema Mjema.


Mjema alisema mara baada uchunguzi kukamilika wilaya tukijilizisha ndio itaendelea na kazi ya urasilimishaji aridhi katika kata ya Majohe.

Ameagiza kampuni zingine ambazo zipo wilaya ya Ilala  za urasimishaji makazi kufuata taratibu na sheria za Wizara ya Ardhi  .

Awali wananchi walikuwa wakirasimishiwa makazi yao kwa kupimiwa kwa gharama ya shilingi 300,000/= kwa wananchi waliokuwa pamoja baadae Serikali ilishusha gharama za urasimishaji makazi sasa hivi kila mwananchi kupima shilingi 150,000/=

Kwa upande wake Afisa Ardhi halmashauri ya Ilala  Burton Rutta alisema maagizo yaliyotolewa na Mkuu wa Wilaya kuhusiana na kampuni ya Dimwe atafatilia na kuyafanyia kazi mara baada uchunguzi  kukamilika watakabidhi taarifa.

Naye Mtaalam wa Kampuni ya Dimwe Athumani Mauld alisema kampuni yao imepewa tenda katika Mitaa miwili Mtaa wa Viwege na Mji Mpya kila Mwananchi alikuwa akipimiwa eneo lake kwa shilingi 180,000/=  na Wazee bure wakazi walikuwa wakitoa fedha kwa awamu wa tatu.

Afisa Afya Mazingira Ilala Pius Mwalupembe alisema halmashauri ya Ilala tayari imetangaza tenda kwa Wakandarasi wa Usafi lakini amna vikundi vilivyoomba kuchukua tenda za usafi .

Mwalupembe alisema katika manispaa ya Ilala kama vikundi vipo vina uwezo vichukue fomu kuomba tenda za ukandarasi wa usafi ili wapate fursa .

Aliagiza vikundi vya Jukwaa la Wanawake ambao wana uwezo wa kusimamia tenda hizo wachangamkie fursa watapewa tenda wachangamkie zabuni ikitangazwa tena.

MWISHO
majohe ziara ya Mkuu wa wilaya Ilala
Octoba 24/2019
Share To:

msumbanews

Post A Comment: